Knockout ya Mama: Rais Samia aguswa na Dulla Mbabe, ampa Tsh Milioni 2 kama zawadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa zawadi ya Tsh Milioni 2 kwa ajili ya Dulla Mbabe ambaye amepoteza pambano lake dhidi ya bondia kutoka Zambia.
Akizungumza katika tukio hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, amesema mapambano ya leo hayana mkanda, hivyo Rais ametoa pesa hiyo kama zawadi kwa mabondia wanaopambana kwa ajili ya kuipeperusha bendera ya nchi.
Hata hivyo, Msigwa alisema mabondia wengine ambao wameshinda wamepewa Tsh Milioni 1 kama zawadi.
Kila nikiona au kusikia habari hizi nafarijika. Upande wa pili wa shilingi nawakumbuka vijana ambao kwa miaka 10 wako unemployed Watanganyika Mungu atusadie.