Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani Mheshimiwa George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania. Mheshimiwa Masaju anachukua nafasi ya Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu.
Uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika tarehe 15 Juni, 2025 Ikulu, Chamwino Dodoma kuanzia saa 4.00 asubuhi.
2009 - 2015: Bwana Masaju, aliyewahi kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Januari 02, 2015 - Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi alioendelea kuwa nao hata wakati wa Magufuli
Februari 01, 2018 - Aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Magufuli alimteua George Mcheche Masaju kuwa Jaji wa Mahakama Kuu
Aprili 20, 2023 - Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alimteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President - Legal Affairs), akiwa bado ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Januari 10, 2025 - Rais Samia Suluhu alimteua Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Juni 13, 2025: Rais Samia amemtua kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu Ibrahim Juma