Rais Samia ametangaza siku 7 za maombolezo Kitaifa kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda

Rais Samia ametangaza siku 7 za maombolezo Kitaifa kufuatia kifo cha Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda

Kuna kisa nakikumbuka wakati Fredrick Chiluba alipomuweka Mzee Kaunda Jela Mzee Kaunda akafanya mgomo wa kula,Nyerere alipoona hivyo akaondoka mbiombio hadi Lusaka kwenda kumtoa mahabusu Rafiki yake😁
Chiluba alikuwa mtu wa ovyo sana.

Amandla...
 
Kila nafsi itaonja mauti,
Muhimu kujitayarisha vile namna utaondoka
Wakati utakapofika
 
Naikumbuka na ile timu ya Taifa ya soka ya Zambia, ambayo wenyewe Wazambia walizoea kuiita KK11.

Mzee huyu jina lake ni kubwa sana katika Afrika kutokana na yale aliyoyafanya.

Keneth Kaunda alikuwa ni kiongozi, mwanamapinduzi na mwanademokrasia wa kweli. Licha ya kuwa mkuu wa vyombo vyote vya dola na vya kiutendaji vya Serikali, aliruhusu demokrasia imee na kustawi nchini mwake. Hakuruhusu wizi wa kura, hakuruhusu kutangazwa walioshindwa kuwa washindi kama ilivyo hapa kwetu. Alikuwa kiongozi miaka mingi iliyopita lakini mwenye fikra kisasa wakati wote.

Mwenyezi Mungu ulinena kuwa kuishi miaka mingi ni neema na ni thawabu, nina imani ulimpa mzee huyu umri wa kutosha wa kuwa hapa Duniani kutokana na mema yake. Sasa umemwita kwako, tunakuomba uyaoshe mapungufu yake kwa mema aliyotyatenda, na kwa hekima yako, tunakuomba, umvishe cheo kikubwa cha utakatifu katika ufalme wako.

Kwa heri Mzee Kaunda. Maisha na uongozi wako iwe shule kwaajili ya watawala wengi wa Afrika ambao kwao haki, demokrasia, utawala wa sheria na uadilifu, ni adimu kuliko jiwe la almasi.
 
Kizazi cha dhahabu cha Waafrika wapigania uhuru ndio almost kwishiney
 
Vipi mwakilishi gani amekwenda kuzika huko ?

Kama wamekosa watume hizo ticket hapa kwangu through JF niende kuwakilisha TZ.... (Dont Worry Tavaa Barakoa)
 
Ni Sawa kabisa KK ni MTU mwenye historia na Taifa hili. Poleni WaZambia. Huwezi kumtaja KK bila kumkumbuka JK Nyerere.
Huyu Kaunda alishindwa urais mwaka 1992 ktk uchaguzi wa vyama vingi,lakini aliwaachia wapinzani kuongoza nchi ingawa alikuwa na uwezo wa kutumia nguvu,hakuiba kura ingawa uwezo wa kuiba alikuwa nao. Aliheshimu sana mawazo ya wengi kupitia democracy. Hapa kwetu tuna la kujifunza ili tubadilike au tutabadilishwa kwa nguvu ya wakati na dunia.
 
Hivi unaachaje, kwa mfano, kwenye hii orodha kumtaja JPM, Anko Magu, Bulldozer, Tingatinga, Jembe, Chuma!??? Au akaunti yako imedukuliwa!??? Unajua JPM amefanya hata makaburi ya hao wazee wetu wapigania-uhuru, watetezi wa utu na rasilimali za Afrika, yasafishwe na kuonekana vizuri upya.
Huyo ni saizi ya kina Mwigulu.
 
Huyu Kaunda alishindwa urais mwaka 1992 ktk uchaguzi wa vyama vingi,lakini aliwaachia wapinzani kuongoza nchi ingawa alikuwa na uwezo wa kutumia nguvu,hakuiba kura ingawa uwezo wa kuiba alikuwa nao. Aliheshimu sana mawazo ya wengi kupitia democracy. Hapa kwetu tuna la kujifunza ili tubadilike au tutabadilishwa kwa nguvu ya wakati na dunia.
Nakumbuka tukio moja Baya kijana wake Wezi Kaunda aliuawa sikumbuki vizuri lakini hakuwa picha nzuri Kwa utawala WA wakati huo walimkosea Sana Mzee WA WA watu.
 
Apumzike kwa amani Mzee wetu KK, atufikishie salamu zetu kwa NYERERE, KENYATA, MANDELA, NKURUMAH na wapigania uhuru wengine wa Afrika. True Sons of Africa. Wapumzike kwa amani wote
Mkuu, Mbona hutumi Salamu kwa Shujaa wa Africa, Namaanisha Mwendazake Jiwe
 
Kenneth Kaunda death: Botswana President Masisi declares 7-day mourning​

FRIDAY JUNE 18 2021​

Kenneth Kaunda.

Zambia's former President Kenneth Kaunda. PHOTO | AFP
ADVERTISEMENT

General Image

By ARNALDO VIEIRA
More by this Author

Botswana President Mokgweetsi Masisi has declared a seven-day mourning period following the death of Zambia's founding President Kenneth Kaunda.

“I have learnt of the demise of Dr Kenneth Kaunda, the founding father of the Republic of Zambia, a great statesman, and African leader. In honour of this great son of the soil, I have declared a seven-day mourning period in Botswana during which all flags shall fly at half-mast,” the president said in a statement Thursday.

“Dr Kaunda was Botswana’s best friend and together with the likes of Sir Seretse Khama and Mwalimu Julius Nyerere, championed the liberation and independence of our region...Former President Kaunda’s death is a loss to his compatriots in Zambia, their friends in Botswana, and the continent of Africa. We send our condolences to the people of Zambia during this trying time”.

He said Dr Kaunda was the first Head of State to visit Botswana shortly after independence in 1966.

“His four-day State Visit to Botswana, from May 21st, to May 24, 1968 ushered in a period of unparalleled excellent bilateral relations between Botswana and Zambia; after Zambia attained its own independence from British colonial rule which saw Dr Kaunda assuming the first presidency of the country in 1964.”
 
Tuomboleze kama Nani , hii nchi hatujawah kujua nini hasa lengo letu
 
Tuomboleze kama Nani , hii nchi hatujawah kujua nini hasa lengo letu

..katika Maraisi wa Afrika Kenneth Kaunda tunaweza kusema alikuwa rafiki kipenzi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.

..katika kuomboleza msiba wa Mwalimu Nyerere, Mzee Kaunda alishiriki kwa karibu kama mwanafamilia.

..Mzee Kaunda alitufariji Watanzania kwa maneno ya nasaha na utenzi maalum kwa rafiki na kaka yake Julius Kambarage Nyerere.

..Reli ya Uhuru / Tazara toka Dar Es Salaam mpaka Kapiri Mposhi ni alama ya undungu tulioachiwa na waasisi wetu Julius Nyerere na Kenneth Kaunda.
 
TAZAMA PIPELINE!
 
Back
Top Bottom