Rais Samia alistahili kuwa Rais wa kipindi cha mpito

Rais Samia hana kosa...

Urais si mtu tu aitwaye Rais....

Kwanini yeye ni rais ?!!

Alijiweka kutoka Kizimkazi ?!!

Wakulaumiwa si yeye...si Dr.Mpango...si Mh.Majaliwa...

Lawama tuzipeleke wapi ?!!

Taifa la KIJAMAA NA KUJITEGEMEA linafutaje taratibu njema zilizokuwa ndani ya AZIMIO LA ARUSHA?!!

Ikiwa AZIMIO LA ARUSHA lilikuwa ni bora sana ,ni kwanini lilivunjika ?!!

Ikiwa AZIMIO LA ARUSHA lilitengenezwa kwa sababu zisizo za muda mrefu ,ni kwanini "think tanks" wake walilisimika na kutuonjesha "ladha yake hiyo ya muda mfupi"?!!!

Mh.Rais Samia yuko katikati ya makundi haya mazito haswa :

-Chama chake cha CCM(wanasiasa)

-Wananchi

-Dola na chombo cha utekelezaji wa kila siku(Serikali).

WANANCHI

Kizazi kinabadilika sana...sisi wa miaka 30 naa tuliopata bahati ya malezi ya kufundishwa UADHIMU wa taifa tuna nafuu kidogo....hasa kwa wale wasio na tamaa....

Ila hawa wadogo zetu waliozaliwa miaka ya katikati ya 90 mpaka 2000 ni kizazi cha KAZI haswa....kiko katikati ya uharaka wa dunia ya sasa na mapinduzi ya TEHAMA na AKILI MNEMBA....

Wengi wa hawa hata kama wamepata bahati ya kufundishwa UADHIMU wa taifa mioyo yao imekaa "kimimi" haswa kutokana na "materialism"....kizazi hichi ni lazima kama nchi tuchukue hatua madhubuti kuwajenga vyema wao na dola letu Tanzania.

KUWAJENGA KIVIPI?!!

Je CCM kama chama tawala kiko tayari kuiishi misingi isiyotetereka aliyotuachia baba wa taifa....viongozi kusimama walipo na wasijihusishe na kutafuta MALI kwa nguvu kubwa ?!!

Hili ni gumu ? !!

Limekaa kizamani na "kimalaika zaidi"?!![emoji1787][emoji1787]

Mwenyezi Mungu alibariki taifa letu aaamin [emoji7]

#Mwenyezi Mungu amhifadhi Rais wetu kipenzi Samia Suluhu Hassan ,aaamen[emoji7][emoji7]
Unajua hujaongea lolote
 
Binafsi, naamini Rais Samia alipochukua madaraka, alikuwa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiutawala, yaani kutengeneza nchi ambayo watu wake wataongozwa kwa haki, kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa maoni, na kisha kujenga uchumi wenye misingi ya haki. Hii ndiyo ilikuwa sababu yake ya kuja na falsafa ya 4Rs.

Katika kuingia kwenye uhalisia, maana yake Rais Samia alikuwa anaingia kwenye kazi ngumu sana ya kuwabadilisha watu ambao wanajua kabisa kuwa uwepo wao katila nafasi walizopo ni kutokana na dhuluma dhidi ya umma wa Watanzania. Hii ilikuwa ni kuanzisha vita dhidi mifumo dhalimu ya ndani ya Serikali na ndani ya chama chake, mifumo iloyoota mizizi na kupata nguvu kwa miaka mingi.

Kubadili mifumo, tena inayoshikiliwa kidhalimu na watu wenye nguvu ndani ya chama na Serikali siyo jambo jepesi, ili kufanikiwa:

1) Rais Samia alihitaji kuwa na watu wenye nguvu na jasiri kweli kweli ambao wangeweza kusimamia utekelezaji. Bahati mbaya Rais Samia aliwakosa watu hao na akalazimika kuwatumia wale wale wafuasi wa mifumo dhalimu ambao aliwakuta. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.

2) Ili afanikiwe, alistahili kutengeneza msingi imara wa kuungwa mkono na umma katika kuleta mabadiliko. Na hapo alistahili kutafuta uungwaji mkono kutoka makundi yote, kuanzia ndani ya chama chake, vyama vya upinzani, taasisi mbalimbali, na umma kwa ujumla, na hilo lingeganyika kwa kuuelimisha umma ambao kwa muda mrefu umefungiwa katika ujinga. Ilitakiwa kuweka wazi ubaya na ubovu wa mifumo iliyopo, na kureleza wazi tunataka kujenga Taifa la watu gani. Ili kufanya hayo kwa mafanikio, alistahili kuondoka kuwa Rais wa CCM, na kuwa Rais wa Watanzania wote, na hiyo ilistahili idhihirike wazi kwa kauli na vitendo. Kwenye hili Rais Samia hakufanikiwa sana kwa sababu mara kadhaa alivishambulia vyama vya upinzani na kuipamba CCM, ambayo kimsingi ndicho baba wa huu udhalimu wote kwani ndicho kilichotengeneza hii mifumo dhalimu ya utawala Inayolisumbua na kuligandamiza Taifa.

3) Ili Rais asimamie haya mabadiliko, hakustahili kutekwa fikra zake kupitia hoja za kushindwa kwenye uchaguzi kama ambavyo wale wadhalimu wamekuwa wakimtishia. Hivyo ili kumwondolea hofu, hata kwa kupitia mifumo isiyo rasmi, angefanywa kuwa Rais wa mpito, yaani kwa kudhihirisha dhamira yake njema, kwa kilaalu wamekuwa wakifanya. njema, Rais Samia angeungwa mkono na vyama vyote vyenye dhamira njema, kwenye uchaguzi , vikijua kuwa baada ya kipimdi cha mpito, utafuata uchaguzi wa ushindani wenye mazingira safi na huu uchafu tulio nao sasa.

Kwa hali ilivyo sasa, kwa Rais Samia kukosa mikakati na mbimu sahihi, waumini wa mifumo dhalimu ndani ya CCM na Serikali, wameweza kumzidi nguvu na kumfanya na yeye aonekana kuwa ni sehemu yao. Sasa tunashuhudia falsafa yake ya 4Rs ikichomwa moto na watekaji watu, ikiuawa na wasiotaka katiba bora, na kichanwachanwa na wasiotaka tume bora ya uchaguzi. Utengamano alioufikiria kuujenga umefutika, na uovu umepata nguvu mpya ya ajabu kiasi cha wananchi wengi kuona kuwa 4R ni falsafa ya hadas ambayo haikuwa na dhamira ya kweli.

Mtihani mkubwa kwa Samia upo mwaka huu na mwaka kesho, ambapo wadhalimu watautumia uchaguzi kummaliza na kumchafua kabisa Rais Samia mbele ya umma. Na mbele ya uso wa jamii ya kimataifa.

Kwa sasa watu dhalimu ndani ya CCM na Serikali wanafurahia ushindi wao dhidi ya falsafa ya 4Rs.
Atabadilisha nini wakati lengo la waliomuweka ilikuwa kumuondoa JPM ili waendelee kuiba.Mtu aliyekuwa na ujasiri wa kubadilisha nchi ni JPM na ndiyo maana ata CCM alibomoa mifumo ya kipuuzi na serikalini pia.Yule Mkwere ndiyo alikuwa behind ya utekaji na uuaji ili kumchagua serikali ya Magufuli the same wanafanya kwa Samia this time kwasababu huwa hawapendi masilahi yao kuguswa, ukikaa Ikulu uwe puppet.
JPM alijaribu kufanya unachosema ila kwa sasa labda jeshi lipindue tuanze upya!
 
Exactly.

Alitakiwa kuishia pale pale kwenye maridhiano then atupishe, amepitiliza muda matokeo yake ameanza kuharibu hata yale mazuri ya mwanzo aliyofanya, shows she is not mentally strong to lead this country.
 
Vyote anavyovifanya ni kazi,iwe chanya au hasi no kazi hivyo hivyo!

Sisi tunasema kazi iendelee!!
 
Rais Samia alipochukua madaraka, alikuwa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiutawala, yaani kutengeneza nchi ambayo watu wake wataongozwa kwa haki, kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa maoni, na kisha kujenga uchumi wenye misingi ya haki.

Hiki ulichokiandika hapa hakiwezekani kwa nchi hii. Hivi vitu vinawezekana kwenye nchi ambayo ina fully democracy, hii nchi ni nchi ya kijamaa behind the scene, ila frontend unaona kama ni nchi flani ya kidemokrasia na inayofata mfumo wa vyama vingi ila katika reality haiko hivyo.

Kuna watu ndani ya CCM wana hofu juu ya future yao. Nadhani ndiyo hao madhalimu unaowasema.
Yaani uumpe mtu haki, demokrasia, uhuru wa maoni then ufanye upuuzi alafu huyo mtu akae kimya anakuangalia tu?

Ukiwapa watu haki, demokrasia na uhuru wa maoni inabidi uwe tayari kuwa challenged kwasababu kuna watu wamezaliwa kuhoji.

Kwahiyo huyo Bi mkubwa ww unamlaumu bure tu, siyo yeye aliyeshika hatma ya Tanzania.
 
Binafsi, naamini Rais Samia alipochukua madaraka, alikuwa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiutawala, yaani kutengeneza nchi ambayo watu wake wataongozwa kwa haki, kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa maoni, na kisha kujenga uchumi wenye misingi ya haki. Hii ndiyo ilikuwa sababu yake ya kuja na falsafa ya 4Rs.
Naunga mkono hoja.
Katika kuingia kwenye uhalisia, maana yake Rais Samia alikuwa anaingia kwenye kazi ngumu sana ya kuwabadilisha watu ambao wanajua kabisa kuwa uwepo wao katila nafasi walizopo ni kutokana na dhuluma dhidi ya umma wa Watanzania. Hii ilikuwa ni kuanzisha vita dhidi mifumo dhalimu ya ndani ya Serikali na ndani ya chama chake, mifumo iloyoota mizizi na kupata nguvu kwa miaka mingi.

Kubadili mifumo, tena inayoshikiliwa kidhalimu na watu wenye nguvu ndani ya chama na Serikali siyo jambo jepesi, ili kufanikiwa:
Ni kweli, changing mind set za watu ni kazi ngumu sana!.
1) Rais Samia alihitaji kuwa na watu wenye nguvu na jasiri kweli kweli ambao wangeweza kusimamia utekelezaji. Bahati mbaya Rais Samia aliwakosa watu hao na akalazimika kuwatumia wale wale wafuasi wa mifumo dhalimu ambao aliwakuta. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.
Ni kweli kabisa, sio kweli kuwa Rais Samia amewakosa watu hao, bali tatizo ni uwezo wake kuweza kuwabaini nani wanaweza kumsaidia kiukweli kweli, alipoanza alitupa matumaini makubwa sana Pascal Mayalla: Tanzania sasa inajenga Mifumo na sio kujenga watu kama enzi za Hayati Magufuli ila teua tumbua zilipoanza tukaona kama ni kufanya trial and error, mwanzo nilidhani ni anakoseshwa na wasaidizi wake Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda, zilipozidi nikauliza Could there be a problem with our vetting systems? These hirings and firings hazitaonekana kama signs za incompetence on part of appointing authority? teua tumbua ilipozidi, nikaona kama flipy flop nimelizungumzia humu Hizi pangua pangua za Rais Samia kwa wateule wake kila uchao zote zina maslahi kwa taifa au kuna flip-flops ?. na nikasema watu wenye akili, tayari wanajua udhaifu ulipo. Watu watakaomsaidia Rais Samia, ni wale ma bold wanaoweza kumwambia ukweli Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
Mtihani mkubwa kwa Samia upo mwaka huu na mwaka kesho, ambapo wadhalimu watautumia uchaguzi kummaliza na kumchafua kabisa Rais Samia mbele ya umma. Na mbele ya uso wa jamii ya kimataifa.

Kwa sasa watu dhalimu ndani ya CCM na Serikali wanafurahia ushindi wao dhidi ya falsafa ya 4Rs.
Ni kweli ila hawatafanikiwa kwasababu kwa mfumo wetu wa uchaguzi, CCM hata ikisimamisha jiwe, jiwe litashinda!.
P
 
Binafsi, naamini Rais Samia alipochukua madaraka, alikuwa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiutawala, yaani kutengeneza nchi ambayo watu wake wataongozwa kwa haki, kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa maoni, na kisha kujenga uchumi wenye misingi ya haki. Hii ndiyo ilikuwa sababu yake ya kuja na falsafa ya 4Rs.

Katika kuingia kwenye uhalisia, maana yake Rais Samia alikuwa anaingia kwenye kazi ngumu sana ya kuwabadilisha watu ambao wanajua kabisa kuwa uwepo wao katila nafasi walizopo ni kutokana na dhuluma dhidi ya umma wa Watanzania. Hii ilikuwa ni kuanzisha vita dhidi mifumo dhalimu ya ndani ya Serikali na ndani ya chama chake, mifumo iloyoota mizizi na kupata nguvu kwa miaka mingi.

Kubadili mifumo, tena inayoshikiliwa kidhalimu na watu wenye nguvu ndani ya chama na Serikali siyo jambo jepesi, ili kufanikiwa:

1) Rais Samia alihitaji kuwa na watu wenye nguvu na jasiri kweli kweli ambao wangeweza kusimamia utekelezaji. Bahati mbaya Rais Samia aliwakosa watu hao na akalazimika kuwatumia wale wale wafuasi wa mifumo dhalimu ambao aliwakuta. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.

2) Ili afanikiwe, alistahili kutengeneza msingi imara wa kuungwa mkono na umma katika kuleta mabadiliko. Na hapo alistahili kutafuta uungwaji mkono kutoka makundi yote, kuanzia ndani ya chama chake, vyama vya upinzani, taasisi mbalimbali, na umma kwa ujumla, na hilo lingeganyika kwa kuuelimisha umma ambao kwa muda mrefu umefungiwa katika ujinga. Ilitakiwa kuweka wazi ubaya na ubovu wa mifumo iliyopo, na kureleza wazi tunataka kujenga Taifa la watu gani. Ili kufanya hayo kwa mafanikio, alistahili kuondoka kuwa Rais wa CCM, na kuwa Rais wa Watanzania wote, na hiyo ilistahili idhihirike wazi kwa kauli na vitendo. Kwenye hili Rais Samia hakufanikiwa sana kwa sababu mara kadhaa alivishambulia vyama vya upinzani na kuipamba CCM, ambayo kimsingi ndicho baba wa huu udhalimu wote kwani ndicho kilichotengeneza hii mifumo dhalimu ya utawala Inayolisumbua na kuligandamiza Taifa.

3) Ili Rais asimamie haya mabadiliko, hakustahili kutekwa fikra zake kupitia hoja za kushindwa kwenye uchaguzi kama ambavyo wale wadhalimu wamekuwa wakimtishia. Hivyo ili kumwondolea hofu, hata kwa kupitia mifumo isiyo rasmi, angefanywa kuwa Rais wa mpito, yaani kwa kudhihirisha dhamira yake njema, kwa kilaalu wamekuwa wakifanya. njema, Rais Samia angeungwa mkono na vyama vyote vyenye dhamira njema, kwenye uchaguzi , vikijua kuwa baada ya kipimdi cha mpito, utafuata uchaguzi wa ushindani wenye mazingira safi na huu uchafu tulio nao sasa.

Kwa hali ilivyo sasa, kwa Rais Samia kukosa mikakati na mbimu sahihi, waumini wa mifumo dhalimu ndani ya CCM na Serikali, wameweza kumzidi nguvu na kumfanya na yeye aonekana kuwa ni sehemu yao. Sasa tunashuhudia falsafa yake ya 4Rs ikichomwa moto na watekaji watu, ikiuawa na wasiotaka katiba bora, na kichanwachanwa na wasiotaka tume bora ya uchaguzi. Utengamano alioufikiria kuujenga umefutika, na uovu umepata nguvu mpya ya ajabu kiasi cha wananchi wengi kuona kuwa 4R ni falsafa ya hadas ambayo haikuwa na dhamira ya kweli.

Mtihani mkubwa kwa Samia upo mwaka huu na mwaka kesho, ambapo wadhalimu watautumia uchaguzi kummaliza na kumchafua kabisa Rais Samia mbele ya umma. Na mbele ya uso wa jamii ya kimataifa.

Kwa sasa watu dhalimu ndani ya CCM na Serikali wanafurahia ushindi wao dhidi ya falsafa ya 4Rs.
We jamaa, huwa nakukubali sana ujuwe, hata hivyo, kwenye hili sikuungi mkono

Na sababu ya kutokukuunga mkono ni mahali pamoja tu!

Ijulikane kabisa kwamba, nchi yetu hii Tanzania watu wake hasa watumishi wa umma, wengi ni majangili wa kutupwa

Ni mafujaji ya kodi za wananchi, hayana huruma kwa raia na nchi hata kidogo

Unapozungumzia kiongozi yupi anafaa kuiongoza nchi hii, ni lazima kwanza aondoe kabisa hii mifumo iliyoingia kwenye damu za watumishi wa serikali ambao ni majizi

Ni lazima tu atumie nyenzo zote, Demokrasia kidogo na huku udikiteta ukishika hatamu

Kumponda Magufuli na mifumo yake, kivyovyote, siwezi kukubali na stomkubalia yeyote yule
 
actually,
macho na masikio ya jumuiya za kimaTaifa kwa wakati huu ni Tanzania hasa kutokana na umahiri wa serikali sikivu ya CCM chini ya kiongozi wetu makini sana ambae pia ni kipenzi cha waTanzania wote Dr Samia Suluhu Hassan kuliunganisha taifa na kuifungua nchi miongni mwa mataifa ya ulimwengu....

na ndio maana Dr.Tulia Akson, spika wetu ni Rais wa shirikisho la mabunge Duniani, na alishinda nafasi hiyo kwa kishindo sana kwasabubu ya influence ya Dr Samia Suluhu Hassan, Lakini pia uwezo wake mkubwa katika uongozi,
Lakini pia tuna mkurugenzi mkuu wa WHO Dr.Faustine Andungulie nae ameshinda kwa kishindo kikuu zaidi uchaguzi ule kwasabb ya influence ya Dr Samia Suluhu Hassan,

kwasabb hizo,
nchi yetu imefunguka, inaaminika na kusifika duniani kote na macho ya mataifa yote kwasasa ni Tanzania..

Tunapoelekea uchaguzi wa serikali, serikali sikivu ya CCM chini ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuonyesha duniani kwamba chaguzi zetu huendeshwa kwa haki zaidi, uhuru zaidi, na uwazi zaidi pengine kuliko nchi yoyote ulimwengu....

Zaidi ya hapo,
uchaguzi mkuu wa wazi, haki na huru wa kihistoria utafanyika Oct. 2025 kwa amani na utulivu haijawahi kutokea Tangu uhuru, mwana mama huyu Dr Samia Suluhu Hassan alishinda kwa kishindo kikuu, ngwe yake ya pili katika uongozi wa juu wa Taifa letu Tanzania 🐒
Hivi unadhani kuna mtu asiyependa uchaguzi ufanyike kwa uwazi na misingi ya haki? Unadhani kuna mtu asiyependa Rais Samia aiongoze nchi vizuri kwa kuzingatia haki za watu?

Dunia lazima itafuatilia yanayofanyika Tanzania kwa sababu Rais aliiahidi jumuia ya kimataifa kubadili uharamia uliokuwa ukifanyika kwenye uchaguzi, LAKINI je hiyo ahadi yake inapewa nguvu kiasi gani na ushenzi unaofanyika wa kuteka watu ambao ama wanaiokosoa serikali au wanamkosoa yeye binafsi?

Jamii ya kimataifa inafuatilia ili ipate kuoanisha maneno na uhalisia.

Marehemu Magufuli aliahidi kuwa uchaguzi wa 2020 utakuwa huru na wa haki. Lakini alipopokea tathmini ya watu wake, akabadili maneno yake na kuamua kuwanyima vibali vya kuingia nchini, hata watazamaji wa kimataifa.

Rais Samia, mapema kabisa ameanza kuonesha dalili mbaya, kwa kuwapa kibaki watekaji wa wakosoaji wake, kulazimisha uchaguzi wa serikali za mitaa usimamiwe na waziri mkwe wake badala ya tume ya uchaguzi, mbaya zaidi amegoma kabisa nchi kuwa na Tume huru ya uchaguzi. Alichofanya ni kuiita Tume ya Uchaguzi isiyo huru kuwa ni Tume Huru ya Uchaguzi. Alichokifanya hakina tofauti na alichofanya Maduro kule Venezuela.
 
Binafsi, naamini Rais Samia alipochukua madaraka, alikuwa na dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko ya mifumo ya kiutawala, yaani kutengeneza nchi ambayo watu wake wataongozwa kwa haki, kwa kuzingatia misingi ya demokrasia, uhuru wa maoni, na kisha kujenga uchumi wenye misingi ya haki. Hii ndiyo ilikuwa sababu yake ya kuja na falsafa ya 4Rs.

Katika kuingia kwenye uhalisia, maana yake Rais Samia alikuwa anaingia kwenye kazi ngumu sana ya kuwabadilisha watu ambao wanajua kabisa kuwa uwepo wao katila nafasi walizopo ni kutokana na dhuluma dhidi ya umma wa Watanzania. Hii ilikuwa ni kuanzisha vita dhidi mifumo dhalimu ya ndani ya Serikali na ndani ya chama chake, mifumo iloyoota mizizi na kupata nguvu kwa miaka mingi.

Kubadili mifumo, tena inayoshikiliwa kidhalimu na watu wenye nguvu ndani ya chama na Serikali siyo jambo jepesi, ili kufanikiwa:

1) Rais Samia alihitaji kuwa na watu wenye nguvu na jasiri kweli kweli ambao wangeweza kusimamia utekelezaji. Bahati mbaya Rais Samia aliwakosa watu hao na akalazimika kuwatumia wale wale wafuasi wa mifumo dhalimu ambao aliwakuta. Hilo lilikuwa kosa lake la kwanza.

2) Ili afanikiwe, alistahili kutengeneza msingi imara wa kuungwa mkono na umma katika kuleta mabadiliko. Na hapo alistahili kutafuta uungwaji mkono kutoka makundi yote, kuanzia ndani ya chama chake, vyama vya upinzani, taasisi mbalimbali, na umma kwa ujumla, na hilo lingeganyika kwa kuuelimisha umma ambao kwa muda mrefu umefungiwa katika ujinga. Ilitakiwa kuweka wazi ubaya na ubovu wa mifumo iliyopo, na kureleza wazi tunataka kujenga Taifa la watu gani. Ili kufanya hayo kwa mafanikio, alistahili kuondoka kuwa Rais wa CCM, na kuwa Rais wa Watanzania wote, na hiyo ilistahili idhihirike wazi kwa kauli na vitendo. Kwenye hili Rais Samia hakufanikiwa sana kwa sababu mara kadhaa alivishambulia vyama vya upinzani na kuipamba CCM, ambayo kimsingi ndicho baba wa huu udhalimu wote kwani ndicho kilichotengeneza hii mifumo dhalimu ya utawala Inayolisumbua na kuligandamiza Taifa.

3) Ili Rais asimamie haya mabadiliko, hakustahili kutekwa fikra zake kupitia hoja za kushindwa kwenye uchaguzi kama ambavyo wale wadhalimu wamekuwa wakimtishia. Hivyo ili kumwondolea hofu, hata kwa kupitia mifumo isiyo rasmi, angefanywa kuwa Rais wa mpito, yaani kwa kudhihirisha dhamira yake njema, kwa kilaalu wamekuwa wakifanya. njema, Rais Samia angeungwa mkono na vyama vyote vyenye dhamira njema, kwenye uchaguzi , vikijua kuwa baada ya kipimdi cha mpito, utafuata uchaguzi wa ushindani wenye mazingira safi na huu uchafu tulio nao sasa.

Kwa hali ilivyo sasa, kwa Rais Samia kukosa mikakati na mbimu sahihi, waumini wa mifumo dhalimu ndani ya CCM na Serikali, wameweza kumzidi nguvu na kumfanya na yeye aonekana kuwa ni sehemu yao. Sasa tunashuhudia falsafa yake ya 4Rs ikichomwa moto na watekaji watu, ikiuawa na wasiotaka katiba bora, na kichanwachanwa na wasiotaka tume bora ya uchaguzi. Utengamano alioufikiria kuujenga umefutika, na uovu umepata nguvu mpya ya ajabu kiasi cha wananchi wengi kuona kuwa 4R ni falsafa ya hadas ambayo haikuwa na dhamira ya kweli.

Mtihani mkubwa kwa Samia upo mwaka huu na mwaka kesho, ambapo wadhalimu watautumia uchaguzi kummaliza na kumchafua kabisa Rais Samia mbele ya umma. Na mbele ya uso wa jamii ya kimataifa.

Kwa sasa watu dhalimu ndani ya CCM na Serikali wanafurahia ushindi wao dhidi ya falsafa ya 4Rs.
Ni sawa pia maana anaachia mwingine 2025, yeye anapumzika baada ya kufanya kazi nzuri baada ya kifa cha Rais akiwa madarakani.
 
Hivi unadhani kuna mtu asiyependa uchaguzi ufanyike kwa uwazi na misingi ya haki? Unadhani kuna mtu asiyependa Rais Samia aiongoze nchi vizuri kwa kuzingatia haki za watu?

Dunia lazima itafuatilia yanayofanyika Tanzania kwa sababu Rais aliiahidi jumuia ya kimataifa kubadili uharamia uliokuwa ukifanyika kwenye uchaguzi, LAKINI je hiyo ahadi yake inapewa nguvu kiasi gani na ushenzi unaofanyika wa kuteka watu ambao ama wanaiokosoa serikali au wanamkosoa yeye binafsi?

Jamii ya kimataifa inafuatilia ili ipate kuoanisha maneno na uhalisia.

Marehemu Magufuli aliahidi kuwa uchaguzi wa 2020 utakuwa huru na wa haki. Lakini alipopokea tathmini ya watu wake, akabadili maneno yake na kuamua kuwanyima vibali vya kuingia nchini, hata watazamaji wa kimataifa.

Rais Samia, mapema kabisa ameanza kuonesha dalili mbaya, kwa kuwapa kibaki watekaji wa wakosoaji wake, kulazimisha uchaguzi wa serikali za mitaa usimamiwe na waziri mkwe wake badala ya tume ya uchaguzi, mbaya zaidi amegoma kabisa nchi kuwa na Tume huru ya uchaguzi. Alichofanya ni kuiita Tume ya Uchaguzi isiyo huru kuwa ni Tume Huru ya Uchaguzi. Alichokifanya hakina tofauti na alichofanya Maduro kule Venezuela.
gentleman,
mimi si mtu wa kudhani dhani kama mlivyo ninye wenye imani haba za kishirikiana....

ni bayana na uhakika kabisaa kwamba Dr.Samia Suluhu Hassan ameshaiunganisha nchi ameshalifungua Taifa duniani...

na kwa kutumia 4Rs theories alizobuni RAIS, kipenzi cha wananchi wote Tanzania, tunaelekea kufanya Uchaguzi huru, wazi na wa haki wa kihistoria Tanzania, mpende, msipende...

zaidi ya hapo,
dalili zinaonyesha wazi maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa2025 ni full peace, hakuna manung'uniko kwenye maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura, na hivyo ni Imani ya Serikali, wananchi na jumuiya nzima ya kimatafa Uchaguzi mkuu ujao utakua na amani zaidi kufanyika Tanzania 🐒

washirikina endeleeni kung'ang'ana na yaliyopita,
wakati vyama na Serikali yenye maono vinajiandaa na chaguzi zijazo ,

ramli, ushirikina na kutegemea huruma vitaendelea kuwatesa na kuwachelewesha sana 🐒
 
Ndo wamemtuma kuuza Bandari? Ndo wamemtuma kuuza Ngorongoro? Ndo wamemtuma kuhamishia pesa Zanzibar!!

Unaongea vitu visivyo na maana Kwa maisha ya watu!! Eti 4R

pesa zipi zilizohamishiwa Zanzibar? acha story za vijiweni
 
Samia hawawezi CCM, nilijua mapema atashindwa. If you can't beat them join them.

Tatizo la nchi hii sio Samia bali ni CCM, na CCM ina mizizi mipana sana, ukiwa ndani ya mfumo wao ni nearly impossible kubadilisha mwenendo wa nchi. na ndio mana suluhisho la hii nchi ni CCM kuong'oka madarakani, Hata Lissu atanngazwe leo raisi lakini ikiwa kwa kupitia ndani ya CCM basi hakutakuwa na mabadiliko ya kweli.
na wanaohisi Samia 2025 anaondoka nahisi nao ni wagonjwa wa akili.
 
Back
Top Bottom