Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo Rais Samia Suluhu atapokea kombe la COSAFA Ikulu ya Dar es Salaam kutoka timu ya wanawake, Twiga Stars ililipata kombe hilo nchini Afrika Kusini baada ya kuishinda timu ya wanawake ya Malawi.
Kuwa nami kwa yatakayojiri
=========
Anaeongea sasa ni Katibu mkuu, Dkt. Hassan Abbas na anatambulisha wageni waliohudhuria ikiwemo watu wa tasnia ya mpira na tasnia ya urembo(Viziwi). Abass anasema watu wa mpira wanasema mama Samia anupiga mwingi na wasanii wamemtuma aseme ananata na biti kwa kufanya kazi kubwa.
Wallace Karia(TFF): Mheshimiwa Rais, hii ni heshma kubwa kwa wachezaji na viongozi wanaosimamia michezo. Timu hii ilishinda michezo yote mitano iliyocheza, wachezaji walipambana na kurejea na kombe hilo kama walivyotuahidi. Tunakushukuru kwa kupunguza idara ya habari kwenye wizara ya michezo, tunaamini itaongeza ufanisi.
Katika kipindi cha uongozi wangu tumechukua makombe kumi na safari hii limeongezeka la tano la wanawake na huu ni uthibitisho kuongeza nguvu kwa soka la wanawake ulikuwa uamuzi mzuri na matunda tunayaona.
Pamoja na mafanikio yanayopatikana, bajeti yetu ya kuhudumia timu za taifa ni ndogo sana, tunayo changamoto kubwa ya usafiri kwenda nchi wanazocheza zao za nje lakini tukushukuru kwa kauli yako, wizara imetusaidia.
Kwa taarifa, kwenye mashindano ya kombe la dunia, sisi ndio tunaongoza kwenye group letu tukifuatiwa na Benin kwahiyo tuna nafasi kubwa ya kuweza kushinda na hii hatua tuliyofikia hatujaweza kufikia toka tunapata uhuru.
Ni matarajio yetu tutaweka historia hiyo lakini pia historia itawekwa katika kipindi chako, Mwenyezi Mungu ikimpendeza tutakutana hapa tufurahi kwa mafanikio haya.
Samia Suluhu: Naomba nizungumzie jambo la unyanyapaa katika soka, japo nasikia umepungua baada ya mimi kuwasemea, fedha za Soka la wanawake wapewe na sio zihamishiwe kwa Wananume
Samia Suluhu: "Kipekee nakupongeza Zubeda Mgunda, hususan kwa kudaka michomo na kupangua mikwaju ya penati. Ulipokuwa unadaka zile penati taswira zilizokuwa zinanijia ni kama golikipa Fabian Barthez, Van der Sar na nyumbani ilinijia taswira ya Juma Pondamali na Hamis Kinye." Rais Samia Suluhu
Samia Suluhu: Nilikuwa namwangalia mwanangu Fatma issa, hongera sana pamoja na hijabu yake lakini amecheza vizuri sana kwahiyo msitudharau tunaovaa Hijabu"Samia Suluhu, Rais wa Tanzania
Rais Samia Suluhu: Kuna vijisenti vya mafuta vitapitapita huko kwa wachezaji na makocha wao, lakini huku nyuma nilikuwa nalia, nasema kuna timu ilicheza hapa Taifa Stars, wakafunga timu kuingia sijui nusu fainali, kina Hassan waksimama na wakurugenzi na Karia, piga viwanja wote.
Lakini waliokuwa wameleta makombe, kombe kabisa hili hapa sio nusu fainali, sasa leo na-revange, nitawapatia watoto wangu viwanja vya kujenga nyumba zao.
Bahati mbaya au nzuri viwanja vyote vitakuwa kule ambapo mama yenu ninapokaa, Dodoma. Najua baadhi yenu itakuwa shida kujenga Dodoma lakini kwanza pokeeni tutaona nini cha kufanya huko mbele.
Nawapa viwanja kwa sababu na nilisema siku ile, maneno yangu yakaenda kugeuzwa juu chini, nilisema vijana hawa wana-future wanamaisha baada ya wao kuacha kucheza, mchezo huu unategemea miguu na nguvu za mwili watafika pahali watachoka