kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Timu zetu zilikuwa hazifanyi vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa. Vilabu na timu za taifa zilikuwa zinafungwa na hata vinchi vidogo na vyenye vurugu kila siku kama Burundi na Rwanda. Hii ilimfanya Rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kuzifananisha timu zetu na kichwa cha mwendawazimu ambacho kila mtu anajifunzia kunyoa nywele (ukinyozi).
Awamu ya sita ya Rais Dr. Samia mambo yamegeuka kama vile mtu aliyetumwa kunya kuondosha yale maneno mabaya ya Mzee Mwinyi kwa timu zetu. Timu zetu sasa zinashinda, Yanga na Simba, timu ya taifa, timu za vijana na wanawake na walemavu kwenye awamu hii ya mama zote zinafanya vizuri. Ameondoa gundu.
Tumuombe tu aseme na wana CCM wenzake waone aibu kuvishikilia viwanja vyote vya mpira na kudai ni vyao wavirudishe serikalini na TFF ili vipangiwe bajeti na mikakati ya kuvikarabati na kuvitunza.