Rais Samia akishiriki shughuli ya kuanza kujaza maji Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), 22/12/2022

Rais Samia akishiriki shughuli ya kuanza kujaza maji Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), 22/12/2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki shughuli ya kuanza kujaza maji kwenye bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) leo Desemba 22, 2022



Maharage Chande, Mkurugenzi wa TANESCO
Maji yanayopita katika mashine moja ya kufua umeme ni lita 225,000 kwa sekunde, wakati kwa jiji la Dar es Salaam lita za maji kwa sekunde ni 30,000. Hapa unaweza kuona ukubwa wa mradi huu.

Mradi huu unakadiriwa kutumia jumla ya trilioni 6.5, hadi kufikia mwezi novemba mkandarasi alikuwa amelipwa trilioni 4.5 ambayo ni sawa na asilimia 70 ya malipo yote. Fedha za mradi huu ni fedha za kodi zetu Watanzania na mkandarasi hadai.

Pia, hadi kufikia mwezi novemba mwaka huu, jumla ya wafanyakazi 12, 275 waliajiriwa ambapo kati yao Watanzania ni 11,164 sawa na 90.97%, wageni ni 1,111 sawa na 9.1%

Kikwete.jpg

Rais mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Samel Shokry,Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Misri ambaye ameiwakilisha Serikali nchi hiyo Katika zoezi la uzinduzi wa ujazaji wa maji Katika bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere JNHPP ambaoo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan atashuhudia.
Mwinyi.jpg

Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria Katika uzinduzi huo wa kukaza maji kwenye bwawa la Julius Nyerere JNHPP Leo Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.


Rais Samia anazungumza:
Mradi huu unatoa taswira kuwa Tanzania inaweza kufanya mambo makubwa, unapotaja mabwawa makubwa, hili nalo linaingia kwenye orodha hiyo, mradi huu utatuletea umeme wa uhakika.

Nimeona kazi kubwa na nzito iliyofanywa, ni kazi kubwa na yenye ubora ya viwango vinavyotakiwa. Wzo la mradi huu lilianza wakati wa Mwalimu Nyerere, ilipofika Awamu ya Tano, Nchi yetu chini ya John Pombe Magufuli tulisema liwalo na liwe katika kutekeleza mradi huu.

Nakumbuka 'sabotage' zilizofanywa, lakini marehemu akasema tunaendelea na tutafanya.

Wakati nakabidhiwa Nchi kuongoza, ujenzi wa mradi huu ulikuwa katika 37% kwa sasa upo 78%, huu ni mradi wenye faida nyingi, utasaidia kudhibiti mafuriko, utaimarisha fursa la utalii hasa eneo la Kusini mwa Tanzania na hivyo kutoa ajira za moja kwa moja na nyinginezo.

Maji yanayopita hapa ni mengi, yanaweza kusaidia maj safi na salama kwa Dar es Salaam na viunga vyake, nimuelekeze Waziri wa Maji aitaka Dawasa

Hivyo ujenzi wa Bwawa utumike kupeleka maji Dar na ikiwezekana tuyafikishe kwenye maeneo mengine yenye shida kama vile Tanga na Morogoro, hatuwezi kuendelea kutegemea Mto Ruvu kutokana na mabadiliko ya mazingira.

Makamu wa Rais alitoa maelekezo kuwa mifugo yote ambayo imeingia kwenye bonde hili iondolewe

Nataka niseme jambo moja tunaposhughulikia migogoro hii ya kuhamisha wafugaji tuzingatie Sheria na Kanuni, weledi na haki za binadamu pia zizingatiwe

Katika Wilaya moja Kilosa au jirani nah apo DC alivyoulizwa sababu za migogoro ya wakulima na wafugaji alisema ng’ombe wengi wanaoingizwa ni wa wakubwa nay eye hawezi kuwagusa.

Nasema hakuna mkubwa mbele ya sheria, hakuna mkubwa atakayetuharibia mradi huu, hakuna mkubwa atakayetuharibia rasilimali hii tuliyoijenga kw agharama kubwa

Naomba wakuu wa mikoa na Wilaya mkafanye kazi zenu, atakayeogopa wakubwa anyoonye mkono wakubwa wamshughulikie.

Wananchi, wafanyabiashara na taasisi zote wanochepusha maji katika Mto wa Rufiji wazuiwe, natambua maji haya pia yanahitajika kwa matumizi mengine ya kiuchumi na maendeleo

Kanuni za mgawano wa maji zizingatiwe, vibali vya matumizi ya maji na uwekezaji katika shughuli za uzalishaji zinazohitaji maji mengi visitolewe katika maeneo ya juu bali wawekezaji waelekezwe katika uwanda wa chini wa mradi huu.

Itasaidia kama tutaunda kamati za ulinzi wa mazingira na zipewe mafunzo.


======================

Rais Samia Atoa maagizo kwa Wizara 5 Utunzaji wa Mazingira

Na. Beatrice Sanga - MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara 5 za Kisekta Nchini ikiwemo Kilimo, Uvuvi, Maji Mazingira pamoja na Ufugaji kuketi na kutumia nafasi zitokanazo na Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere huku akisisitiza uhifadhi wa mazingira katika vyanzo vya maji vinavyo jaza Mto Rufiji kutokana na umuhimu wa Mto huo katika Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo Rufiji Mkoani Pwani wakati wa ufunguzi ujazaji maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere ambapo amesema kwa sasa Sekta zote zenye nafasi ya kuvutia wawekezaji na kutengeneza fursa kutokana na maji ya Bwawa la Mwalimu Nyerere kufanya hivyo ikiwemo Sekta ya Kilimo na Maji ambao ndio watanifaika kupitia Bwawa la Mwalimu Nyerere.

"Nazielekeza Wizara ya Kilimo, Wizara ya Ardhi na TAMISEMI na mamlaka nyingine mkapime maeneo hayo na muyaweke katika mashamba makubwa kwa ajili ya kufanya mnada wa wazi kwa wawekezaji wa uhakika katika kilimo, nawasihi pia mtenge maeneo maalum kwa ajili ya wakulima wadogowadogo hasa wa maeneo hayo yatakayokuwa na Miundombinu ya umwagiliaji maji" Amesema Rais Samia.

Aidha Rais Dokta Samia ameagiza Wizara ya Mazingira kuchukua hatua dhidi ya waharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji katika mito na maeneo muhimu ambayo yanatumika kama chanzo cha maji katika Bwawa la Mwalimu Nyerere.

"Ndugu wananchi manufaa ya Bwawa hili katika nyanja zote yanawezekana tu kama tutatunza mazingira katika vyanzo vya mabonde ya Mito inayoleta maji mabwawani hapa nataka nisisitize umuhimu wa kutunza mazingira Kwani huu mradi tumeujenga kwa gharama kubwa na kwa kujinyima vitu vingi muhimu itakuwa ni dhambi kubwa kama hautatimiza malengo yake kwa sababu ya uzembe na ubinafsi wetu kwahiyo kulinda mazingira na kulinda mradi huu Sasa ni suala la kufa na kupona" Amesema Rais Samia.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati January Makamba pamoja na Mkurugenzi wa TANESCO maharage Chande wamesema Serikali inaendelea na mipango ya muda ya mrefu ya kukabiliana na changanoto ya umeme ikiwemo kujenga mabwawa manne pamoja na kuanzisha miradi mingine kupitia Nishati jadilifu ili kukabiliana na changamoto ya umeme.

"Tupo katika kupanga mbele na ukiangalia Ile chati yetu sisi Leo hii tunajua mpaka 2040 mradi gani utaingia kwenye gridi, tumejipanga kwa muda mrefu na sio kwa muda mfupi, tunachoomba ni subira tatizo la kukatika umeme litaisha, sisi tunataka ndani ya miaka ijayo ibaki historia kwamba chini ya uongozi wako Mheshimiwa Rais ndipo ulimaliza shida yote ya umeme ya kudumu na Hilo ndilo tunalolifanya na subira tunayo na na mipango tunayo hivi Leo tunavozungumza tuna mabwawa mengine mawili ambayo tunatafutia wakandarasi” Amesema Mhe. Makamba

Katika hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi kutoka nchini Misri, Spika wa Bunge Tullia Akson , Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulahman Kinana ambapo wakizungumza katika hafla hiyo wameutaja Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kama moja ya Mradi utakao leta mapinduzi katika Sekta ya Nishati ambayo ni muhimu kwa maendeleo.

Hata hivyo pamoja na zoezi la kubofya kitufe kuashilia kuanza kujaza maji pia Rais Samia amepokea tuzo sanjari na Marais Wastaafu kutokana na kufanikisha ndoto za ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo likikamilika litazalisha Megawati 2115.

PIA SOMA

TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA


HISTORIA

 
Hakika ni hatua kubwa ya kiuchumi inafikiwa na Taifa letu. Bwawa hili ni Mhimili Mkuu wa Uchumu wa nchi yetu, Pongezi kwa Rais wetu Dr. Samia kwa kuhakikisha mradi huu mkubwa unakamilika.

Wazalendo wote tupo pamoja na Rais wetu.
 
Hakika ni hatua kubwa ya kiuchumi inafikiwa na Taifa letu. Bwawa hili ni Mhimili Mkuu wa Uchumu wa nchi yetu, Pongezi kwa Rais wetu Dr. Samia kwa kuhakikisha mradi huu mkubwa unakamilika.

Wazalendo wote tupo pamoja na Rais wetu.
Mimi nasubiri kwanza , Gesi ya Mtwara kuna hadi waliotumbuliwa mimba , na tuliambiwa maneno haya haya tu , lakini uliona kitu ?
 
Hizo familia kumi na mbili nanii atakosa kweli!!??...........ndio ni huyo huyo. Ni mtu mbadi sana
 
Tanzania hata mimi ikatokea kuitwa Mheshimiwa ghafla nageuka kuwa mtaalamu wa kila fani.
 
Namuona waziri kakomaa na mic kuonyesha shughuli na hatua za mradi kama vile yeye ndio mtaalamu wakati ni mwanasiasa tu,aache kutafuta ujiko,hautafutwi namna hiyo
Acha wivu we mfuasi wa mzilankende. Fanya ufanyavyo makambo is a very good leader if you compare him with his predecessor in that ministry.

Kama unaumia kasage wembe unywe.
 
Back
Top Bottom