Rais Samia amemteua Brigedia Jenerali Yohana Ochalla Mabongo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC). Jenerali Mabeyo kwa sasa ana umri wa miaka 65, inawezekana ndiyo anastaafu na maandalizi ya mrithi wake yameanza.
Inasemwa kuwa mtu anayeshika nafasi ya CDF ni mwenye cheo cha Brigedia Jenerali, ambapo ikiwa Rais hawataki wenye vyeo hivyo kushika nafasi hiyo basi option aliyonayo ni kuwaondoa watu hao jeshini ili kumpa unafuu wa kuongoza jeshi mtu atayemteua kushika nafasi ya CDF. JPM baada ya kumteua Mabeyo inasemwa kuwa Mabeyo alipata upinzani kutoka kwa mabrigedia wengine na ndipo wakaondoshwa jeshini kwa kupewa teuzi sehemu mbalimbali ili Jenerali Mabeyo aongoze jeshi vyema.
Uteuzi wa Brigedia Mabongo inaweza kuwa ndio utekelezaji wa OPTION ya kuwaondoa watu hawa jeshini na pia inaweza kuwa ishara kuwa CDF mpya atapatikana karibuni. Ingawa sijui kama uteuzi wa huyu brigedia unamuondoa jeshini (kwa maana ya kuendelea na majukumu ya kila siku ya kijeshi) au la. Wenye uelewa na haya mambo tupeni ufafanuzi.
View attachment 2134005
Mleta mada kabla ya kuleta Mada za kijeshi kwanza uwe na uhakika na utafiti kwa kile unachokileta,,Jeshi ni taasisi nyeti ambayo kama hauko makin unaweza lisha watu matango pori,,
Kwa ufupi huwezi kuwa polisi aina ya OCS ukarukishwa kuwa mkuu wa RPC.
Kwa ufafanuzi mara zote ,vyeo vya jeshi vya jeshi viko hivi kuanzia na oficcer wa chini kabla haujafika kwenye Generali mwenyewe,,
1.kwa cheo cha kwanza cha officer wa chini wa jeshi anaitwa Oficcer Cadet au anaitwa Ofisa mteule,mara nyingi huyu anateuliwa na kupelekwa mafunzo ya kiofisa kwa ajili ya kuja kuwa Luteni usu,na huyu afisa mteule huwa anapewa nyota moja ambayo ukitaka kumjua nyota yake hua rangi ya dhahabu kawaida kama zingine ila iko kwenye kivuli cha rangi nyeupe katikati,
2. Luteni usu,huyu ni afisa wa jeshi au second Lieutenant,huyu ni afisa wa jeshi kwa cheo cha Luten kamili ngazi ya pili mwenye nyota kamili moja,,na ukitaka kutoutisha na officer candidate huyu nyota yake inakuwa haiko kwenye kivuli cheupe,
3. Luteni,hii ni ngazi ya kiofisa ambayo huyu askari anakuwa ni Luteni ngazi ya juu yenye nyota mbili,
4. Capteni, huyu ni officer wa jeshi mwenye nyota tatu begani,so ukitoka Luteni unaenda Capteini,
NB: Hivi vyeo vitatu kwa maana Luteni usu,Luteni na Capteni ni maofisa wa jeshi kwenye rank ya Junior officers.
Kuanzia namba tano(5) mpaka 7 hapa ndo tunaingia kwa magwiji wa siri za jeshi na nchi kwa ujumla,hawa wanaitwa wasaidizi wa kutoa maamzi ya jeshi.
5.MEJA, hiki ni cheo cha juu cha kijeshi baada ya Capteni, na ili kumjua askari ni MEJA jeshini utamkuta begani gwanda lake lina nembo ya BIBI NA BWANA,,huyo ndo MEJA
6. LUTENI KANALI, hiki ni cheo cha juu cha jeshi baada ya Meja,na kumtambua askari kuwa ni Luteni kanali anagalia begani gwanda lake litakua lina nembo ya BIBI NA BWANA halafu na NYOTA MOJA,
7. KANALI,hiki ni cheo cha juu cha jeshi baada ya Luteni kanali,na ili kumtambua kanali utamuona gwanda lake lina nembo ya BIBI NA BWANA na NYOTA MBILI BEGANI,
NB.kuanzia cheo cha Meja,Luteni kanali na kanali hawa wanaitwa Senior officcers jeshini,
Kuanzia namba nane 8 mpaka magogoni huko ndo watoa maamzi kamili na wenye kumiliki siri za jeshi na nchi kwa ujumla.
8. BRIGEDIA JENERALI, huyu ni afisa wa jeshi wa juu baada ya kanali ambaye yuko kwenye sytem nyeti,,na ukitaka kumjua utamtambua kwa kuona bega lake kwa gwanda likiwa na nembo ya BIBI NA BWANA, NYOTA MOJA na MKASI,gari yake inakua na nembo ya nyota moja mbele,huyo ndie Brigedia Generali wa jeshi,,gwijiiiiiii
9. MEJA JENERALI, hiki ni cheo cha juu cha jeshi baada ya Brigedia Jenerali,,haya majina yana uzito wake kuyataja sio kitoto, na ukitaka kumtambua akiwa na gwanda,ww anagalia utaona bega limechafuka vitu vifuatavyo, NEMBO YA BIBI NA BWANA,NYOTA MBILI na MKASI, gari yake inakua na nembo ya nyota mbili,huyo ndio MEJA JENERALI
10. LUTENI JENERALI,cheo cha juu zaid jeshini baada ya Meja jenerali,,hatariii
Ukitaka kumtambua huyu high rank officer,ibia macho yako juu ya gwanda la bega lake utaona nembo zifuatazo zimesimama, nembo ya BIBI NA BWANA, NYOTA TATU na MKASI,gari yake inakua na nembo ya nyota tatu, huyo ndo MEJA JENERALI JESHINI,,ni wachache sana,
11. JENERALI,,,,,,,,,,,,,,,,,hiki cheo kinaitwa FOUR STAR RANK,na hiki ndicho cheo cha juuuu sanaaaaaa jeshini hapa ndo unampata CDF,,na gari yake ina nembo ya nyota 4.
NB: Kuanzia cheo cha Brigedia Generali, Meja jenerali, Luteni jenerali na Jenerali hawa ni kundi la maoficcer wa juu sana jeshini,,linaitwa GENERALI/FLAG OFFICERS.
Kwahiyo CDF anatoka kundi la Three star generals,kwa maana anatoka kwa oficcers wa LUTENI JENERALI akiwa na Three star general rank na kupandishwa kuwa A four star General rank,,na sio kwamba CDF anatoka kwenye kundi la BRIGEDIA JENERALI,,hapa mbali saanaa na ikitokea ni mara moja kwa miaka mia,,
Wajuzi,karibuni!!!