SI KWELI Rais Samia ameomba CHAN iwachukulie hatua Kenya kwa kununua tiketi uwanja wa mkapa

SI KWELI Rais Samia ameomba CHAN iwachukulie hatua Kenya kwa kununua tiketi uwanja wa mkapa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
RAISSAMIA21AG2025.jpg
RAISSAMIA.21AG2025.jpg
 
Tunachokijua
Tovuti ya Shirikisho la soka barani Afrika inaweka bayana kuwa mashindano ya TotalEnergies Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) 2024 yamefika hatua ya mtoano, ambapo ratiba ya robo fainali imethibitishwa baada ya raundi ya mwisho ya mechi za makundi siku Jumanne.

Mashindano hayo yanayoandaliwa kwa ushirikiano na mataifa matatu Kenya, Tanzania na Uganda, mataifa hayo yote matatu yamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, jambo linalochochea hamasa kubwa ya mashabiki katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kupitia mafanikio ya wenyeji hao kwa pamoja, kaulimbiu ya mashindano haya ya “Pamoja” imepata nguvu zaidi, huku Afrika Mashariki ikijiandaa kushuhudia tena viwanja vilivyojaa na uungwaji mkono wa hali ya juu.

Kuelekea mchezo wa robo fainali kati ya Tanzania dhidi ya Morocco utakaopigwa Agosti 22, 2025 majira ya saa mbili kamili usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam kumekuwepo na taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuwa mashabiki wa soka kutoka Kenya wamekuwa wakinunua tiketi za mchezo huo ili kuzuia nafasi kwa watanzania kwenda kushuhudia mechi hiyo.

Kutokana na hiyo ipo nukuu inayosambazwa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu ameomba CHAN iwachukulie hatua Kenya kwa kununua tiketi uwanja wa Mkapa.

Je, ni upi uhalisia wa nukuu hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa nukuu hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani haijatolewa na Rais Samia Suluhu.

Aidha grafiki zilizotumika kusambaza nukuu hiyo ni za kughushi, kwani zimebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo makosa ya kiuandishi.​
Back
Top Bottom