Rais Samia aliposema atateua vijana naona amewaibua vijana wa CCM kila kona wanashambulia jukwaa waonekane

Rais Samia aliposema atateua vijana naona amewaibua vijana wa CCM kila kona wanashambulia jukwaa waonekane

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Tumejenga Taifa la watu wa ajabu sana. Ni siku tatu toka vijana waahidiwe ajira za DC, DAS na DED zilizotangazwa na Mhe. Rais.

Baada tu ya tangazo lile vijana wa chama Cha mapinduzi wameibuka kila Kona ya nchi kutoa matamko na kukemea baadhi ya vitu Jambo ambalo awali kabla ya kauli ya Rais atukulishuhudia. Kinachotokea Sasa na kwa agenda wanazojadili unagundua wazi kwamba hakuna kijana ndani ya UVCCM anayejipanga kuwahudumia wananchi bali wanawaza kuwatawala wananchi.

Haiwezekani wazungumze vijana zaidi ya kumi Tena viongozi na wakemee wale wanaotaka Katiba mpya. Haiwezekani agenda ziwe zilezile zinazotangazwa na CHADEMA ndizo zinajadiliwa na kutolewa matamko wakati zipo agenda nyingi za wananchi. Hawa vijana wanapaswa kupewa kitchen pat, wanapwaya sana, Wanalala sana, wanazubaa sana kufikiri na inasikitisha kuona Hawa Hawa ndio Rais anategemea awateue kuliongoza Taifa kufikia uchumi wa Kati.

Mama nikuombe, waliojitokeza kuzungumza wanyime nafasi ili wajitengenezee utaratibu wakuliwazia Taifa hata Kama hakuna nafasi za uteuzi mbele yao.

Kwanini wajitokeze baada ya Tamko la Rais? Walikuwa wapi?
 
Kama hujawazoea CCM watakupa tabu sana mana hao ni WASAKATONGE NA WATU WA MASLAHI NA NDIO MAANA HAKUNA HATA MMOJA MWENYE AKILI.
 
Tena wanapinga katiba mpya naona ndio agenda kuu ya uvccm kwa sasa
 
Vijana CCM tupunguze kudemka kwa ajili ya hivi vyeo,ukidemka sana ndio unaharibu kabisa.
 
Back
Top Bottom