Rais Samia akutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Juni 28, 2021

Rais Samia akutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari - Juni 28, 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Jamhui ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akutana kuzungumza na waandishi wa habari Ikulu, Dar es Salaam leo Juni 28, 2021



Updates:
Deodatus Balile, Mwenyekiti - Jukwaa la Wahariri

Tangu ulivyoingia madarakani hakuna redio iliyofungiwa, gazeti lililofungiwa, mtandao au akaunti iliyofungiwa wala Mtanzania aliyefikishwa mahakamani kutokana na kutoa maoni mtandaoni. Tunakushukuru sana.

Tuna changamoto nyingi. Kwa uchache sana naomba nipitie mambo ya msingi ambayo yanaathiri vyombo vya habari ambayo naamini yote yanatugusa.

Hali ya Uchumi wa Vyombo vya Habari
Kuna baadhi ya magazeti na redio ambayo yameamua kujifunga wenyewe kutokana na uchumi ambao ni mbaya sana kwa vyombo vya habari kwa miaka 6 iliyopita. Na hii ni pamoja na magazeti ya Habari Corporation kujifunga na kushindwa kujiendesha.

Kulikuwepo kanuni ya kimyakimya kuwa vyombo vya habari vya binafsi visipewe matangazo na matokeo yake serikali ndiyo mtangazaji mkuu, vimeishia kufa kifo cha asili.

Bahati mbaya hata wale waliopata matangazo, bahati mbaya hayalipwi kwa wakati.

Tunaomba kumshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa alipokuja Morogoro kufungua Mkutano wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Mei 20, alituambia tukusanye hayo madeni yote na tuyapeleke ofisini kwake. Tumeyakusanya; jumla kampuni 8 zimewasilisha madeni na deni lipo kati ya Shilingi Bilioni 6.5 hadi Bilioni 6.8

Waziri Mkuu alisema angeangalia namna kufikia Juni 30 deni hili liwe limelipwa.

Mh. Rais, tunaomba uongezee nguvu uamuzi hu una nia njema ya Waziri Mkuu tuone kama tunaweza kuvikomboa vyombo vya habari, maana vinakufa kifo cha asili.

Tunaomba utusaidie kufuta hii kanuni ya kimyakimya ya kuvinyima matangazo vyombo vya habari binafsi

Tunaomba urejeshe utaratibu wa Serikali kutangaza na vyombo vya habari bila kujali ni binafsi au serikali.

Kwa nchi za wenzetu wameangalia hali za waandishi wa habari na vyombo vyao na wakaweka ka-stimulus package ili kuvipa ruzuku ya kuvirejeshea uhai ambavyo vinakufa. Ikikupendeza Mh. Rais, uliangalie hilo kwa hapa Tanzania.

Idara ya Habari kuna Vyombo vinne ambavyo wakati mwingine vinafanya kazi zinazofanana na ni vigumu kutekelezeka

Mbaya zaidi hilo linaloitwa Baraza Huru la Vyombo vya Habari halina chanzo cha mapato, wanasema tutatafuta kwa Wafadhili waweze kuliendesha

Nchi nyingine Baraza hili linapata pesa kutoka kwa Serikali lakini hapa kwetu kuna hoja dhaifu kuwa, likipata fedha kutoka kwa Serikali litawekwa mfukoni.

Jukwaa la Wahariri tunajiuliza, mbona Bunge inapata pesa kutoka kwa Serikali na halijawekwa mfukoni?

Kwa bahati mbaya hata Mpango wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 haina hata kifungu kimoja kwenye kurasa 42 za Mpango huo kinachoonesha jinsi ya kushirikisha Vyombo vya Habari.

Matokeo yake wanatarajia Vyombo vya Habari vitangaze Mpango huo.

Innocent Bashungwa, Waziri - Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo
Tupo kwenye hatua za mwisho kufanya vetting ili tuweze kuanzisha Bodi ya Ithibati. Pamoja na kuanzishwa huko, tutakuwa na Baraza huru la Wanahabari na Mh. Rais , Sheria hii iliangalia hili jambo ili kuweza kuleta mazingira ya Utawala Bora kwenye tasnia ya habari kama ilivyo kwenye Wizara ya Elimu tuna TCU.

Bodi hii ya Ithibati ya wanahabari ni chombo ambacho kinakuwa independent na kinatatua changamoto za tasnia ya habari kwa kupitia wadau wenyewe. Haraka iwezekanavyo tumemuomba Katibu Mkuu Kiongozi atusaidie kukamilisha utaratibu wa kupata wajumbe na lipo katika hatua za mwisho.

Samia Suluhu Hassan, Rais - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Vyombo vya Habari vina mchango mkubwa kulinda Umoja wa Kitaifa, Usalama Nchi, Kuchochea shughuli za maendeleo. Vinasaidia Kufichua Maovu kwenye Jamii ikiwemo uzembe kazini, rushwa na ubadhirifu wa mali za Umma

Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa nchi yetu

i. Vyombo vya habari kunyimwa matangazo
Hili la Vyombo vya Habari kunyimwa matangazo, sijalikuta mezani kwangu

Kuna ushindani katika kupata matangazo

Kule Zanzibar tunayo Suluhu Network TV, mpaka leo mishahara tunachanga! Hatujapata matangazo ya kuendesha kituo

ii. Madeni
Suala la Madeni, nitashirikiana na Waziri Mkuu yalipwe kidogokidogo. Lakini lazima tuyahakiki kama ni madeni halali

iii. Stimulus package
Stimulus package kwaajili ya athari za #COVID19 kwakweli ni changamoto

Tunaweza kuliangalia huko mbeleni, hata Uchumi wenyewe wa Taifa unapitia wakati mgumu

iv. Leseni kulipiwa kwa Dola
Suala la Leseni kulipwa kwa Dola hata nami naliona kuwa ni changamoto > Hatuwezi kuwa Watumwa wa Sheria tunazozitunga. Tutakaa kitako tuangalie tunakwendaje

v. Kazi ya Urais
Labda niwaambie bila kupepesa kazi ya urais ni ngumu lakini kwa sababu urais ni taasisi yenye vyombo kadhaa vinavyosaidia ndipo urahisi wake ulipo. Rais afanye kazi peke yake kama mnavyojua Serikali ina sekta kadhaa ambayo kila linalozuka linashughulikiwa

Rais anapelekewa aidha kwa maelekezo au kwa uamuzi, lakini ndani ya ofisi ya rais kuna wasaidizi kadhaa wanaosaidia kuchakata na kukupa kwa ajili ya uamuzi. Lakini niseme sio rahisi ki hivyo kwa sababu lazima ujue kila kitu kinachotokea au kilichopo ndani ya nchi ili kinapokuja kisiwe kigeni kwako

Inakuwa ngumu zaidi kama hukujipanga kuichukua

vi. Siku 100 Madarakani
Katika siku 100 nilizokaa madarakani, kuna ambayo nami nimesikia yamefanyika nami nikashangaa

Tumehimili vishindo; thamani ya pesa yetu bado iko imara na mfumuko wa bei umedhibitika

Tuna akiba ya takribani Dola Bilioni 4.97 hivyo uhakika wa kujiendesha miezi 6 upo

vii. Idara ya Habari kwenda Wizara ya Teknolojia ya Habari
Kuhusu pendekezo la Idara ya Habari iende kwenye Wizara ya Teknolojia ya Habari, tutakaa tuyaangalie kwa pamoja

Tukiwa na 'justification' ya kutosha basi tunaweza tukaamua vinginevyo

viii. Kukabiliana na Covid 19
Nataka niwe mkweli, Tanzania tuna wagonjwa katika hili wimbi la tatu. Mpaka taarifa nilizozipata juzi, nadhani kuna wagonjwa kama 100 na, kati yao si chini ya 70 wako kwenye matibabu ya gesi, wengine wako kwenye matibabu ya kawaida

Watanzania wengine wameshakwenda kuchanja wapo waliokwenda Dubai, Afrika Kusini, kwa hiyo tukasema chanjo zije ili watu wachanje kwa hiari,

Juzi tulikaa kwenye baraza la mawaziri tukakubaliana kwamba twende kama dunia inavyokwenda,” amesema Rais Samia na kuongeza kwamba tayari Tanzania imewasilisha maombi ya kupata chanjo.

Tumeamua tukubali chanjo kwa walio tayari

Tanzania tumeingia kwenye COVAX community

Wataalamu wetu wanafanyia kazi Chanjo ipi inafaa kwa Watanzania

Kuna mashirika mengi wamejitokeza kutaka kusaidia Watanzania lakini lazima wataalamu wetu ndio watoe ushauri kitaalamu

Mapambano ya Covid 19 si ya Serikali tu. Sisi kama Serikali tunahimiza yale yanayoshauriwa na wataalamu; kama unaamini kwenye kupiga nyungu - wewe piga. Kila mmoja atekeleze wajibu wake. Jikingeni sana na wakingeni watoto

Tuna $470m za kuagiza chanjo na vifaa vya kupambana na Covid 19

ix. Teuzi za viongozi
Kwenye teuzi hatuwezi kumchukua kila aliyesema “CCM OYEE”

Kwenye teuzi kuna waliokuwa wapinzani, kuna wasiokuwa na vyama na hata wana CCM. None is left behind

x. Uwekezaji nchini
Wawekezaji waliosajiliwa kuanzia Machi hadi Mei ni mara mbili ya waliojitokeza kipindi kama hiki mwaka jana

Naendelea kufungua milango ya kukuza uchumi

xi. Katiba Mpya na Mikutano ya Kisiasa
Kama inavyosemwa nimeanza vizuri naomba nipeni muda nisimamishe nchi kwanza kiuchumi. Tuite wawekezaji wawekeze ajira zipatikane uchumi ufunguke halafu tutashughulikia Katiba, tutashughulikia mikutano ya hadhara wakati ukifika

Kwa sasa tunaruhusu mikutano ya ndani ya vyama na wabunge wapo huru kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao si maeneo ya wengine, ile yeyeee ingieni, hili naomba sana Watanzania tujipe muda tufanye uchumi wetu, sisemi katiba si ya maana lakini naomba mnipe muda kwanza nisimamishe uchumi kisha tutatizama mengine.
 
Ha
Ndio maana tumepanga kuandamana nchi nzima ili uchaguzi mkuu 2025 usifanyike. Bora hela za uchaguzi zitumike kujenga shule, barabara au vyuo vikuu.
Hayo ni mawazo yako nje ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom