Rais Samia akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU 2023/2024 Ikulu Dar, Machi 27, 2025

Rais Samia akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU 2023/2024 Ikulu Dar, Machi 27, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais Samia akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU 2023/2024 Ikulu Dar es Salam Machi 27, 2025



Aliyoyasema Mkurugenzi wa TAKUKURU - Crispin Chalamila

Tanzania Yapanda Katika Viwango vya Kupambana na Rushwa


"Taarifa ya Transparency International kwa kutumia kiashiria cha Corruption Perception Index ilitolewa Tareh 11 February 2025 imeonesha kwamba Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi cha vitendo vya rushwa kati ya nchi 10 za Afrika Mashariki"

"Taarifa hii inaonesha kwamba kwa mwaka 2024 Tanzania imepata alama 41 juu ya 100 na kushika namba 82 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti ukilinganisha na alama 40 kati ya 100 ilivyokuwa mwaka 2023 ambapo tulishika nafasi ya 87"

TAKUKURU Yarejesha Bilioni 6.8 za Ushuru na Kubaini Kasoro Katika Malipo ya Kodi

"Ushuru ulikusanywa katika maeneo ya Minada, Masoko na maeneo mengine ya Halmashauri ya Ilala kiasi cha Tsh. Bilioni 6.8, lakini Wakusanyaji wa Ushuru hawakuwasilisha Fedha hizo Benki, TAKUKURU ilifuatilia na Fedha hizo zimefanikiwa kurejeshwa na kuwekwa katika Akaunti ya Mfuko Mkuu wa Jiji la Ilala"

"Uchambuzi wa TAKUKURU umebaini Halmashauri 52 kati ya 101 zilizofikiwa zinakata Kodi ya Zuio kutoka kwa Wazabuni mbalimbali, kati yao Halmashauri 41 zinawasilisha Kodi kikamilifu na zilizosalia (11) zinawasilisha Kodi pungufu"


Miradi ya Trilioni 11.48 Yachunguzwa, Kasoro Kwenye Sekta ya Ardhi Zatajwa

"Uchambuzi umebaini changamoto zinazokabili Huduma ya Sekta ya Ardhi, upungufu wa rasilimali Watu na Fedha, Mifumo ya TEHAMA kutosomana, kutoa namba ya malipo kwa umilikishaji ardhi kwa zaidi ya mtu mmoja, kupokea malipo ya umilikishaji ardhi kwa zaidi ya mtu mmoja na utendaji hafifu wa baadhi ya Watendaji"

"TAKUKURU imefanya ufuatiliaji katika Miradi 1,773 yenye thamani ya Tsh. Trilioni 11.48, lengo la ufuatiliaji ni iwapo fedha zilizotengwa ilitumika kulingana na Mikataba ya kazi na Sheria ya ununuzi na UjenziTAKUKURU ilibaini kutozingatiwa kwa Sheria za ujenzi, kwa mujibu wa Mikataba kwa baadhi ya miradi na ucheleweshwaji wa malipo ya Wakandarasi"

TAKUKURU Yakamilisha Uchunguzi wa Majalada 728 ya Rushwa

"TAKUKURU imekamilisha uchunguzi wa majalada 728 ya Rushwa na kuwezeshwa kuchukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa Sheria, kati ya hayo 17 ni ya Rushwa kubwa yanayohusisha thamani ya Tsh. Bilioni 1 na kuendelea"
 
Hii ripoti ya TAKUKURU huwa muhimu sana, tatizo kubwa inamezwa kwa CAG hivyo kupoteza mvuto.
 
Hao Takukuru wangekuwa wana follow the Money lazima kuna Madalali wangekuwa na la kujibu ila ndio hivyo haya mambo ni cosmetics tu...

 
Rais Dkt. Samia kupokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji kazi wa Takukuru na Ripoti ya CAG kwa Mwaka wa Fedha 2023/24

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia Akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel: Ikulu Tanzania Tovuti: ikulu.go.tz
 

Attachments

  • 20250327_102800.jpg
    20250327_102800.jpg
    212.6 KB · Views: 41
Hatimae swali langu limapata jibu leo.

Hata hivyo, tutarajie business as usual.
 
Kama huyo mama yupo hapo ,basi takukuru waondoke naye. Maana amegawa rushwa ya pikipiki nchi nzima. Takukuru mkamaeni mpelekeni mahabusu huyu mzanzibari mwanamke
 
Rais Samia akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU 2023/2024 Ikulu Dar es Salam Machi 27, 2025


 
Kama huyo mama yupo hapo ,basi takukuru waondoke naye. Maana amegawa rushwa ya pikipiki nchi nzima. Takukuru mkamaeni mpelekeni mahabusu huyu mzanzibari mwanamke
Wakamuhoji kabisa, kapata wapi pesa za kununua pikipiki za Samia 2025 nyingi kiasi kile
 
Rais Samia akipokea Taarifa ya Mwaka ya Utendaji Kazi wa TAKUKURU 2023/2024 Ikulu Dar es Salam Machi 27, 2025


 
Hizi ripoti kama zitaendelea kutofanyiwa kazi basi moja ya athari ni Kushuka kwa Imani ya Umma. Kama zinaibua kero za kiwango kikubwa cha rushwa bila hatua madhubuti za kuwawajibisha wahusika, wananchi wanaweza kupoteza imani na taasisi za serikali, wakiamini kuwa hakuna mabadiliko halisi yanayofanyika.
 
Back
Top Bottom