Rais Samia alistahili kuwa Rais wa kipindi cha mpito

Unajua hujaongea lolote
 
Atabadilisha nini wakati lengo la waliomuweka ilikuwa kumuondoa JPM ili waendelee kuiba.Mtu aliyekuwa na ujasiri wa kubadilisha nchi ni JPM na ndiyo maana ata CCM alibomoa mifumo ya kipuuzi na serikalini pia.Yule Mkwere ndiyo alikuwa behind ya utekaji na uuaji ili kumchagua serikali ya Magufuli the same wanafanya kwa Samia this time kwasababu huwa hawapendi masilahi yao kuguswa, ukikaa Ikulu uwe puppet.
JPM alijaribu kufanya unachosema ila kwa sasa labda jeshi lipindue tuanze upya!
 
Exactly.

Alitakiwa kuishia pale pale kwenye maridhiano then atupishe, amepitiliza muda matokeo yake ameanza kuharibu hata yale mazuri ya mwanzo aliyofanya, shows she is not mentally strong to lead this country.
 
Hata sasa ni rais wa mpito, maana hatopita 2025 hata kwa mbinu za maporini.
Ulishawahi kusimamia uchaguzi mkuu wa Tanzania?kama haujawahi umesamehewa maana haujui unaloandika.
 
Vyote anavyovifanya ni kazi,iwe chanya au hasi no kazi hivyo hivyo!

Sisi tunasema kazi iendelee!!
 

Hiki ulichokiandika hapa hakiwezekani kwa nchi hii. Hivi vitu vinawezekana kwenye nchi ambayo ina fully democracy, hii nchi ni nchi ya kijamaa behind the scene, ila frontend unaona kama ni nchi flani ya kidemokrasia na inayofata mfumo wa vyama vingi ila katika reality haiko hivyo.

Kuna watu ndani ya CCM wana hofu juu ya future yao. Nadhani ndiyo hao madhalimu unaowasema.
Yaani uumpe mtu haki, demokrasia, uhuru wa maoni then ufanye upuuzi alafu huyo mtu akae kimya anakuangalia tu?

Ukiwapa watu haki, demokrasia na uhuru wa maoni inabidi uwe tayari kuwa challenged kwasababu kuna watu wamezaliwa kuhoji.

Kwahiyo huyo Bi mkubwa ww unamlaumu bure tu, siyo yeye aliyeshika hatma ya Tanzania.
 
Naunga mkono hoja.
Ni kweli, changing mind set za watu ni kazi ngumu sana!.
Ni kweli kabisa, sio kweli kuwa Rais Samia amewakosa watu hao, bali tatizo ni uwezo wake kuweza kuwabaini nani wanaweza kumsaidia kiukweli kweli, alipoanza alitupa matumaini makubwa sana Pascal Mayalla: Tanzania sasa inajenga Mifumo na sio kujenga watu kama enzi za Hayati Magufuli ila teua tumbua zilipoanza tukaona kama ni kufanya trial and error, mwanzo nilidhani ni anakoseshwa na wasaidizi wake Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda, zilipozidi nikauliza Could there be a problem with our vetting systems? These hirings and firings hazitaonekana kama signs za incompetence on part of appointing authority? teua tumbua ilipozidi, nikaona kama flipy flop nimelizungumzia humu Hizi pangua pangua za Rais Samia kwa wateule wake kila uchao zote zina maslahi kwa taifa au kuna flip-flops ?. na nikasema watu wenye akili, tayari wanajua udhaifu ulipo. Watu watakaomsaidia Rais Samia, ni wale ma bold wanaoweza kumwambia ukweli Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
Ni kweli ila hawatafanikiwa kwasababu kwa mfumo wetu wa uchaguzi, CCM hata ikisimamisha jiwe, jiwe litashinda!.
P
 
We jamaa, huwa nakukubali sana ujuwe, hata hivyo, kwenye hili sikuungi mkono

Na sababu ya kutokukuunga mkono ni mahali pamoja tu!

Ijulikane kabisa kwamba, nchi yetu hii Tanzania watu wake hasa watumishi wa umma, wengi ni majangili wa kutupwa

Ni mafujaji ya kodi za wananchi, hayana huruma kwa raia na nchi hata kidogo

Unapozungumzia kiongozi yupi anafaa kuiongoza nchi hii, ni lazima kwanza aondoe kabisa hii mifumo iliyoingia kwenye damu za watumishi wa serikali ambao ni majizi

Ni lazima tu atumie nyenzo zote, Demokrasia kidogo na huku udikiteta ukishika hatamu

Kumponda Magufuli na mifumo yake, kivyovyote, siwezi kukubali na stomkubalia yeyote yule
 
Hivi unadhani kuna mtu asiyependa uchaguzi ufanyike kwa uwazi na misingi ya haki? Unadhani kuna mtu asiyependa Rais Samia aiongoze nchi vizuri kwa kuzingatia haki za watu?

Dunia lazima itafuatilia yanayofanyika Tanzania kwa sababu Rais aliiahidi jumuia ya kimataifa kubadili uharamia uliokuwa ukifanyika kwenye uchaguzi, LAKINI je hiyo ahadi yake inapewa nguvu kiasi gani na ushenzi unaofanyika wa kuteka watu ambao ama wanaiokosoa serikali au wanamkosoa yeye binafsi?

Jamii ya kimataifa inafuatilia ili ipate kuoanisha maneno na uhalisia.

Marehemu Magufuli aliahidi kuwa uchaguzi wa 2020 utakuwa huru na wa haki. Lakini alipopokea tathmini ya watu wake, akabadili maneno yake na kuamua kuwanyima vibali vya kuingia nchini, hata watazamaji wa kimataifa.

Rais Samia, mapema kabisa ameanza kuonesha dalili mbaya, kwa kuwapa kibaki watekaji wa wakosoaji wake, kulazimisha uchaguzi wa serikali za mitaa usimamiwe na waziri mkwe wake badala ya tume ya uchaguzi, mbaya zaidi amegoma kabisa nchi kuwa na Tume huru ya uchaguzi. Alichofanya ni kuiita Tume ya Uchaguzi isiyo huru kuwa ni Tume Huru ya Uchaguzi. Alichokifanya hakina tofauti na alichofanya Maduro kule Venezuela.
 
Ni sawa pia maana anaachia mwingine 2025, yeye anapumzika baada ya kufanya kazi nzuri baada ya kifa cha Rais akiwa madarakani.
 
gentleman,
mimi si mtu wa kudhani dhani kama mlivyo ninye wenye imani haba za kishirikiana....

ni bayana na uhakika kabisaa kwamba Dr.Samia Suluhu Hassan ameshaiunganisha nchi ameshalifungua Taifa duniani...

na kwa kutumia 4Rs theories alizobuni RAIS, kipenzi cha wananchi wote Tanzania, tunaelekea kufanya Uchaguzi huru, wazi na wa haki wa kihistoria Tanzania, mpende, msipende...

zaidi ya hapo,
dalili zinaonyesha wazi maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa2025 ni full peace, hakuna manung'uniko kwenye maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura, na hivyo ni Imani ya Serikali, wananchi na jumuiya nzima ya kimatafa Uchaguzi mkuu ujao utakua na amani zaidi kufanyika Tanzania πŸ’

washirikina endeleeni kung'ang'ana na yaliyopita,
wakati vyama na Serikali yenye maono vinajiandaa na chaguzi zijazo ,

ramli, ushirikina na kutegemea huruma vitaendelea kuwatesa na kuwachelewesha sana πŸ’
 
Ndo wamemtuma kuuza Bandari? Ndo wamemtuma kuuza Ngorongoro? Ndo wamemtuma kuhamishia pesa Zanzibar!!

Unaongea vitu visivyo na maana Kwa maisha ya watu!! Eti 4R

pesa zipi zilizohamishiwa Zanzibar? acha story za vijiweni
 
Samia hawawezi CCM, nilijua mapema atashindwa. If you can't beat them join them.

Tatizo la nchi hii sio Samia bali ni CCM, na CCM ina mizizi mipana sana, ukiwa ndani ya mfumo wao ni nearly impossible kubadilisha mwenendo wa nchi. na ndio mana suluhisho la hii nchi ni CCM kuong'oka madarakani, Hata Lissu atanngazwe leo raisi lakini ikiwa kwa kupitia ndani ya CCM basi hakutakuwa na mabadiliko ya kweli.
na wanaohisi Samia 2025 anaondoka nahisi nao ni wagonjwa wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…