PreGE2025 Rais Samia akihutubia na Kuhitimisha Shughuli za Bunge la 12, Dodoma July 27, 2025

PreGE2025 Rais Samia akihutubia na Kuhitimisha Shughuli za Bunge la 12, Dodoma July 27, 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuhutubia na kufunga Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukio hilo litafanyika leo Juni 27, 2025 bungeni jijini Dodoma ambapo baada ya kufunga Bunge hilo hatua hiyo itaruhusu kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Updates. Rais Samia

Rais Samia ametoa pongeza kwa Spika wa Bunge, Naibu Spika na Viongozi wote ambao wamefanya kazi kwa pamoja tangu amekuwa rais wa awamu hii ya sita. Aidha Rais Samia ametoa pole kwa familia ya viongozi ambao walifariki dunia akiwemo Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli.

Katika historia ya nchi yetu wewe ni mwanamke wa pili kushika wadhifa huu katika mhimili wa kutunga sheria, hakika hujatuangusha wanawake wenzio.

Uzoefu wako wa kitaifa na kimataifa umekuwa chachu inayohakikisha kazi hii inafanyika kwa viwango vya juu, hivyo kuendelea kulijengea heshima Bunge letu,” amesema.

Amempongeza kwa kutekeleza majukumu hayo sambamba na majukumu yake ya Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Kule nako umeweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, tunakupongeza sana kwa kuitumikia nafasi hiyo,”

"Nchi yetu iko salama, mipaka yetu iko salama na imara...jeshi limeendelea kutimiza ipasavyo kazi yake ya kulinda mipaka ya nchi yetu".

Pongezi nyingi sana kwa jeshi la polisi kwa kazi kubwa na nzuri wanaifanya, kasi ya kuabaini wahalifu kuwakamata na kuwapeleka Mahakamani, Lakini naangiza jeshi la polisi kukomesha matukio ya watu kupotea.

Mchakato wa katiba mpya ni miongoni ya ahadi ambazo zinaonekana katika ilani ya CCM ya mwaka 2025- 2030 hivyo ni kusema kwamba utekelezaji utafanyika katika kipindi kijacho.

Niseme kuwa tume uhuru ya taifa ya uchaguzi itatangaza hivi karibuni tarehe ya siku uchaguzi , zoezi la uandikishaji limeshakamilika. Sote tumeshuhudia mwitikio mzuri wa wananchi kujiandikisha, tunatumaini kuwa tume itatutangazia watu waliojiandikisha.

Rais Samia uhuru wa vyombo vya habari na watu kutoa maoni umeongezeka kwa kiwango kikubwa.

Ongezeko la ukusanyaji wa mapato ya ndani yameongezeka kwa mwezi kutoka shilingi trilioni 1.51 mwezi November 2020 hadi Trilioni 3.09 mwezi March 2025 ikiwa niongezeko ya asilimia 104.

Kukua kwa deni la taifa hakutokani tu na mikopo anayoomba yeye peke yake, bali fedha madeni mengine ni mikopo iliyoombwa na maraisi wa awamu zilizopita.

Mimi nimetumia takwimu kwa yaliotendekea kwa kipindi hiki cha miaka 4

Chura Kiziwi is a self-aggrandizement freak. Ni Rais gani mwingine katika historia ya nchi yetu amewahi kuwa na mpambe (ADC) mwenye cheo cha zaidi ya colonel? ADC typically ni mjeda mwenye cheo cha lieutenant colonel (kwa vyovyote vile sio zaidi ya colonel).

Kwa kawaida, ADC akipanda cheo na kuwa brigadier, anarudi jeshini. Huyu kenge alimpandisha ADC wake cheo, lakini akambakiza kuendelea kuwa ADC ili yeye aonekane kuwa ni mtu wa maana sana.
 
Rais Samia amesema,"Bunge linafungwa lakini sheria lazima zifuatwe. Kumbukeni Chalamila yupo."

Sijui kwa nini Rais amesema hivyo.

Chalamila nadhani alifukuzwa kazi( na Magufuli labda) halafu alikuwa in the wilderness, alikuwa na mental confusion,I believe,na sometimes alikuwa anahudhuria maombi..

Ilianza Chalamila alivyokuwa Mkuu wa Mkoa wa wapi, sikumbuki, alipokuwa anawabeza waganga wa kienyeji, anasema wafufue mtu halafu ndio atawaamini..

Halafu akapewa ukuu wa Mkoa Dar na Rais akawa anasema, Chalamila ulikuwa una matatizo lakini sasa nadhani umetulia.

Lakini juzi nilikuwa namsikia mtu anaongea, anasema,"Nilimuona Chalamila siku moja, alikuwa,vipi sijui. There followed,some unflattering remarks,kwamba labda Chalamila hakuwa katika hali nzuri. Alikuwa anaongea,I was not interested in what was being said. Lakini nadhani ilikuwa inahusiana na zile siku ambazo Chalamila alikuwa in the wilderness. Surely naweza kuuliza walikuwa wanaongea nini,it was just two days ago. But what for? Ni makosa kuuliza when you are asking about evil .
 
Hongera kwake
Hongera amefanya nn sasa cha ajabu?!
Chawa bhn, yaani mtu anatimiza wajibu wake kikatiba unampa hongera...ni sawa na mtu akusifie hongera kwa kuny.a mkuu!!
Huyu Mama anajitahidi Speech, huchoki kumsikiliza
Wew ni muongo na mnafki, bila shaka ni chawa...ktk marais tuliopata kuwa nao huyu mama ndio mwenye hotuba nyepesi kuliko wote...tena akiwa anatoa hotuba bila kusoma alichoandaliwa ndio hewa kabisaaa!!
 
Back
Top Bottom