Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Kwa kweli Katika hotuba aliyoitoa leo huko kwenye Chuo cha Polisi Moshi, Rais Samia ameamua kuyaweka wazi maovu yanayofanywa na Jeshi hilo la Polisi na hivyo nampongeza Sana Rais wetu kwa ujasiri wake huo.
Kwanza amesisitiza kuwa ni lazima Jeshi la Polisi lizingatie Nidhamu, Haki na Weledi Katika utendaji wao wa Kazi za kila siku.
Ameeleza kuwa Jeshi la Polisi, halina sifa nzuri ndani ya jamii ya Watanzania.
Akisema kuwa Rushwa imekithiri ndani ya Jeshi hilo, akitoa mifano hai kabisa, kama vile askari wa barabarani ambao huwa wanachukua Rushwa waziwazi!
Anaendelea kusisitiza kuwa hata dhamana, ambayo ni Haki ya mtuhumiwa, lakini Jeshi hilo limekuwa "likiwakamua" watuhumiwa, ikiwa ni uthibitisho wa kauli mbiu ya sisi raia, kuwa kuingia kwenye selo za Polisi ni bure, lakini kutoka ni kwa Pesa!
Akakemea pia tabia ya Polisi kuwabambikia Kesi raia, ambapo bila kujali, namna wanavyowatesa hao wanaobambikiwa Kesi.
Pia amekemea tabia za Ufisadi, zilizokithiri ndani ya Jeshi hilo la Polisi, akitoa mfano namna Jeshi hilo linavyofanya "biashara" ya kuuza sare hizo za Polisi kwa Majeshi mengine kama vile kwa Jeshi la zimamoto.
Akaomgeza namna maafisa wa Jeshi hilo, wanavyotumia bajeti ya mafuta ya Jeshi hilo na kuyapeleka kwenye magari yao binafsi!
Nampongeza Sana Rais Samia kwa kuyaanika hadharani maovu hayo ya Jeshi la Polisi, ambapo sisi raia wema, tumekuwa tukiyakemea maovu hayo kwa kipindi kirefu Sana, lakini yamekuwa hayasikilizwi kabisa.