George Michael Uledi.
August 4,2023.
Kwa lugha rahisi unaweza kusema haijawahi kutokea tangu Uhuru kwa Nchi ya Tanzania kuandaa Jukwaa na Maonyesho Makubwa ya Sikukuu ya Wakulima Nchini yaani NaneNane kwa kushirikisha Nchi jirani tena safari hii yakifanyika katika Jiji la Mbeya,Tanzania.
Uwekezaji huu katika Sekta ya Kilimo ambao haujawahi kufanyika Nchini tangu Uhuru ni muendelezo wa Mapinduzi Makubwa ya Uwekezaji ndani ya Serikali ya CCM ya awamu ya Sita ambayo "imeseti"Bajeti ya Kilimo ya Bilioni 900+ Tsh kwa Mwaka 2023/2024 hivyo kuziacha mbali Nchi za Kusini mwa Ukanda wa SADC.
Serikali ya awamu ya Sita ya CCM imeendelea kuteka Majukwaa Makubwa ya Uwekezaji duniani kwani inatarajia "Kuhost"Mkutano Mkubwa wa Jukwaa la Chakula Duniani utakaofanyika Jijini Dar es salaam September 5-8 Mwaka 2023.
Uwekezaji ndani ya Bandari ya Dar es Salaam unatajwa kama Mkakati wa Maandalizi ya Nchi kuweza "kuexport" Mazao ya Kilimo na Mifugo hasa kwenye Nchi za UAE ambazo mahitaji yake ya Mazao ya Mifugo ni fursa kubwa ya kuweza kuzilisha Nchi hizo za Saudia, Dubai, Qutal na nyinginezo.
Bandari ya Somalialand na Djibouti zinatengeneza fedha nyingi za kigeni kupitia uuzaji wa bidhaa za mifugo kwenye Nchi za soko la UAE.
Ni suala la muda tu kwani Uwekezaji ndani ya Bandari ya Dar hasa sehemu za kutunzia chakula unaweza ukaifanya Tanzania kuwa Best Exporter wa Mazao ya Mifugo ukizingatia Nchi ya Tanzania kitakwimu ni Nchi ya Pili yenye mifugo mingi barani Afrika kwa sasa.
Kuna watu watakimbia Nchi hii kwa AIBU ya kuutukana Uwekezaji wa DP World Dubai ndani ya Tanzania sio mbali,probably Mwaka 2027 hapo.
Nipo pale. Tusubilie tu.