Kwa hii video sina la kuongezea...karibuni
View attachment 2071433
Toa maoni yako...
Mkuu
Mag3
Kuna viumbe hawaelewi hadi yawafike .
Ndugai hakubaliani na katiba mpya hata siku moja. Anadai mifumo ipo sawa kwasababu ya Uspika na marupu rupu yake na Familia. Leo pale Kongwa hawezi kukubaliana na hoja hiyo tena
Nape alifungia uhuru wa habari hadi yalipomfika akikabiliana ana kwa ana na punje za shaba
Leo Nape anaelewa maana ya uhuru ni nini, udikteta nini na haki za watu ni nini
Polepole alikuwa katika rasimu ya Warioba. Alizunguka nchi nzima akipiga kelele za Katiba mpya.
Alipopewa ulaji, Polepole yule yule akasema katiba si muhimu tena bali uchumi
Majuzi kaondolewa karudi kusema katiba si kipaumbele mama aachwe afanye kazi
Wiki iliyofuata kasema katiba inaandikwa na Rais anayeondoka
Polepole mmoja ana 'evolve' kila baada ya miaka kwasababu ya utamu.
Juzi kashtakiwa na 'hakuna' kahukumiwa na TCRA na kuzibwa mdomo wa uhuru wa maoni ambayo ni haki yake. Leo Polepole yule anayegeuka atakwambia katiba mpya ni muhimu
Hatuwezi kufanikiwa kuongea lugha moja na hawa viumbe kama hawapitii madhila.
Yes hoja ya Ndugai ni muhimu lakini kuondoka kwakwe ni muhimu zaidi. Ndugai kanajisi Bunge sana pengine anguko la pua ukichanganya na wengine linaweza kutusaidia kutoa funzo
Kwamba, tunahitaji haki kama Raia kupitia katiba na kwamba anayekaa mbali au asiyetaka kushiriki ipo siku katiba hiyo hiyo itamweka kitako kama si yeye ni mwanae au mjukuu
JokaKuu