Rais Samia amemsifu waziri Jenista Mhagama kwa kazi anayoifanya ndani ya Serikali. Hata Ummy nae alisifiwa hivi hivi na Kuvimba Kichwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Jimbo la Peramiho, Mkoa wa Ruvuma linaloongozwa na Jenista Mhagama, amemsifu mbunge ambaye ni Waziri wa Afya kwa kazi anayoifanya ndani ya Serikali.

"Nalishukuru tumbo lililomleta Jenista Mhagama, mimi pamoja na kwamba ni Rais, lakini namwita kiraka changu. Nikiona mambo huku yameharibika nampeleka na niwahakikishie hakuwahi kukosea," amesema.

Mhagama amekuwa Waziri kwa kipindi kirefu akihudumu wa wizara mbalimbali ikiwamo ya Sera, Bunge na Uratibu na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Soma Pia: Waziri Jenista Mhagama agalagala chini ikiwa ni ishara ya kumshukuru Rais Samia kwa miradi jimbo kwake

Chanzo
: mwananchi_official

Ummy aliinuliwa Ukumbini na kupewa Sifa Kem Kem na kujiona kamweka Mama Kiganjani ghafla tu akatumbuliwa!!!!
 
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Jimbo la Peramiho, Mkoa wa Ruvuma linaloongozwa na Jenista Mhagama, amemsifu mbunge ambaye ni Waziri wa Afya kwa kazi anayoifanya ndani ya Serikali.

"Nalishukuru tumbo lililomleta Jenista Mhagama, mimi pamoja na kwamba ni Rais, lakini namwita kiraka changu. Nikiona mambo huku yameharibika nampeleka na niwahakikishie hakuwahi kukosea," amesema.

Mhagama amekuwa Waziri kwa kipindi kirefu akihudumu wa wizara mbalimbali ikiwamo ya Sera, Bunge na Uratibu na Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Chanzo: mwananchi_official

Ummy aliinuliwa Ukumbini na kupewa Sifa Kem Kem na kujiona kamweka Mama Kiganjani ghafla tu akatumbuliwa!!!!
Jenista amejiongeza kwa kwenda some miles a head
IMG_2954.jpeg
 
Nimekumbuka ya yule wadhili aliesakata rhumba na kuruka majoka akikata na kuyarudi mithili ya fifi motoo..

Mzee alikula kichwa jumla... Hadi leo chenga chengaa
 
Back
Top Bottom