Rais Samia amedhamiria, Reforms ya kibabe kwenye Afya

Kweli kabisa

Wanakopeshana pesa za NHIF , na kununua magari ya anasa

Watu wote wapende watoto kupata matibabu
 
Nimewaza sana kuhusu Jenista kupewa wizara nyeti hivi, Mungu anisamehe nikisema sijawahi kumuelewa huyu waziri.
Jenista muhagama hapana, hii wizara inahitaji professional doctor kabisa, sio ku rotate mawazir wale wale, efficiency haito tokea
Pendekezeni majina ya Watu ambao mnaona wanafaa kuteuliwa katika nafasi hii ya Waziri wa Afya. Tajeni Majina yao ili kumsaidia Rais kwenye suala hili, tusiendelee kuwategemea Tiss peke yao katika kupendekeza majina ya Wateule kwa nafasi mbalimbali za Uongozi wa nchi kwani imedhihirika wazi kwamba jukunu Hilo limewashinda. JF pia chanzo kizuri cha Rais wa nchi kuweza kupata taarifa sahihi za yeye kuweza kuzifanyia Maamuzi (OSINT),
 
Jenista muhagama hapana, hii wizara inahitaji professional doctor kabisa, sio ku rotate mawazir wale wale, efficiency haito tokea
kama si kwa nafasi aliyopendekezwa kule WHO Afrika,Faustine Ndugulile angefaa sana hapa,
 
kama si kwa nafasi aliyopendekezwa kule WHO Afrika,Faustine Ndugulile angefaa sana hapa,
Hii nayo ni point, basi tu siasa zimeingilia wizara za wataalam. Kuna wizara ni technical hazihitaji politicians kabisa, sijui mamlaka ya teuzi watajifunza lini
 
Kumbe siku hizi hapa JamiiForums kila Member akiandika post yake akimaliza kwa chini anatakiwa aandike jina lake na mahala alipo ( eneo na nchi ) pia?

GENTAMYCINE, Nachingwea, Tanzania
 
Jipe muda (kama miezi sita) halafu njoo tena kuupitia huu uzi wako huenda utakuja kumkumbuka tena Ummy.

Laiti ungejua namna Ummy alivyokuwa anapingana kimya kimya na sera mpya za NHIF usingesema hayo. Hivi hujui issue ya Ummy kudaiwa analinda maslahi ya hospitali binafsi kwa sababu ni mdau kwenye hospitali binafsi?

Sijui inakumbuka issue ya kikokotoo cha wastaafu mpaka kuna mkurugenzi na waziri kufukuzwa, nini kilifuata baada ya kuletwa mkurugenzi mpya na waziri mpya? Kikokotoo kile kile kibovu kilikuja kutumika.
 
Hii nchi mtawalaumu tu watu, wakati tatizo ni mfumo mzima, mtendaji mkuu PS, si amebaki?? Huyo mama wa ngekewa aliypelekwa huko ana nini cha ziada?? Ndio maaana kila siku ni panga pangua tu lakini hakuna la maana.
 
Kuna jembe letu huyu mama yupo vzr Dkt Gwajima D apewe wizara hii ya afya kuna mchwa upo pale NHIF tunakosa huduma nzur wao wanakula hela zetu
Mama Samia tunamuomba huyu mama aje anyooshe hii wizara
 
Bila kuondokana na mtindo wa kuteua Mawaziri kutoka Bungeni hatutafika popote
 
Hata tukipendekeza watasikia? Ata tilia maanani? Anyway we have list of qualified individuals
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…