Rais Samia amteua Dkt. Immaculate Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu NEMC

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Immaculate Sware Semesi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhifadhi wa Bahari na Maeneo Tengefu na anachukua nafasi ya Dkt. Samuel Gwamaka Mafwenga ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu unaanza tarehe 05 Januari, 2024.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

 
Hongera SANA Dkt
 
Huyu siyo Rais, ni mpitaji tu
 
Kikubwa ni mtanzania na ni msomi mbobevu,ana utaalam husika wa kuisaidia nchi. Pongezi kwake
Tanzania issue siyo utaalam issue ni sera mbovu, hapo juu kuna Rais, Makamu, PM, Sijui Naibu PM, Waziri, KM, Wabunge, RC na takataka zingine hazitaki utalaam zaidi ya wizi na ufisadi na maamuzi mabovu, ingekuwa yeye ndiyo final say utalaam wake ungefanya kazi.
 
Haya na wewe nenda katoe vibali hovyo hovyo matajiri wakajenge vituo vya kuuza mafuta kwenye makaazi ya watu.
 


Hongera zake yupo kwenye group ya Tambaza form 6 1996.
 
Mimi

Nimeteuliwa kuwa Admini wa grupu la wasapu la lumumba buku 7.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…