Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Historia imeandikwa, historia imevunjwa chini ya Mh John John Mnyika Katibu Mkuu wa Chadema.
Mnamo Tarehe 21 January 2025 kulifanyika uchaguzi Mkuu katika Chama Hicho. Uchaguzi huo ulijaa kashi kashi za kusigana kati ya miamba miwili katika chama kikuu cha upinzani Nchini Tanzania.
Awali ilionekana kutokana na moto mkali huenda uchaguzi huo usifanikiwe kwani dalili nzito zenye viashiria hatari vilianza kuonekana katika makundi mawili au matatu ya ushindani.
Upande mmoja ukiwa ni wa Anayemaliza Nafasi ya Mwenyekiti Taifa, Upane wa aliyekuwa Makamu mwenyekiti na Wengine wakiwa hawana Upande wowote.
Nchi na vyombo vya nchi vilisimama, vilikaa chonjo, vikalala tongo macho yaani Sleeping Eye Open. Wengine wakisema baada ya uchaguzi huo Chadema unajifia kifo cha mende iwe kashinda mwenyekiti au Makamu.
Upande wa serikali walijiandaa kweli kweli. Pongezi kwa wahusika.
Hata Hivyo JJ Mnyika akaonesha ukomavu, kipaji, uwezo, ujuzi na maarifa kama. Katibu Mkuu aliyekuwa Mwamba ktk uchaguzi huo. Akiwa ndiye Mtendaji Mkuu na msimamizi wa shughuli zote za Uchaguzi.
Nchi ilizizima, Nchi ilijaa hofu, asiwepo wakujua nini kitatokea hapo wakati na baada ya uchaguzi.
Hakika Historia imeandiwa!
Basi wakaalikwa Maustadhi, Mashekhe, Mapadre, Maaskofu na Mafadha. Mialiko ikavuka mipaka ya afrika mashariki, wakaja wageni kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, kongo pia haikuachwa nyuma.
Mialiko.ya watu mashuhuri ikafanyika ikavuka Nchi na Mabara, Korea wakaja, Urusi wakawepo, Wachina pia😅
Mabalozi kila rafikinna muhisani akawiwa kuhudhuria, yayumkinika hata wale ambao wahakupewa Mwaliko basi waliomba wenyewe waje washuhudie. Walivutiwa na mchakato.
EU, United States, SADC, EAC, mabalaza yote ya haki na amani Tanzania yaliomba kuhudhuria na yakapewa nafasi.
Hili jambo sio la kawaida hata kidogo. Rudia kusoma tena.
Basi tuseme nini Juu ya Kiongozi Huyu JJ Mnyika? Kama mlikuwa hamjaona Kipaji chake, uwezo na umahiri wake basi umeonekana na tunajaribu kuwaonesha. Mnasubiri Nini?
Kwa Heshima Na Taadhima, Tunamuomba Mh Rais Dr Samia Suluhu Hassan amteua Kijana Huyu Akaitumikie Nchi. Ampe ukamishina katika Tume Huru Ya Taifa ya Uchaguzi, mamalaka anayo.
Maendeleo hayana Vyama.
Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Rais Samia.