Nachojua Tukio la ajali Kariakoo wakati linatokea Rais Samia alikuwa bado nchini, kaondoka nchini baada ya ya tukio kuwa tayari na taarifa alikuwa nayo, ila akapanda ndege kwenda Brazil, leo anasema wakati tukio linatukia alikuwa tayari safarini kwa nini anadanganya umma?
Taarifa ya Ikulu ilichapishwa saa 5 na dakika 57 kuwa anaagana na viongozi uwanja wa Ndege kwa ajili ya safari, ajali ya Kariakoo imeanza kuripotiwa Majira ya ya saa 3 Soma hapa. Asubuhi hiyo ya tarehe 16 Novemba 2024 ambapo Samia aliondoka majira ya saa 5 hivyo alikuwa bado nchini na alikuwa na uwezo wa kubaki nchini ila hakuona kuwa kubaki nchini lilikuwa ni chaguo bora kuliko yeye kwenda kwenda mkutano wa watu Brazil.
Posti ya Ikulu ikionesha muda wa saa 5 Rais Samia alikuwa nchini.