Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa

Slaa haaminiki alinunuliwa kwa vipande 30 vya fedha na CCM akaisaliti chadema hana tofauti na yuda iskariot wa enzi za Yesu kristo.
Sir Elton John Robert mambo yako ya kupumuliwa kisogoni peleka hukohuko na kwa nini ufiche jina lako la kwanza Elton
 
Wewe mzee hebu jitafakari kama akili yako ipo sawa. Ulianza kuvuliwa upadri , Ukaingia kwenye siasa Chadema wakakuvua uanachama baada ya kusaliti chama chako na kuingia CCM. Leo hii tena umevuliwa Ubalozi cheo ulichopewa na CCM baada ya kuhama kutoka Chadema.

Kama mtu mzima lazima ujiulize wewe una matatizo gani? Kwanini kila ulipo jamii inakukataa.?

Nakushauri achana na mambo yote kaungame kanisani kwako ubaki muumini wa kawaida na utubu kwa Mungu akusamehe makosa yako.

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Sir Elton John Robert mambo yako ya kupumuliwa kisogoni peleka hukohuko na kwa nini ufiche jina lako la kwanza Elton
 
DKt Wilbroad Slaa amevuliwa hadhi ya ubalozi kuanzia leo Septemba 1, 2023. Taarifa imetolewa hivi punde na Ikulu katika mtandao wa kijamii wa X ama Twitter.

Hayati Rais John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Willibroad Slaa ambaya ni Katibu Mkuu wa zamani wa chama cha Upinzani, CHADEMA kuwa Balozi mnamo Novemba 23, 2017

Julai 22, Dkt. Slaa alizungumza na Wananchi kupitia vyombo vya habari akisema ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi kuhusu kasoro zilizopo kwenye mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Aliweka wazi kuwa hapingi uwekezaji katika bandari hiyo ya Dar es Salaam bali anapinga mkataba wa uwekezaji kwa kueleza kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Aidha, siku hiyo alisema “Najua maneno hayo ni makali… nimepokea vitisho na mimi pia sio tu Mawakili, wengine wakasema ubalozi wako tutachukua, nawaambia chukueni sasa hivi, siishi kwa ajili ya ubalozi. Nimesema sina chama najiamini najau ninachosimamia“

View attachment 2735983

=====
WILLIBROD PETER SLAA NI NANI?
View attachment 2735984
Dk Slaa alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1948 wilayani Karatu. Alipata elimu ya msingi katika shule za Karatu na Kwermusi (Mbulu) kati ya mwaka 1958 na 1965.

Alisoma elimu ya sekondari katika Shule za Dung’unyi Seminari na Itega Seminari kati ya mwaka 1966 na 1971.

Ni kiongozi mwenye stashahada tatu pamoja na shahada ya Uzamivu (PhD). Anayo Shahada ya Uzamivu (PhD ) katika Sheria ya kanisa kutoka Chuo Kikuu cha St. Urban, Rome. Pia anastashahada ya Theolojia kutoka Kipalapala Seminari, Stashahada ya falsafa kutoka Kibosho Seminari, Stashahada ya Afya ya Macho kutoka Kituo cha Kimataifa cha Macho.

Amewahi kuwa padri wa Kanisa Katoliki kuanzia mwaka 1977 hadi 1991, akishika nafasi za kiutawala katika kanisa pia. Amepata kuandika vitabu vitatu ambavyo ni Utimilifu wa Msichana (1977), Utimilifu wa Mvulana (1977) na Expediency and exigency Liturgical Legislation (1981).

Ni mzungumzaji wa Lugha nane kwa ufasaha; ambazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kilatini, Kiitaliano, Kijerumani, Kihispania, Kireno na Kifaransa.
Siku ya Alhamisi, Novemba 23, 2017 Aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alimteua Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kuwa balozi. Alikuwa Balozi wa Sweden, pia ailiidhinishwa kwa Nchi za Denmark, Finland, Norway, Iceland, Estonia, Latvia, Ukraine na Lithuania.

Kipindi Dk Slaa anateuliwa kuwa Balozi, alikuwa anaishi Canada, alitangaza kuachana na siasa kutokana na kutofautiana na chama chake katika kumpokea Edward Lowassa aliyehama kutoka CCM na baadaye kumpitisha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa vyama vya siasa wa Ukawa.

Pia, soma: Balozi Dkt. Wilbroad Slaa kuvuliwa ubalozi na kukamatwa!
Siku zote za maisha ya siasa zingatia!

Siasa haina adui au Rafiki wa kudumu. Adui yako wa leo kwenye siasa anaweza kuja kuwa rafiki mzuri sana na rafiki yako wa sasa katika siasa anaweza kuja kuwa adui mkuu sana, chukua hii utakuja kunishukuru [emoji3516][emoji3516]
 
Mwenyewe amefafanua CLUBHOUSE yaani karatasi ya mistari haina athari kwake hadhi za ubalozi ni more advanced
 
CCM ni ileile. Samia hatekelezi mambo yake bali anayoagizwa na CCM maana ndiyo imeunda serikali na kumuweka hapo. Samia hana ubavu wa kuivimbia CCM. Hata Mkapa aliwahi kumkemea Magufuli waziwazi tena matangazo yakiwa live kuwa serikali ni ya CCM na sio ya mtu so aache kusema serikali yangu.

Ukiangalia kwa makini unagundua kwamba wakati Samia anachukua kitu cha uraisi alizungumza mambo mengi kuwa atayabafilisha yaende tofauti na alivyokua anafanya Magufuli. Kumbe alisahau Magufuli alikua kioo tu cha kumulika yale yanayotakiwa kufanywa na CCM. Sasa Samia ameijua CCM halisi na amegundua alikua anajidanganya.

Magufuli alipodaiwa katiba mpya alisema yeye kwenye kampeni hakuahidi katiba, watu wakaona kama anayesema ni Magufuli wakasahau nguvu ya magufuli ni CCM iliyomuweka pale. Samia mwaka jana akakurupuka kuanza mchakato wa katiba, CCM wamemwita na kumpa za uso. Ukiuliza sasa hivi mchakato una hali gani hana jibu la maana.
Akaahidi kuleta maridhiano na wakosoaji wa serikali. Sasa Slaa karuka naye kwenye jambo moja tu tayari kavuliwa ubalozi. Waliopo karibu wanajua Samia alikua anaahidi abadi hewa. Hakuijua CCM halisi, mwakani subirini yale ya 2920 yatakavyoshamiri na Samia hatanyanyua hata neno moja kukemea.

CCM NI ILEILE, WANAOBADILIKA NI WATU
 
kizazi cha sasa kina uwezo mdogo sana wa kufikiri mambo.....

Dr slaa amekuwa wazi kwenye misimamo yake tangu enzi na enzi.... na ni mtu anaetetea maslahi ya taifa..
kuvuliwa hadhi ya ubalizi kwake hakuwezi kumyumbisha....
Wenye akili tumekuelewa mkuu
 
Wakimaliza wanahamia na kwako kuja kukuvua uanaume wako, maana una pigo za ki upinde wewe
CCM ni ileile. Samia hatekelezi mambo yake bali anayoagizwa na CCM maana ndiyo imeunda serikali na kumuweka hapo. Samia hana ubavu wa kuivimbia CCM. Hata Mkapa aliwahi kumkemea Magufuli waziwazi tena matangazo yakiwa live kuwa serikali ni ya CCM na sio ya mtu so aache kusema serikali yangu.

Ukiangalia kwa makini unagundua kwamba wakati Samia anachukua kitu cha uraisi alizungumza mambo mengi kuwa atayabafilisha yaende tofauti na alivyokua anafanya Magufuli. Kumbe alisahau Magufuli alikua kioo tu cha kumulika yale yanayotakiwa kufanywa na CCM. Sasa Samia ameijua CCM halisi na amegundua alikua anajidanganya.

Magufuli alipodaiwa katiba mpya alisema yeye kwenye kampeni hakuahidi katiba, watu wakaona kama anayesema ni Magufuli wakasahau nguvu ya magufuli ni CCM iliyomuweka pale. Samia mwaka jana akakurupuka kuanza mchakato wa katiba, CCM wamemwita na kumpa za uso. Ukiuliza sasa hivi mchakato una hali gani hana jibu la maana.
Akaahidi kuleta maridhiano na wakosoaji wa serikali. Sasa Slaa karuka naye kwenye jambo moja tu tayari kavuliwa ubalozi. Waliopo karibu wanajua Samia alikua anaahidi abadi hewa. Hakuijua CCM halisi, mwakani subirini yale ya 2920 yatakavyoshamiri na Samia hatanyanyua hata neno moja kukemea.

CCM NI ILEILE, WANAOBADILIKA NI WATU
Unasemaje? CCM haiwezi kubadilika?
 
Back
Top Bottom