Rais Samia amejitoa na kujitolea Maisha yake kwa ajili ya kuleta Tabasamu na Matumaini katika mioyo ya Watanzania

Unaandika usichokijua. Unajua maana ya " kutoa maisha yake" wewe?
Huu ni uandishi wa ki-chawa !!
 
Ngoja walinda legacy wauone huu uzi, utajuta!!
 
Sahihi naona mtaani kidogo kidogo maisha yananadilika na baadhi wameanza kuona.
 
Watanzania wanaona na wameona matunda makubwa na maendeleo katika kila secta yaliyopatikana ndani ya muda mfupi kutokana na uchapa kazi wa mh Rais wetu,ndio maana wanaendelea kumuunga mkono.

Lete fact, zitaje hizo secta then waliomo humo watasema
 
Hivi huyo mamako ni lini atayawajibisha mafisadi ripoti ya CAG, au ndio ile kusema stupid?!.
Inamchukua muda gani kufanya maamuzi yeye kama amiri jeshi mkuu.
 
Hivi huyo mamako ni lini atayawajibisha mafisadi ripoti ya CAG, au ndio ile kusema stupid?!.
Inamchukua muda gani kufanya maamuzi yeye kama amiri jeshi mkuu.
Uwe na subira mkuu maana mama Hana mchezo na wabadhirifu wa pesa za umma maana anafahamu uchungu na jasho avujalo mtanzania katika kulipa Kodi ili ajenge nchi yake.
 
Lete fact, zitaje hizo secta then waliomo humo watasema
Secta ya kilimo Ni mafanikioa matupu,Afya ni hatua tupu ambapo zahanati na vituo vya Afya vimejengwa kwa Kasi kila eneo,mfano mwanzo mwa mwaka huu kulijengwa vituo vya Afya 234 hapa nchini,Katia Elimu nako Ni matunda matupu ambapo Sasa wanafunzi wanapata nafasi ya kuripoti shule kwa wakati mmoja kutokana na kujengwa kwa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20,lakini pia Elimu Ni bure Mpaka kidato Cha sita huku mikopo ya Elimu ya juu ikitolewa kwa wanafunzi wote wenye sifa
 

So haya yote yameboreshwa Kwa miaka 2 Tu?
 
Amejitolea kwenu nyie chawa.
 
Nchi masikini ndio zinazoongoza kwa kusifu viongozi wake, wale wenye akili timam wanawakosoa viongozi wao bila uoga...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…