Rais Samia anaifanya elimu kuwa bora na nafuu

wanzagitalewa

Senior Member
Joined
Jan 25, 2018
Posts
128
Reaction score
84
Lengo namba nne la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 ni kuhakikisha watu wote wanapata elimu bora, yenye usawa na kutoa fursa kwa wote kujiendeleza na kufikia vipawa vyao kikamilifu. Ili kufikia lengo hilo, mamlaka zinatakiwa kutoa fursa sana kwa wavulana na wasichana, kuongeza idadi ya wanafunzi na kuifanya elimu kuwa nafuu zaidi.

Utekelezaji wa lengo hilo umekuwa ukikumbana na changamoto ikiwemo gharama za elimu ambapo uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza sera ya elimu bila ada na kufuta ada kidato cha tano na sita, kuondoa michango isiyo ya lazima na kuboresha mazingira ya ajira kunaisogeza Tanzania hatua mbele zaidi kufikia lengo hilo.

Septemba 15 mwaka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) lilitangaza kufuta ada ya mtihani wa darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita kwa shule za umma ambayo ni TZS 50,000 kwa sekondari na 15,000 kwa shule za mzingi za umma. Watanzania wengi wakiwa ni wenye kipato cha chini, kuondolewa kwa gharama hizi ni ahueni kubwa kwao pamoja na wanafunzi ambao matokeo yao yalikuwa yakizuiwa kwa kutokulipa ada ya mtihani.

Licha ya kuwa kuondolewa kwa fedha hizi kutalikosea baraza mapato takribani TZS bilioni 35, ambayo lilikuwa likiyatumia kujiendesha, Rais amechukua hatua hiyo ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto yeyote anayekosa fursa ya elimu, ikiwa pia ni utekeleza wa matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Hakuna elimu ya bure duniani ,Wanafunzi wanakaa chini,walimu hawana posho ,mishahara haifiki tarehe 10,vitabu vimeota mbawa,elimu ya kukariri,mitihani ni kuchagua swali la Kwanza hadi 45, hiyo elimu ni elimu gani ya kipumbavu!!
 
Huu unafki na kusifiasifia ovyo unapeleka nchi yetu kaburini
 
Hakuna elimu ya bure duniani ,Wanafunzi wanakaa chini,walimu hawana posho ,mishahara haifiki tarehe 10,vitabu vimeota mbawa,elimu ya kukariri,mitihani ni kuchagua swali la Kwanza hadi 45, hiyo elimu ni elimu gani ya kipumbavu!!
Nashukuru Sana kwa kuonesha udhaifu wa elimu yetu kongole mkuu.

je,nini kifanyike kuboresha Elimu yetu iwe sambamba na dunia ya leo?
 
Back
Top Bottom