Rais Samia Akutana na kusalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli

Rais Samia Akutana na kusalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan,amekutana na kusalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli Mkoani Mwanza Wilayani Misungwi.

Ambapo Mama Mzazi huyo wa Mama Janeth Magufuli ameonekana kuwa mwenye furaha,tabasamu na bashasha kubwa sana katika uso wake.imeonyesha hajaamini kuonana ana kwa ana na mtu mwenye nafasi ya juu na Raia namba moja ,ambaye ni mkuu wa nchi, Amiri Jeshi Mkuu na kiongozi mkuu wa serikali.

Tukio hilo limewezekana kwa Mama huyu kuonana na Mheshimiwa Rais licha ya ratiba yake ngumu na kutingwa na kazi kwa sababu tu ya unyenyekevu,ukarimu na upendo mkubwa sana alio nao Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa.Ambapo amekuwa akifikika kwa Urais na watu wa matabaka yote na kuwafanya watu wajiskie fahari na kumuona ni Rais wa watanzania wote.

Mama yetu Mpendwa hana Makuu,hana kiburi wala dharau wala kujikweza wala kujiweka mbali na watu. Ni Mama na kiongozi aliyejitoa na kujitolea kwa ajili ya kuwatumikia watanzania.ni mama na kiongozi ambaye Maisha yake yanaendelea kuleta tabasamu , matumaini na nuru kwenye maisha ya wengi.

Licha ya cheo chake na madaraka yake makubwa lakini unamuona akichangamana na watu,akipanga foleni kujiandikisha kwenye daftari la kupiga kura hapo baadaye , akisalimiana na wananchi wa kawaida kabisa . Kwake uongozi ni utumishi kwa watu na ndio maana anawatumikia watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote ile na kuwa karibu nao.

Hii ndio sababu ameendelea kupendwa , kukubalika na kuungwa mkono na mamilioni ya watanzania. na kulakiwa na maelfu ya wananchi kila anapofanya ziara au kupita tu.watu wanatamani kutandika kanga na vitenge mabarabarani kama Sehemu ya heshima kwa Mheshimiwa Rais. Mama yetu Mpendwa Daktari Samia ni mtu wa watu mwenye kumgusa kila mtu mwenye kuhitaji mkono wake
Screenshot_20241013-191420_1.jpg


Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mama Mzazi wa Mama Janeth Magufuli (Juliana Stephano Kidaso) katika eneo la Kigongo Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza tarehe 13 Oktoba, 2024.
 

Attachments

  • 1728837127739.jpg
    1728837127739.jpg
    662.3 KB · Views: 11
Unaaema huyo mama hajaamini kukutana uso kwa uso na mtu ambaye ni Rais wa nchi!.Kwamba huyo mama katika maisha yake hajawahi kukutana uso kwa uso na mtu mwenye nafasi hiyo?.
 
Unaaema huyo mama hajaamini kukutana uso kwa uso na mtu ambaye ni Rais wa nchi!.Kwamba huyo mama katika maisha yake hajawahi kukutana uso kwa uso na mtu mwenye nafasi hiyo?.
Suala siyo habari za katika Maisha yake.jambo unalopaswa kufahamu ni kuwa kupata bahati ya kuonana na kusalimiana na Mkuu wa nchi ana kwa ana siyo jambo rahisi hata kidogo.inatokea hivyo kwa Rais Samia kuonana na watu wengi kwa sababu Mama ni mtu wa watu, Mnyenyekevu,mkarimu na mwenye upendo mkubwa sana na watanzania
 
Samia amekwemda Mwanza mara nyingi zaidi kwanini?
 
Samia amekwemda Mwanza mara nyingi zaidi kwanini?
Kwa sababu nako ni Tanzania na kuna watanzania kama ambavyo amekwenda maeneo yote yenye watanzania.na ambako hajafika kuna viongozi wote kuanzia ngazi ya mkoa na pia hupeleka pesa za miradi mbalimbali ya maendeleo
 
Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Naunga mkono hoja, Mama anatosha sana kiliongoza taifa letu awamu ya pili, lakini kwa vile anayepanga sio wewe, sio yeye, na sio sisi, bali ni Mpangaji, tuzidi kumuombea ili Mpangaji ampange yeye, kwasababu hata JPM alitosha sana kwa awamu ya pili, kumbe Mpangaji hakumpangia yeye bali alimpangia Samia,
Naendelea kusisitiza Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

P
 
Back
Top Bottom