Kimalingano
JF-Expert Member
- Mar 27, 2023
- 709
- 919
Usiwe na wasiwasi,Paskal alishatabiri kuwa CCM hawatamsimamisha mwaka 2025.Miaka ya majaribio madini na bahari mapori vyote vimeuzwa kwasasa Tanzania ina deni la trion 91 hii maana yake NI kwamba kwa watanzania milion 60 Kila mtanzania anadaiwa tsh 1,500,000/= kwanza hapo ulipo hiyo pesa unayo?
Kwangu Mimi naona chawa wapunguze mihemko mama ana Kila sababu ya kutogombea 2025 alishakula mema ya nchi kama NI nchi ameitumikia vya kutosha NI Bora aachie ngazi maana naona meli inazidi kuzama kama vile haina nahodha.
Tuhuma alizopewa waziri wa kilimo serikali imeshindwa kuzikanusha kwa fact hivi kweli kampuni ya Simu ya itel ndiyo yakupewa tenda ya kuagiza sukari nje?
Mama tulichobaini NI kwamba ubadhilifu unaofanywa na watendaji wako Una baraka zako kwani hatuoni hatua zozote unazochukua Zaidi ya kuwahamishahamisha hii nchi kweli imekuwa ya kuhamishahamisha watendaji wa bovu na wabadhilifu kweli mama kweli hapana tunasema hapana wewe hizo pikipiki zako Rudisha Tu Sisi kwenye chama tumechoka haya maigizo.
Akishasema yeye huwa hakuna mashaka.