Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Tulibahatika kumpata Mwalimu Nyerere. Alikuwa ni Rais mwenye maono. Alifahamu kunahitajika nini ili nchi yetu isonge mbele.
Tukumbuke aliipokea nchi ikiwa na wasomi wachache, teknolojia duni kabisa, yenye miundombinu hafifu, elimu dhaifu, viwanda vichache sana, hakuna taasisi za utafiti, n.k. Aliondoka madarakani kukiwa na shule nyingi japo siyo za kutosha, mahospitali, reli, barabara, ndege, viwanda, vituo vya utafiti, n.k.
Kubwa kuliko vyote, aliwaacha Watanzania wakiwa wamoja. Wanaopingana kwa hoja na siyo kwa makabila yao, maeneo yao au dini zao.
Kwa kuzingatia hayo, tukampa cheo kikubwa kabisa cha BABA WA TAIFA.
Bila kutarajia, tumempata Rais Mama. Kaichukua nchi ikiwa kwenye dimbwi la uonevu, udhulumaji, uabuduji wa watu, ubambikiaji kesi, utekwaji wa watu, upotezwaji wa watu, ubaguzi kwa misingi ya vyama, ubambikiwaji wa kodi na maonevu mengine mengi. Rais mwanamama, kwa yote hayo, amesema hapana. Tunachomwomba kwa sasa, asiishie tu kuyakataa na kuyazuia maovu hayo, bali aitengeneze Tanzania kwa kaisi ambacho uovu huo hautatokea tena.
Ili kuyazuia maovu hayo ya watawala dhidi ya watawaliwa, ni lazima TUPATE KATIBA MPYA INAYOJALI MASLAHI YA TAIFA KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE.
Kama Rais Samia atawaletea Watanzania KATIBA inayoangalia zaidi maslahi ya Taifa na ya watu wake wote kwa usawa, katiba inayolinda haki na mamlaka ya wananchi, basi napendekeza apewe hadhi ya kuwa MAMA WA TAIFA.