SI KWELI PreGE2025 Rais Samia amesema 'kama uchaguzi wa Oktoba 29 haukuhusu ni bora ukabaki zako nyumbani'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
​
 
Tunachokijua
Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Januari 19, 2025 ulimpitisha kuwa mgombea wa nafasi ya Urais huku Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar.

Mwezi Agosti 9, 2025 Dkt. Samia alichukua fomu ya kugombea Urais katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) akiongozana na mgombea mwenza, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ambao wanajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Madai

Kumekuwepo na picha iliyochapishwa katika kikundi cha mtandao wa Facebook na mtu mwenye utambulisho usiojulikana, ikiwa na ujumbe unaoonekana kuchapishwa na Rais Samia kwenye ukurasa wake wa X ukisema 'kama uchaguzi wa Oktoba 29 haukuhusu ni bora ukabaki zako nyumbani'

Je, ni upi uhalisia wa Ujumbe huo?


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa ujumbe huo haujachapishwa kwenye ukurasa rasmi wa Rais Samia kupitia mtandao wa X.

Aidha ujumbe huo una mapungufu yanayodhihirisha kuwa ni wa kutengenezwa na wapotoshaji. Picha yenye ujumbe huo haiakisi uhalisia kama ilivyo katika mtandao wa X, mfano kutumika kwa tiki ya bluu (blue checkmark) badala ya tiki yenye rangi ya kijivu (Grey checkmark) ambayo inatumiwa na Rais Samia.

Kukosekana kwa alama ya Grok, nukta tatu upande wa juu kulia, umbo la picha katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka mtandao wa X, muonekano wa picha ya wasifu. Pia kwenye mtandao wa X Rais Samia anatumia 'Samia Suluhu' na si Samia Suluhu Hassan kama inavyoonena

Katika siku za karibuni kumekuwa na uwepo wa picha zenye ujumbe kama huo zikitumia utambulisho wa Rais Samia ili kupotosha uhalisia. Rejea hapa, hapa na hapa. Epuka kusambaza machapisho, picha au video ambazo unapata mashaka kuhusu uhalisia wake kabla ya kuthibitisha ili kuepusha upotoshaji.​
Kiburi, jeuri na ufedhuri tu..........!

Mungu mwamuzi wa Haki...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…