Mimi naamini kwamba kwa katiba hii na mamlaka ya Raisi chini ya katiba hii akiamua kuleta mabadiliko ya kweli hakuna mtu wa kuuzuia! Tuendelee kumuombea Mhe. Raisi Mama Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA mungu azidi kumpa hekima, busara na maono ya kulitendea mema taifa lake. Mungu azidi kumpa mawazo ya kulitumikia taifa lake mambo muhimu kuliko kufikiria maslahi ya chama chake cha kisiasa, dini yake au sehemu anakotoka.
Naomba nimkumbushe Mama SASHA kuwa amekabithiwa jukumu kubwa sana la kuongoza taifa kama kiongozi wa juu kabisa, Raisi JMT. Ni bahati kubwa sana na ni watu wachache sana katika nchi yeyote duniani wanaobahatika kufika hatua hii, hivyo ni jukumu lake binafsi kutengeneza legacy yake kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Wahenga walisema kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza! Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA anajiuza mwenyewe kwa jinsi anavyoliongoza taifa letu la Tanzania [emoji1241] kwa sasa. Wananchi tulio wengi tumejawa na matumaini makubwa sana kutokana na uongozi wake japo ni muda mfupi tangu akabithiwe kijiti cha kuliongoza taifa. Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA amepokewa kwa furaha na wananchi wengi kwa sababu anaonekana kwa matamshi mwenyewe kama kiongozi anayependa HAKI kwa wote, ni kiongozi anayeonekana kuelewa kwa dhati kabisa kuwa hii ni nchi yetu wote bila kujari dini zetu, vyama vyetu vya kisiasa, makabila yetu, nasaba zetu au jinsia. Ni kiongozi anayetupa matumaini kwa wananchi wake wote kwa maono yangu!
Angalizo kwa Mhe Raisi Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA. Naomba akasome kitabu cha Hayati Raisi mstaafu Benjamin W. Mkapa. Katika kitabu chake hicho kuna sehemu anaongelea kuhusu wanasiasa wa kitanzania kwa ujumla. Anasema alikuja kugundua kuwa nchi hii ina wanasiasa wakweli wachache sana wanaoingia kwenye siasa kwa lengo la kusaidia wananchi wetu masikini. Na hii ni kwa vyama vyote, walioko chama tawala na vyama vya upinzani. Kuhusu walioko chama tawala alidokeza kuwa walio wengi wanakuja hadi maprofesa kutoka vyuo vikuu kwa tamaa ya kuja kupata ubunge na baadae uwaziri na benefits kibao zinazoambatana mafao ya kibunge. Kwa wafanyabiashara alisema, kundi hili uingia kwenye siasa kwa lengo kubwa la kulinda biashara zao maana kwa kuwa mbunge tu ni rahisi kukutana na kiongozi yoyote wa serikali na hii ni faida ya biashara zake, kupata passport zenye hadhi ya kibalozi ili kurahisisha kusafiri nje ya nchi katika shughuli zao! Kwahiyo Mhe Raisi tunaomba atambue kuwa mtu kuvaa tu shati la kijani na kujionesha kuwa yeye ni kada wa "CCM" kindakindaki haimpi mtu sifa ya kuwa mzalendo wa kweli wa nchi hii. Baadhi au niseme walio wengi utafuta hifadhi na manufaa kwani wanajua chama tawala ndio kila kitu!
Umenena vema.
Rais Mama Samia, aitazame Tanzania, awatazame Watanzania, wanaoishi leo na watakaoishi miaka 100 ijayo, ambao hawana sauti ya kumpamba kwa sifa kemu kemu leo.
Kwa akili aliyozaliwa nayo, na hekima aliyojaliwa na atakayojaliwa na Mungu, auone unafiki wa viongozi wanaomzunguka. Ajiulize, katika hao viongozi alio nao, ni nani aliye mzalendo wa kweli?
Je, ni Mwigulu, aliyepinga kuwa TRA haionei wafanyabiashara pale Nape alipoomba ukusanyaji wa kodi ufanywe kwa weledi, lakini leo akiwa kwenye utawala wa Mama Samia, anasema, TRA inatakiwa kubadilika?
Je, ni Ndugai aliyewapinga wabunge wa upinzani bungeni kwa vile tu walisema mikopo ya wanavyuo itolewe mpaka vyuo vya chini, halafu leo yeye anatoa kauli hiyo hiyo, akijifanya ni wazo jipya?
Je, ni Majaliwa, chini ya utawala uliopita, hakuwahi kutoa neno hata moja wakati mwanahabari Azori Gwanda akipotezwa, lakini leo anasema, ole wake atakayewanyanyasa wana habari?
Katika hawa viongozi tulio nao sasa, sijamwona mzalendo hata mmoja. Kiongozi anayesimama katika anachokiamini, anayetembea juu ya maneno yake, ambaye yupo tayari hata kupoteza cheo na fedha kwaajili ya kusimamia anachoamini ni sahihi.
Je, ni Biteko, aliyeisimamia sekta ya madini na kusababisha wawekezaji wote kuondoka Tanzania, na kufurahia kuwa mabeberu wameondoka, halafu leo akitamka kuwa anataka wawekezaji?
Kwa kiasi fulani, viongozi wachache sana wa upinzani, angalao wana misimamo katika yale wanayoamini. Maana wana uwezo wa kuamka na kusema, nimeamua kujiunga na CCM, na kesho yake wakapata cheo, lakini hawajafanya hivyo, lakini ni wachache sana.