Rais Samia amekuwa mzito sana wa kufanya maamuzi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kila kitu kinachofanyika, kutendeka au kutendwa, kinapaswa kuwa katika kiwango ambacho hakipungui sana au kuzidi sana(kiwe within reasonable limits).

Kwa msingi huo, hata viongozi wetu katika kufanya maamuzi, wanapaswa kuzingatia hilo ili wasiharubu, na pia ili wasionee watu.

Mwendazake katika kufanya maamuzi, kuna wakati ni wazi alipitiliza na alionea sana watu, na ndio maana tuliona baadhi ya aliowaondoa katika nafasi zao, baadae aliwarudisha(inaonyesha aligundua makosa yake).

Sasa huyu Mama yetu anaonekana kuwa ni kinyume cha Mwendazake kwa kuwa mzito kuchukua maamuzi kwa viwango nachosema ni cha kupitiliza(it is getting too much).

Mfano sahihi ni jinsi anavyokuwa mzito kumuondoa huyu Bosi wa Mapolisi ambae sasa anapigiwa kelele karibu kila kona ila Mama bado haoni kuwa huyu mtu ni tatizo (anapaswa kuondolewa).

Kama anapokea maagizo kutoka juu, njia mowajawapo ya kurekebisha hali hii bado itabaki kuwa ni kumuondoa tu na kumpangia kazi nyingine, na mrithi wake asiingiliwe, vinginevyo hatua ya kumuondoa itakuwa haina maana.

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama Mama ataendelea kupuuza hizi sauti, basi awe tayari kukubaliana na matokeo, na sijui kama kuna binadamu wa kushindana na Mungu.

Hata Mwendazake alimlinda sana Bashite na kupuuza sauti ya walio wengi, ila mwisho wa siku yalimshinda.

Too much of everything is harmful-Mama utajionea siku si nyingi.

Tukumbuke hata Mama mwenyewe anawalalamikia hawa jamaa.

Time will tell.
 
Kwenye hoja zenye mashiko , watu wataanza uchadema na uccm...
Imekuwa kero, huu mvutano wa hivi vyama ni kansa kwenye hili taifa... wananchi wanaumia...
ccm nao kila wanalofana wanafanya kuwakomoa chadema bila kujali maslahi ya wananchi...

Kila anayeonekana kutoa ushauri na kukosoa serikali anaonekana ni chadema...

Ndugu zangu tutangulize uzalendo kwanza...

Tanganyika na Zanzibar zimekuwepo hata kabla ya waanzilishi wa vyama hivyo hawajazaliwa....
 
Tatizo lenu chadema mnajiona mpo parfect sana hiyo lazima itawakost imagine gaidi limeua askari wanaolinda usalama wetu lakini mnawatukana polisi na kumpongeza gaidi na bado mnalilia haki je haki huwa inaupande mmoja?
 
Kila kitu kinachofanyika, kutendeka au kutendwa, kinapaswa kuwa katika kiwango ambacho hakipungui sana au kuzidi sana(kiwe within reasonable limits).

Kwa msingi huo, hata viongozi wetu katika kufanya maamuzi, wanapaswa kuzingatia hilo ili wasiharubu, na pia ili wasionee watu.

Mwendazake katika kufanya maamuzi, alipitiliza na alionea watu na ndio maana tuliona baadhi ya aliowaondoa katika nafasi zao baadae aliwarudisha(ni wazi aligundua makosa yake).

Sasa huyu Mama yetu anaonekana kuwa ni kinyume cha Mwendazake kwa kuwa mzito kuchukua maamuzi kwa viwango nachosema ni cha kupitiliza(it is getting too much).

Mfano sahihi ni jinsi anavyokuwa mzito kumuondoa huyu Bosi wa Mapolisi ambae sasa anapigiwa kelele karibu kila kona ila Mama bado haoni kuwa huyu mtu ni tatizo (anapaswa kuondolewa).

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama Mama ataendelea kupuuza hizi sauti, basi awe tayari kukubaliana na matokeo na sijui kama kuna binadamu wa kushindana na Mungu.

Hata Mwendazake alimlinda sana Bashite na kupuuza sauti ya walio wengi ila mwisho wa siku yalimshinda.

Too much of everything is harmful-Mama utajionea siku si nyingi

Time will tell.
Hapo kwa mapolis is too much kwakweliii
 
Maelezo yako Kwa watanzania yanaeleweka. Pale kile kitabu Cha mwaka 1977, kilipoandikwa Rais akifa Makamu wake anachukua nafasi bila kuwekwa kipindi Cha mpito Cha kumpima then ufanyike uchaguzi mkuu hapo ndipo mliliwa. Sasa haijulikani atatawala Hadi lini so vumilieni na muisome namba sawa sawa .
 
Kila kitu kinachofanyika, kutendeka au kutendwa, kinapaswa kuwa katika kiwango ambacho hakipungui sana au kuzidi sana(kiwe within reasonable limits).

Kwa msingi huo, hata viongozi wetu katika kufanya maamuzi, wanapaswa kuzingatia hilo ili wasiharubu, na pia ili wasionee watu.

Mwendazake katika kufanya maamuzi, alipitiliza na alionea watu na ndio maana tuliona baadhi ya aliowaondoa katika nafasi zao baadae aliwarudisha(ni wazi aligundua makosa yake).

Sasa huyu Mama yetu anaonekana kuwa ni kinyume cha Mwendazake kwa kuwa mzito kuchukua maamuzi kwa viwango nachosema ni cha kupitiliza(it is getting too much).

Mfano sahihi ni jinsi anavyokuwa mzito kumuondoa huyu Bosi wa Mapolisi ambae sasa anapigiwa kelele karibu kila kona ila Mama bado haoni kuwa huyu mtu ni tatizo (anapaswa kuondolewa).

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama Mama ataendelea kupuuza hizi sauti, basi awe tayari kukubaliana na matokeo, na sijui kama kuna binadamu wa kushindana na Mungu.

Hata Mwendazake alimlinda sana Bashite na kupuuza sauti ya walio wengi ila mwisho wa siku yalimshinda.

Too much of everything is harmful-Mama utajionea siku si nyingi

Time will tell.
yajayo yanafurahisha
 
Tatizo lenu chadema mnajiona mpo parfect sana hiyo lazima itawakost imagine gaidi limeua askari wanaolinda usalama wetu lakini mnawatukana polisi na kumpongeza gaidi na bado mnalilia haki je haki huwa inaupande mmoja?
Bro samahani, hivi wewe ni Mod au Bot?
 
sikuwahi kujua kuwa jinsi ambavyo tunashabikia simba na Yanga, tunaweza kushabikia na uendeshaji wa serikali, mfano shabiki akomae Haji Manara afukuzwe Yanga, hamna utofauti na kusema IGP afukuzwe,
Kimsingi ni mihemuko ya ushabiki hamna mantiki.
 
Natafuta cha kulalamika lakini nakosa..😂
 
Nimepata sasa!. Naomba waruhusu bangi tu tulime ili wachukue tozo vizuri 😅
 
Mkuu hata yule mwenyekiti aliejimilikisha kiti pale ufipa wengi wameshamchoka, kama tulivyoona week moja au mbili zilizopita, kuna vijana mbali mbali waliotaka mageuzi kupitia katiba ya chama japo walipigwa vita na genge lake ambalo linaishi kupitia mfuko wake. Lkn bado kuna uzito fulan aidha kwa makusudi au kwa kuogopa kumwambia ukweli kwamba a step down ili waje wangine wenye mawazo mbadala (sio kati ya wale wanafiki niliowaweka hapo chini kwenye picha) waendeleze mapambano ya kujenga upinzan imara. Sio huu wa kupigania au kulinda masilahi ya mabwanyenye wachache ndan ya chama. So aina hii ya viongozi wazito wasioweza kuchukua maamuzi ya haraka kwa faida ya wanachama au wananchi ndani ya vyama au serikali haiwezi kuisha. Maana imekuwa kama vile ni utamaduni wa tabia za baadhi ya viongozi mbali mbali haijalishi ni wa chama au serikali.

images (7).jpeg

2878995_images_9.jpeg
 
Anaogopa kuwatumbua hata kama wamepwaya, anaongoza nchi kama nyumba ya ibada, yeye anajua kuwakandamiza wananchi na tozo zake za uzalendo.
 
Mkuu hata yule mwenyekiti aliejimilikisha kiti pale ufipa wengi wameshamchoka, kama tulivyoona vijana mbali mbali waliotaka mageuzi kupitia katiba ya chama japo walipigwa vita na genge lake ambalo linaishi kupitia mfuko wake. Lkn bado kuna uzito fulan aidha kwa makusudi au kwa kuogopa kumwambia ukweli kwamba a step down ili waje wangine wenye mawazo mbadala (sio kati ya wale wanafiki niliowaweka hapo chini kwenye picha) waendeleze mapambano ya kujenga upinzan imara. Sio huu wa kupigania au kulinda masilahi ya mabwanyenye wachache ndan ya chama.

View attachment 1911315

View attachment 1911316
Kwanini vichwa vyenu huko lumumba vime stuck kwa kiwango cha kutisha namna hii?

Hamna mawazo mapya nyie mbuzi.
 
Kila kitu kinachofanyika, kutendeka au kutendwa, kinapaswa kuwa katika kiwango ambacho hakipungui sana au kuzidi sana(kiwe within reasonable limits).

Kwa msingi huo, hata viongozi wetu katika kufanya maamuzi, wanapaswa kuzingatia hilo ili wasiharubu, na pia ili wasionee watu.

Mwendazake katika kufanya maamuzi, kuna wakati ni wazi alipitiliza na alionea sana watu, na ndio maana tuliona baadhi ya aliowaondoa katika nafasi zao, baadae aliwarudisha(inaonyesha aligundua makosa yake).

Sasa huyu Mama yetu anaonekana kuwa ni kinyume cha Mwendazake kwa kuwa mzito kuchukua maamuzi kwa viwango nachosema ni cha kupitiliza(it is getting too much).

Mfano sahihi ni jinsi anavyokuwa mzito kumuondoa huyu Bosi wa Mapolisi ambae sasa anapigiwa kelele karibu kila kona ila Mama bado haoni kuwa huyu mtu ni tatizo (anapaswa kuondolewa).

Kama anapokea maagizo kutoka juu, njia mowajawapo ya kurekebisha hali hii bado itabaki kuwa ni kumuondoa na kumpangia kazi nyingine, na mrithi wake asiingiliwe vinginevyo hatua ya kumuondoa itakuwa haina maana.

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama Mama ataendelea kupuuza hizi sauti, basi awe tayari kukubaliana na matokeo, na sijui kama kuna binadamu wa kushindana na Mungu.

Hata Mwendazake alimlinda sana Bashite na kupuuza sauti ya walio wengi, ila mwisho wa siku yalimshinda.

Too much of everything is harmful-Mama utajionea siku si nyingi

Time will tell.
Naomba kutofautiana na wewe, Mama sio mzito bali ni mtu utulivu mwenye subra na hakurupuki wala hana maamuzi ya papara. Kufuatia watu kuzoeshwa kupelekwa mchaka mchaka, kuperekeshwa na maamuzi ya pupa, papa na kukurupuka, watu mnakuwa mmeizoea hali hiyo, hivyo inapotokea ameondoka ghafla na kuingia mtu mstaarabu, mtaratibu, muungwa, mnamuona kama ni mzito. Tulieni tuu mtazoea!.

Au mnataka Mama aanze kufanya mambo ya hivi...
P
 
Read between lines.
 
Kila kitu kinachofanyika, kutendeka au kutendwa, kinapaswa kuwa katika kiwango ambacho hakipungui sana au kuzidi sana(kiwe within reasonable limits).

Kwa msingi huo, hata viongozi wetu katika kufanya maamuzi, wanapaswa kuzingatia hilo ili wasiharubu, na pia ili wasionee watu.

Mwendazake katika kufanya maamuzi, kuna wakati ni wazi alipitiliza na alionea sana watu, na ndio maana tuliona baadhi ya aliowaondoa katika nafasi zao, baadae aliwarudisha(inaonyesha aligundua makosa yake).

Sasa huyu Mama yetu anaonekana kuwa ni kinyume cha Mwendazake kwa kuwa mzito kuchukua maamuzi kwa viwango nachosema ni cha kupitiliza(it is getting too much).

Mfano sahihi ni jinsi anavyokuwa mzito kumuondoa huyu Bosi wa Mapolisi ambae sasa anapigiwa kelele karibu kila kona ila Mama bado haoni kuwa huyu mtu ni tatizo (anapaswa kuondolewa).

Kama anapokea maagizo kutoka juu, njia mowajawapo ya kurekebisha hali hii bado itabaki kuwa ni kumuondoa tu na kumpangia kazi nyingine, na mrithi wake asiingiliwe, vinginevyo hatua ya kumuondoa itakuwa haina maana.

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama Mama ataendelea kupuuza hizi sauti, basi awe tayari kukubaliana na matokeo, na sijui kama kuna binadamu wa kushindana na Mungu.

Hata Mwendazake alimlinda sana Bashite na kupuuza sauti ya walio wengi, ila mwisho wa siku yalimshinda.

Too much of everything is harmful-Mama utajionea siku si nyingi

Time will tell.
Nchi iko mikononi nje ya Ikulu
 
Bila kupepesa macho alitakiwa aanze na Pm , waziri wa afya,naibu wake hao watu ni waongo sana na wana ndimi mbili. Taifa likiwa na viongozi wa aina hiyo haliwezi kufanikiwa. Kiujumla anatakiwa kulivunja baraza la mawaziri na kuliunda upya,ama kuhusu hawa Makanda wa taasisi zetu angefanya kama kule takukuru awabadirishe wote,kuanzia Jwtz, police , magereza na huko Tiss, hawa walipewa hizo nafasi kulinda maslahi ya mwenda zake, na siyo Taifa.
 
Naomba kutofautiana na wewe, Mama sio mzito bali ni mtu utulivu mwenye subra na hakurupuki wala hana maamuzi ya papara. Kufuatia watu kuzoeshwa kupelekwa mchaka mchaka, kuperekeshwa na maamuzi ya pupa, papa na kukurupuka, watu mnakuwa mmeizoea hali hiyo, hivyo inapotokea ameondoka ghafla na kuingia mtu mstaarabu, mtaratibu, muungwa, mnamuona kama ni mzito. Tulieni tuu mtazoea!.

Au mnataka Mama aanze kufanya mambo ya hivi...
P
Mkuu nena kwa uhuru naona unamashaka ila unashindwa kuyaweka wazi.....
ninachokiona mimi mheshimiwa rais ana ndimi mbili na sioni utulivu ndani yake zaidi yakutuchanganya alikubali mambo ya tozo katika mihamala akarudi akatuahidi jambo hilo lipitiwe likae katika namna inayotufaa baadae akatoa kauli kuwe wengi tunakubali tozo ila wachache wanakataa jambo ambalo kiuhalisia si kweli kwakuwa hakuna utafiti wowote ulifanyika kupima hivyo viwango na mwitikio wa watu,hivi karibuni kumekuwa na mfumuko katika bidhaa/vitu mbalimbali kama gesi waziri husika akatoa tamko kwa bei irudi kama awali ndani ya siku 14 hadi leo kimya,hili swala la luku nalo hajalisimamia vizuri ni wizi mtupu ndani ya miezi minne tunawezakumuweka katika mizani nadhani itaelemea upande wake,kwa kifupi ni kwamba mimi na walio wengi hatuelewi msimamo wake,...sioni usikivu unaotaka kutuonyeshea kwamba upo
 
Back
Top Bottom