Rais Samia amteua Jaji George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania

Jaji Mkuu Masaju ndio pekee mwenye mamlaka ta kumuapisha Rais atakayeshinda kidemokrasia uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
 
Kibaraka, hamna kitu hapo ni maumivi matupu
 
Niseme tu bwana Ibrahim Juma kama ilivyo kwa Bi Tulia Akson mumekuwa viongozi wabovu wa mihimili na bahati mbaya sana mmekutana kipindi kimoja. Bahati mbaya iliyoje kwa watanzania, na cha moto tumekiona kutokana na udhaifu wenu!

Kuwa na mhimili hii dhaifu dhidi ya serikali kwa wakati mmoja huku mkifahamu kuwa ni kimbilio la umma kumeleta kilio kikubwa kwa watanzania wapenda haki.

Umeondoka Bwana Ibrahim naamini pia mwandani wako Tulia nae ataondoka. Je tutapata upenyo wa kuibadili hii mihimili ili irudi kuwa kimbilio la watanzania? Tunasubiri.
 
Alichemsha sana Pale Bungeni TAL alikua anamgaragaza kama mwanae. Mpaka mtemi Chenge anakuja kuokoa jahazi,halafu kibaya zaidi Chenge akija anatoa hoja halafu anamaliza kwa kukubaliana na mapendekezo ya TAL. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kumbe ni yule!
 
Kwa namna yoyote ile kuna tatizo kubwa kwenye idara zinazomzunguka mteuzi..nafasi nyingi za uteuzi kwa sasa zimeegemea sana mkoa wa mara, kwa mara nyingine anateuliwa Jaji mkuu kutoka mara tena, kumbuka makamu mwenyekiti wa ccm ni kutoka mkoa wa mara..na wengine wengi, mafuru aliyepita, mafuru wa utalii, mkurugenzi wa tanesco aliyekufa, mkurugenzi wa benki ya kilimo, juzi tu bwn nyasaho mkurugenzi psssf..ni km vile tiss ina watu wengi kutoka mkoa wa mara ndio maana ni rahisi sana kuconspire kufanya uovu na kuutetea..jibu la hali km hii ni katiba mpya, mamlaka za kufanya vetting na uteuzi ha,iwezi kuwa chini ya watu wachache kutoka mkoa mmoja!
 
Ingawa nafahamu kwamba kuna utaratibu wa rais kumteua jaji mkuu hata hivyo kwa uteuzi huu wa jaji Masaju mimi naona kama ifuatavyo;Jaji George Masaju jaji wa mahakama ya rufani Tanzania ameteuliwa kuwa jaji mkuu wa mahakama ya Tanzania. Jaji George Masaju mbali na kuwa jaji wa mahakama ya rufani pia alikuwa mshauri wa rais wa masula ya sheria,kwa maana hiyo jaji Masaju ndo kamshauri rais amteue jaji Masaju kwa tafsiri nyingine jaji Masaju amejiteua kuwa jaji mkuu. Ingekuwa nchi kama Kenya uteuzi huu ungepingwa mahakamani na ungetenguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…