Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akipokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Mwaka 2024/2025; Taarifa ya Utendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); na Taarifa ya Mwaka ya Tathmini ya Utendaji Kazi wa Ununuzi wa Umma, tarehe 30 Machi, 2026, Ikulu Dar es Salaam.
RAIS SAMIA AAGIZA UWAZI MANUNUZI YA UMMA, ASISITIZA UWAJIBIKAJI
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuimarishwa kwa uwazi na uwajibikaji katika manunuzi ya umma, akielekeza taasisi zinazokiuka taratibu kutajwa hadharani na kuchukuliwa hatua.
Akizungumza tarehe 30 Machi, 2026, Ikulu Dar es Salaam, wakati wa kupokea Taarifa ya Mwaka ya Tathmini ya Utendaji wa Ununuzi wa Umma, Rais Samia amesema sehemu kubwa ya fedha za Serikali hutumika katika manunuzi ya umma, hivyo usimamizi madhubuti ni muhimu kulinda rasilimali za wananchi.
“Ripoti zijazo zitaje wazi taasisi zinazofanya vibaya na zinazofanya vizuri, ili kuongeza uwajibikaji na kuchukua hatua stahiki,” amesema Rais Samia.
Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha nidhamu ya matumizi ya fedha za umma na kuhakikisha rasilimali za Serikali zinatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.
Attachments
-
Ripoti_Kuu_ya_Mwaka_ya_Ukaguzi_wa_TAMISEMI_Sekretarieti_za_Mikoa.pdf11.8 MB · Views: 20
-
Ripoti_Kuu_ya_Mwaka_ya_Ukaguzi_wa_Ufanisi_Machi_2026.pdf10.9 MB · Views: 27
-
Ripoti_Kuu_ya_Mwaka_ya_Ukaguzi_ya_Mashirika_ya_Umma_kwa_Mwaka_wa.pdf13.9 MB · Views: 22
-
Ripoti_Kuu_ya_Mwaka_ya_Ukaguzi_ya_Serikali_Kuu_MDA_kwa_Mwaka_wa.pdf19.2 MB · Views: 25
-
Ripoti_Kuu_ya_Mwaka_ya_Ukaguzi_wa_Mifumo_ya_TEHAMA_kwa_Mwaka_wa.pdf5.8 MB · Views: 29