Rais Samia anaongoza maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya mashujaa -Dodoma

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo katika maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mashujaa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mnara wa Mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.


View: https://www.youtube.com/live/vvJ8gjVKhns?si=w7pu2HxrbmchZaTX
Kila tarehe 25 Julai ya kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya Mashujaa​

Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka. Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini. Pamoja na hayo hufanyika gwaride maalum kwa ajili ya mashujaa wetu.
Your browser is not able to display this video.


Wageni mbalimbali wanaendelea kuwasili katika uwanja wa Mnara wa mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.​

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi wamewasili katika uwanja wa Mnara wa mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Rais Samia amewasili​

Samia Suluhu Hassan ni Rais wa sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wamewasili katika uwanja wa Mnara wa mashujaa, Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

CDF Mkunda ameweka sime kwenye mnara wa mashujaa​

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda ameweka akiweka Sime kwenye Mnara wa Mashujaa katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Mtumba Jijini Dodoma, leo tarehe 25 Julai, 2025.

Rais Samia Suluhu Hassan ameweka Mkuki na Ngao kwenye mnara wa mashujaa​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka Mkuki na Ngao kwenye Mnara wa Mashujaa katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Mtumba Jijini Dodoma, leo tarehe 25 Julai, 2025.
 
Amerudi lini kutoka kizimkaz!!?

Spinning ya Nini hii kimtandao!!?

Kuna ukimya mwingi wa kutoaminika!

Oktoba tuna tick!
 
Mbona sijaona Pole Pole kujibiwa kimafumbo
 
Mashujaa wetu ni Mdude Nyangali, Deusi Soka,Daudi Mwangosi,Mzee Ally Kibao, Ben Saanane, Mawazo na wote waliotekwa, kuteswa, kufanyiwa ukatili, kupotea na kukatishwa uhai wao kwa ajili ya kupaza sauti kupinga dhuluma.

Mashujaa wetu ni Tundu Lissu na wote waliofungwa jela na kuwekwa kizuizini.


Mashujaa wetu ni wanachama au members wote wa jamii forum/jamii Afrika ambao hawachoki kupaza sauti na kukemea udhalimu wote unaofanywa na serikali.

Mashujaa wetu ni waandishi wa habari na watangazaji wa media na mitandao ya kijamii ambao wamesimamishwa ajira zao kwa ajili ya kuandika na kusema ukweli.

Mashujaa wetu ni viongozi wa dini ambao wamesimama na kukemea utekaji na mauaji yanayofanyika.

Mashujaa wetu ni wabunge waliosema ukweli na kutokubaliana na mamlaka ya serikali na kusimamia ukweli bila kuogopa.

Mashujaa wetu ni sisi sote ambao tumekataa uchaguzi haramu na batili wa October 2025 na tunasalimiana kwa salamu ya no reform no election.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…