Rais Samia akutana na Wagombea Urais kutoka Vyama 16 baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025

Rais Samia akutana na Wagombea Urais kutoka Vyama 16 baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025

Ndugu zangu Watanzania,

Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Anaendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa yeye ni chaguo la Mungu Aliyeinuliwa kwa Mkono wa Mungu Mwenyewe na aliyepewa kibali na Mungu kuongoza Taifa letu.

Anaendelea kuonyesha kuwa yupo kwa ajili ya ustawi wa Taifa na watanzania wote kwa ujumla wake. Kwa Hakika itatuchukua Miaka mingi sana kumpata kiongozi mzalendo na mwenye upendo wa Agape na Taifa hili

Embu soma hapa 👎View attachment 3565677View attachment 3565678

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Unyama ni mwingi mwaisa!!!

RAHISI WETU MPENDWA DAKTARI BINGWA MBOBEZI (tusiulizane maswali)
 

RAIS SAMIA AKUTANA NA WAGOMBEA URAIS WA TANZANIA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana tarehe 31 Machi, 2026, alikutana na wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akiitikia wito wao wa kufanya majadiliano ya pamoja kuhusu hali ya kisiasa na masuala ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Viongozi hao kutoka vyama 16 vya siasa nchini walimtembelea Rais Dkt. Samia na kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuimarisha maridhiano ya kisiasa, demokrasia ya vyama, amani na mshikamano wa kitaifa baada ya Uchaguzi Mkuu, pamoja na namna ya kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na kudumisha tunu za umoja wa kitaifa.

Majadiliano hayo pia yaligusia umuhimu wa kuendeleza maadili ya uongozi, uwajibikaji na siasa zenye staha, kama msingi wa kujenga Taifa lenye utulivu wa kisiasa na maendeleo endelevu.

Katika kukuza demokrasia jumuishi, viongozi hao walisisitiza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika masuala ya kitaifa na mchakato wa maendeleo, sambamba na kulinda utulivu wa kisiasa wakati wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, kwa kutambua kuwa mazingira ya amani na umoja ni msingi wa ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Sambamba na hilo, walielezea umuhimu wa kuimarisha utamaduni wa uvumilivu wa kisiasa, kuheshimiana na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau wa kisiasa, kama njia ya kuendelea kudumisha utulivu wa nchi.

Halikadhalika, walisisitiza haja ya kuendeleza mazungumzo ya mara kwa mara baina ya viongozi wa kisiasa ili kujenga uelewano wa pamoja na kushughulikia changamoto za kitaifa kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano, kwa kutanguliza maslahi ya wananchi na maendeleo ya Taifa.

Mazungumzo hayo yanaakisi dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza mawasiliano ya wazi na ya kujenga miongoni mwa viongozi wa kisiasa, kwa lengo la kuimarisha maridhiano na mshikamano wa kitaifa.

Shaaban Kissu
K.n.y. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Fazafaka ameita wacheza maigizo wake Ikulu ili kuendeleza hadaa kwa umma. Faki them, severally and jointly!
 
Maridhiano na wafuasi wa wagombea ambao hawakuona kama kuna shida ya kisiasa kabla, wakati na baada ya uchaguzi? Watu sahihi wa kufanya nao maridhiano ni Chadema maana ndo hata uchaguzi hawakushiriki na wana wafuasi. Hawa wengine waliridhika.
Kikao cha wajinga na wenye njaa utakijua tu! Lazima kiongozwe na mjinga mmoja!
 
1)mechi ilikuwa kati ya simba na yanga

2)baada ya dakika 90 za mchezo kwisha na matokeo kutoka mshindi akatangazwa.

3)mshindi wa mchezo anaenda kuridhiana na manchester united timu ambayo hata haikushiriki hiyo ligi./hayo mashindano
Hao anaokutana nao si walishiriki uchaguzi na si walishatoa tamko kwamba hawaoni tatizo lolote kwenye mchakato wa uchaguzi ulimshindisha SSH kwa 98%!
Hao hata akutane nao chumbani... Aridhiane nao kwa lolote!🤣🤣
Mtaani huku tunajua kura hazikupigwa wala kuhesabiwa wala hakuna takwimu rasmi vituoni wala kwenye tovuti rasmi ya tume kurasimisha ushindi wa ccm.
Kifupi ccm ya sasa inatapa tapa!
 
Vibaraka, njaa ya kwenye ubongo

20260401_200833.jpg
 
Back
Top Bottom