Hotuba iliyotolewa na Mh. Rais wakati wa kuwaapisha viongozi mapema siku ya jana ni muendelezo wa kasi yake katika kuhimiza utendaji wenye tija kwa watumishi wa umma. Baadhi ya mambo yanayohimizwa na Mh. Rais ni pamoja na ;
1. Utendaji wenye tija kwa watumishi wote wa umma katika Wizara, Taasisi na Mashirika yote. Uwepo wa tathimini na ukaguzi utasaidia kuepusha ubadhirifu na kuchochea ufanisi katika utendaji. Uongozi wa Rais Samia unakwenda kuweka ALAMA ya kudumu.
2. Usimamizi wa sheria na utawala bora - Suala hili muhimu linaendelea kupewa kipaumbele ambapo watumishi wa umma wazembe wanachukuliwa hatua kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha kazi au kuondolewa katika nyadhifa husika.
3. Uwazi na uwajibikaji katika wizara, Taasisi na Halmashauri - Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuongeza uwezo wa kiutendaji wa Mamlaka zinazochunguza na kufanya ufuatiliaji wa mapato na matumizi katika Halmashauri, Taasisi na Mashirika ya umma ili kuhakikisha adhma ya uwazi na uwajibikaji inawekwa katika vitendo.
4. Uongozi thabiti na nia ya dhati katika kuwaletea wananchi maendeleo jumuishi - Maagizo yanayoendelea kutolewa na Rais tayari yameanza kutekelezwa na yanakwenda kuhuisha uchapakazi wa viongozi kwa ngazi zote, na tayari ripoti zinaonyesha kupungua kwa hati chafu katika maeneo mengi.
5. Kuhamasisha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri zote. Wataalam wanasema usipojua unapokwenda tayari umefika mwisho, kitendo cha Mh.Rais kuhimiza umuhimu wa kuwa na malengo katika ukusanyaji ni maono ya kuhamasisha watendaji kufanya kazi kwa weledi zaidi.
6. Kuhamasisha ukamilishaji wa miradi kwa wakati. Halmashauri zilizokuwa na mazoea ya kuchelewa kukamilisha miradi kwa wakati sasa zimefikiwa. Hii inakwenda kuchochea maendeleo sawa sawa na maono ya Mh. Rais Samia. Watanzania tumepata bahati ya kuwa na uongozi imara unaojali suala la uwazi na uwajibikaji kwa vitendo. Shime tuendelee kumuunga mkono Rais Samia kwa uongozi wake imara na wenye tija.