Pre GE2025 Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kibajaji ni darasa la saba hajui katiba

Katiba ya CCM inatamka wazi kuwa Mweenyekiti wa CCM ndie atakuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu kumtoa mwenyekiti nje ni ukiukwaji wa katiba na ni mapinduzi ya kumpindua mwenyekiti mchana kweupe
Je katiba ya CCM inaruhusu ule mkutano kumchagua mgombea uraisi?
 
Ndio mkutano mkuu unaruhusiwa kumpitisha Rais kwa Azimio. Na pale walipitisha azimio hilo

Akisoma azimio hilo, mtoa hoja, ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mbunge wa Viti Maalumu, Ng’wasi Kamani, amesema; “Kwa kuzingatia mamlaka tuliyonayo chini ya Ibara ya 101, kifungu kidogo cha tano B cha Katiba ya CCM, kwa pamoja tunaazimia jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa ndiye mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Azimio hilo limeielekeza Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa upande wake, ikizingatia ibara ya 103 kifungu kidogo cha 12 B, kutekeleza jukumu lake hilo leo, Januari 19, 2025.​

pia Ibara ya 99 (7) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 inaeleza pia kwamba Kikao hiki cha juu kabisa ndani ya CCM na chenye nguvu kubwa kuliko Kikao chochote kile kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu
 
Rais Samia alipopendekezwa kuwa mgombea wa urais 2025, kuna mjumbe alisimama na kuwambia yeye na mwinyi inabidi watoke nje ili wapigiwe kura, ambako Rais Samia alijibu hawezi kutoka nje, kama ni kumchana basi wamchane hapo hapo, jambo ambalo linakiuka katiba yao.

View attachment 3211139
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu, Kibajaji akiwasilisha hoja ya kumtaka Samia na Mwinyi watoke ili wajumbe waamue

Yeye kuwa pale wakati anapigiwa kura ina maana ataona wote wanaomkubali na kumkataa ili baadaye alipize kisasi. Kwa mazingira hayo watu wakapiga unafki tu kukubali wote isipokuwa wachache kama Mpina walishindwa kabisa kujizuia hisia zao!

Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Kwa hicho kilichotokea ina maana Samia anatumia ushawishi wa watu fulani kufosi kuwa mgombea urais wakati wengi hawamtaki?

Kama mnakumbuka kulikuwa na kusita sita kumpitisha kutoka kwa Jakaya akiwataka wajumbe kufikiria kuhusu sheria na katiba yao inavyosema, lakini ikabrashiwa shwa shwaa kama haijasikika watu wakapishwa!

View attachment 3211140
Video Jakaya akigusia kuhusu kuzingatia sheria na kuuliza wanasheria kama wanachokifanya kipo sawa

Kuna uwezekano akatokea mwamba akachallenge maamuzi hayo kama ilivyokuwa kwa Lowassa 2015?

===

Maoni ya mdau
Kumbe ilikuwa hivi..!!!?????

Hatukufuatilia mambo yao hawa, macho na masikio yetu yalikuwa kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA

Walivyovaa tu unaweza kudhani kama watu wa maana sana, lakini kumbe ni mbwa mwitu au mafisi ktk mavazi ya kijani...

Kuna kila dalili kuwa maamuzi haya yatapingwa na kundi litakaloibuka kwa nguvu sana miongoni mwa mafisi yenyewe...

BY THE WAY, hivi inawezekana vipi sisi Watanganyika zaidi ya milioni 64 tuendelee kuongozwa na Wazanzibari wawili tena watoto wa baba mmoja (Ally Hassan Mwinyi....?)

Watanganyika ni nani katuloga aisee kiasi cha kukosa akili hivi..??
 
Ndio mkutano mkuu unaruhusiwa kumpitisha Rais

Ibara ya 99 (7) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 inaeleza pia kwamba Kikao hiki cha juu kabisa ndani ya CCM na chenye nguvu kubwa kuliko Kikao chochote kile kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu
Tatizo sio katiba au mamlaka ya kikao...

Tatizo hapa ni utaratibu wa kutekeleza takwa hilo kukiukwa...

Mfano ni kwa vipi agenda ya uteuzi na kuthibitishwa kwa wagombea u - Rais na mgombea mwenza wake iibukie hapohapo ghafla ndani ya kikao pasipo wajumbe kujua kabla kama ambavyo walikuwa wanajua agenda zingine ikiwemo kumthibitisha makamu Mwenyekiti ..??

Kuna siri gani inafichwa nyuma ya pazia kwa tendo hilo..?
 
Kumbe ilikuwa hivi..!!!?????

Hatukufuatilia mambo yao hawa, macho na masikio yetu yalikuwa kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA

Walivyovaa tu unaweza kudhani kama watu wa maana sana, lakini kumbe ni mbwa mwitu au mafisi ktk mavazi ya kijani...

Kuna kila dalili kuwa maamuzi haya yatapingwa na kundi litakaloibuka kwa nguvu sana miongoni mwa mafisi yenyewe...

BY THE WAY, hivi inawezekana vipi sisi Watanganyika zaidi ya milioni 64 tuendelee kuongozwa na Wazanzibari wawili tena watoto wa baba mmoja (Ally Hassan Mwinyi....?)

Watanganyika ni nani katuloga aisee kiasi cha kukosa akili hivi..??

Ni kukosa uzalendo. Asali. Watu wakiwa kwenye mfumo, madaraka hawajali tena maslahi ya nchi.

Wanagawanywa na hao viongozi kikabila, kidini, kikanda, kichama hata hawaoni yapi ni maslahi ya Taifa.
 
23 January 2025
Bonn, Germany

Who is Tanzania’s new opposition party leader, Tundu Lissu?​

View: https://m.youtube.com/watch?v=boP5e9pJA7E
Tanzania's main opposition party has selected Tundu Lissu as its new leader in preparation for the general elections scheduled for October. He is poised to be the presidential candidate for the CHADEMA party and is expected to compete against the incumbent President, Samia Suluhu Hassan. So, who is Tundu Lissu, and what are his prospects in the upcoming elections?
Source : DW Deutsche Welle
 
Bonn, Germany
22 January 2025

Mwelekeo wa CHADEMA chini ya uongozi wa Tundu Lissu​

View: https://m.youtube.com/watch?v=R8ox2CeOv0w
Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Tundu Lissu amemwagia sifa tele Freeman Mbowe ikiwemo kukifanya chama hicho cha upinzani kuwa kikubwa "kuliko pengine" chama tawala cha CCM, nchini Tanzania. Lissu ameyasema hayo leo baada ya kushinda nafasi ya uenyekiti wa chama hicho akimbwaga Mbowe aliyekuwa anatetea nafasi hiyo aliyokuwa akiishikilia tangu mwaka 2004. Unaiona wapi Chadema chini ya uongozi wa Lissu?

Source : DW Deutsche Welle Kiswahili
 
lucas mwashambwa toa ufafanuzi ili hawa wachochezi wakae kimya
Kile kikao, kikatiba,(ya CCM ya 1977 toleo la Disemba 2022, ibara ya 100, kifungu cha 5 c) hakikuwa cha kumpitisha mgombea urais.

Kile kikao kilikuwa cha kumchagua Makamu Mwenyekiti wa CCM.

Habari ya kupitisha jina la mgombea urais hata haikuwa kwenye ajenda, imelazimishwa tu, tena kwa kuvunja katiba ya CCM.
 
Huyu watamtosa tu mwache amalizie pesa kwa machawa badala atunze sikamsaidie huko kizimkaz kuanzia Mwakani 😂
 
Ndio mkutano mkuu unaruhusiwa kumpitisha Rais kwa Azimio. Na pale walipitisha azimio hilo

Akisoma azimio hilo, mtoa hoja, ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na Mbunge wa Viti Maalumu, Ng’wasi Kamani, amesema; “Kwa kuzingatia mamlaka tuliyonayo chini ya Ibara ya 101, kifungu kidogo cha tano B cha Katiba ya CCM, kwa pamoja tunaazimia jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa ndiye mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”​

Azimio hilo limeielekeza Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa upande wake, ikizingatia ibara ya 103 kifungu kidogo cha 12 B, kutekeleza jukumu lake hilo leo, Januari 19, 2025.​

pia Ibara ya 99 (7) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 inaeleza pia kwamba Kikao hiki cha juu kabisa ndani ya CCM na chenye nguvu kubwa kuliko Kikao chochote kile kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu
Taratibu za kikao zilikiukwa.Ilitakiwa asimamie mwenyekiti mwingine na Samia na Mwinyi watoke ili wajadiliwe.
Pia wakati wa kuanza kikao ilitakiwa waongeze ajenda hiyo kwanza ili owe sehemu ya ajenda.
 
Katika mazingira kama hayoo hususani kipindi kam hiki, ndipo unapoona umuhim wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa maslah ya taifa na sio chama wala watawala.
Maana katika mazngira kama haya fisi ndo wanajifanya farasi weupe kitrojenically.
 
Yaan vijana wa uvccm ovyo sana mpka kikwete kawambia " vijana linapozungumzwa jamboa la msingi mtulie na bbadae ndo mshike mabango" na Hawa vijana wamekua wanakurumuka sana pasipo kujua wanakurupukia nn??
Ni Vijana Wa hovyo wanashangilia chochote pasipo kuelewa
Ni aibu sana
 
Mama hajiamini na ndiyo maana anajaza wastaafu katika safu yake ndani ya CCM.
wastaafu wangapi alio wajaza maana hata wasira hakuwahi staafu nchimbi ndio kwanza ana miaka 53 haya yupi mstaafu alie mjaza.kumbuka nafasi ya makamu mwenyekiti bara kipindi cha jpm alikua mzee Mangula na alikua kastaafu na alikua karudi kijijini kwake Mtwango Njombe lkn akarudishwa kazini lkn hakukua na makelele ya hovyo
 
Rais Samia alipopendekezwa kuwa mgombea wa urais 2025, kuna mjumbe alisimama na kuwambia yeye na mwinyi inabidi watoke nje ili wapigiwe kura, ambako Rais Samia alijibu hawezi kutoka nje, kama ni kumchana basi wamchane hapo hapo, jambo ambalo linakiuka katiba yao.

View attachment 3211139
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu, Kibajaji akiwasilisha hoja ya kumtaka Samia na Mwinyi watoke ili wajumbe waamue

Yeye kuwa pale wakati anapigiwa kura ina maana ataona wote wanaomkubali na kumkataa ili baadaye alipize kisasi. Kwa mazingira hayo watu wakapiga unafki tu kukubali wote isipokuwa wachache kama Mpina walishindwa kabisa kujizuia hisia zao!

Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Kwa hicho kilichotokea ina maana Samia anatumia ushawishi wa watu fulani kufosi kuwa mgombea urais wakati wengi hawamtaki?

Kama mnakumbuka kulikuwa na kusita sita kumpitisha kutoka kwa Jakaya akiwataka wajumbe kufikiria kuhusu sheria na katiba yao inavyosema, lakini ikabrashiwa shwa shwaa kama haijasikika watu wakapishwa!

View attachment 3211140
Video Jakaya akigusia kuhusu kuzingatia sheria na kuuliza wanasheria kama wanachokifanya kipo sawa

Kuna uwezekano akatokea mwamba akachallenge maamuzi hayo kama ilivyokuwa kwa Lowassa 2015?

===

Maoni ya mdau
Kwani kuna anayetaka hasara kama hii? Sijui hata kama naye anajitaka. Hata aliyemtengeza, yaani mwenda zake, hukujua alichokuwa akitengeneza.
 
Rais Samia alipopendekezwa kuwa mgombea wa urais 2025, kuna mjumbe alisimama na kuwambia yeye na mwinyi inabidi watoke nje ili wapigiwe kura, ambako Rais Samia alijibu hawezi kutoka nje, kama ni kumchana basi wamchane hapo hapo, jambo ambalo linakiuka katiba yao.

View attachment 3211139
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu, Kibajaji akiwasilisha hoja ya kumtaka Samia na Mwinyi watoke ili wajumbe waamue

Yeye kuwa pale wakati anapigiwa kura ina maana ataona wote wanaomkubali na kumkataa ili baadaye alipize kisasi. Kwa mazingira hayo watu wakapiga unafki tu kukubali wote isipokuwa wachache kama Mpina walishindwa kabisa kujizuia hisia zao!

Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Kwa hicho kilichotokea ina maana Samia anatumia ushawishi wa watu fulani kufosi kuwa mgombea urais wakati wengi hawamtaki?

Kama mnakumbuka kulikuwa na kusita sita kumpitisha kutoka kwa Jakaya akiwataka wajumbe kufikiria kuhusu sheria na katiba yao inavyosema, lakini ikabrashiwa shwa shwaa kama haijasikika watu wakapishwa!

View attachment 3211140
Video Jakaya akigusia kuhusu kuzingatia sheria na kuuliza wanasheria kama wanachokifanya kipo sawa

Kuna uwezekano akatokea mwamba akachallenge maamuzi hayo kama ilivyokuwa kwa Lowassa 2015?

===

Maoni ya mdau
Kwa hicho kilichotokea ina maana Samia anatumia ushawishi wa watu fulani kufosi kuwa mgombea urais wakati wengi hawamtaki?

Kama mnakumbuka kulikuwa na kusita sita kumpitisha kutoka kwa Jakaya akiwataka wajumbe kufikiria kuhusu sheria na katiba yao inavyosema, lakini ikabrashiwa shwa shwaa kama haijasikika watu wakapishwa!😁
 
Rais Samia alipopendekezwa kuwa mgombea wa urais 2025, kuna mjumbe alisimama na kuwambia yeye na mwinyi inabidi watoke nje ili wapigiwe kura, ambako Rais Samia alijibu hawezi kutoka nje, kama ni kumchana basi wamchane hapo hapo, jambo ambalo linakiuka katiba yao.

View attachment 3211139
Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde maarufu, Kibajaji akiwasilisha hoja ya kumtaka Samia na Mwinyi watoke ili wajumbe waamue

Yeye kuwa pale wakati anapigiwa kura ina maana ataona wote wanaomkubali na kumkataa ili baadaye alipize kisasi. Kwa mazingira hayo watu wakapiga unafki tu kukubali wote isipokuwa wachache kama Mpina walishindwa kabisa kujizuia hisia zao!

Pia, Soma: Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025

Kwa hicho kilichotokea ina maana Samia anatumia ushawishi wa watu fulani kufosi kuwa mgombea urais wakati wengi hawamtaki?

Kama mnakumbuka kulikuwa na kusita sita kumpitisha kutoka kwa Jakaya akiwataka wajumbe kufikiria kuhusu sheria na katiba yao inavyosema, lakini ikabrashiwa shwa shwaa kama haijasikika watu wakapishwa!

View attachment 3211140
Video Jakaya akigusia kuhusu kuzingatia sheria na kuuliza wanasheria kama wanachokifanya kipo sawa

Kuna uwezekano akatokea mwamba akachallenge maamuzi hayo kama ilivyokuwa kwa Lowassa 2015?

===

Maoni ya mdau
Safi sana
 
Back
Top Bottom