Rais Samia anaposema Kilimo ni kipaumbele cha Serikali yake anamaanisha?

Mtazamo wa mkosaji siku zote ni mtazamo hasi. Badala ya kukaa na kusimuliwa na wakina Mbowe na Lissu kwamba kura zinaibiwa siku moja jiridhishe ukweli wa mtazamo huo.
 
Machinga huwa hawataki kusikia mambo ya kilimo. Wanataka waachwe wauze mpaka barabarani na serikali ihakikishe chakula ni bei rahisi.
Wakienda kulima baada ya muda wanakuja wakubwa kuwafukuza walipokuwa wanalima !! Wataipenda tena kazi ya kilimo. ?!
 
Reactions: Tsh
Kilimo ni muafaka kwa vijana na Taifa katika kuelekea uchumi wa Kati usio tegemezi. Ukiona hivyo serikali inasisitiza umuhimu wa kilimo kutoka awamu mpaka awamu tambua ni mpango wenye nia ya kumkomboa mtanzania kiuchumi.

Dkt.Samia anaposema hivyo juu ya kilimo tambua hakwepeshi ukweli. Kuanzia bei za pembejeo na mbolea, masoko na Bei nzuri sasa ni tumaini la kula mkulima
 
Wakienda kulima baada ya muda wanakuja wakubwa kuwafukuza walipokuwa wanalima !! Wataipenda tena kazi ya kilimo. ?!
Mkuu Tanzania ina mapori mengi sana. Tuachane na hifadhi za taifa na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Matukio ya kufukuzwa kwenye maeneo yasiyo hifadhi ni machache sana au hayapo kabisa.

We sema serikali itengeneze barabara mapori yafikiwe. Maana kuna maeneo kufika ni balaa.
 

Kama ingekuwa ni kweli usemacho kuhusu kilimo, tusingeona watoto wa viongozi wakijazana kwenye ajira za umma, bali wangeenda kulima kwani tayari mtaji wanao. Cha ajabu wanaohubiri kuhusu kilimo, wao na familia zao wako tayari kupora uchaguzi ili waendelee kubaki kwenye ofisi za umma, na sio kukimbilia kwenye kilimo.
 
Hayo yote nayaelewa. Labda wee ndio haujanielewa mimi. Philip Mpango kachaguliwa na nani!? Na akirithi urais atakuwa kachaguliwa kwa kura!?
 
Mtazamo wa mkosaji siku zote ni mtazamo hasi. Badala ya kukaa na kusimuliwa na wakina Mbowe na Lissu kwamba kura zinaibiwa siku moja jiridhishe ukweli wa mtazamo huo.
Kwa akili yako ya kawaida, kama kale ka mkoa kanakoitwa Zanzibar, wamekataa kukaachia kiasi cha kufuta hata uchaguzi mzima, ndio waje waachie hilo pande lote linaloitwa Tanganyika!? Endelea kulala uote zaidi.
 
Machinga huwa hawataki kusikia mambo ya kilimo. Wanataka waachwe wauze mpaka barabarani na serikali ihakikishe chakula ni bei rahisi.
Ndezi sana wale jamaa![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Reactions: Tsh
Kwa akili yako ya kawaida, kama kale ka mkoa kanakoitwa Zanzibar, wamekataa kukaachia kiasi cha kufuta hata uchaguzi mzima, ndio waje waachie hilo pande lote linaloitwa Tanganyika!? Endelea kulala uote zaidi.
Kama unazungumzia habari za uchaguzi wa 2015 sote tulikuwa na akili timamu ya kujua kilichokuwa kinaendelea. Kitendo Cha Hayati Seif kujitangaza mshindi kitendo hicho kilinajisi uchaguzi mzima.
 
Hayo yote nayaelewa. Labda wee ndio haujanielewa mimi. Philip Mpango kachaguliwa na nani!? Na akirithi urais atakuwa kachaguliwa kwa kura!?
Hatuwezi kuitisha uchaguzi kila Rais anapofariki, kwanza ni gharama pia itasababisha kukosekana utulivu wa kisiasa.

Mamlaka inayotambua mamlaka, wajibu, Majukumu na madaraka ya viongozi ni katiba, kama katiba ingesema kiongozi awe anapendekezwa tu bila kupigiwa kura angekuwa ni kiongozi halali kwa mujibu wa katiba.

Ikitokea Philip Mpango kawa Rais ,kwa mujibu wa katiba ni Rais halali kabisa.
 
Wale waliokuwa wanadanganya watanzania wasiojitambua kwa kuzindua viwanda vya zamani kila siku hawakuwa wapigaji?
 
Samia yupo off track acheni kumdanganya hiki kilimo cha peasants hakiwezi kuleta utajiri kwa wananchi wenzetu.
 
Ujinga tu unakusumbua!
Sidhani kama hata shule ya msingi ulimaliza. Kama ulimaliza,ulikuwa unakomea kwenye magofu kuvuta bange!
 
Wakulima Nchini bado hawathaminiwi !! Miaka yote ni slogans tu kwa kwenda mbele !! Ukishaitwa mkulima mdogo hapa Nchini ambao ndio wengi nchini ujue wewe unachukuliwa kama low class citizen !! Utaburutwa mpaka utaichukia kazi ya kilimo !! Hebu jiulize ni kwanini vijana wengi wanakimbia kutoka huko shamba na kukimbilia mijini ?? Wameichukia hiyo kazi kutokana na adha wanazopata wanapokuwa huko mashambani kwao !!
 
Hii nchi imepitia uongo mwingi hadi sasa.

Nyerere: Kilimo ni siasa
Mwinyi: Kilimo ni uti wa mgongo
Mkapa: Kilimo ni biashara
Kikwete: Kilimo Kwanza
Magufuli: Kilimo ni kazi
Samia: Kilimo ni kipaumbele

Ukiona viongozi wanahimiza wananchi kulima, ujue hicho kilimo hakilipi! Nani aliwahimiza wafanyabiashara pale Kariakoo kufanya biashara pale usiku na mchana?
 
Sio mbolea tuu Bali mwaka huu mtafaidi sana..

Yule aliyeharibu uchumi wenu wenu Sasa hayupo .

Rais Samia karudisha Neema [emoji116]

Sio sababu kwamba yule aliharibu uchumi hapana, nae kuna mambo ameyatengeneza ambayo hayajawahi kuwako nchini.

Wote wapo vzr kwa engo tofauti tofaut.!
 
Ndugu P, bajeti ya wizara ya kilimo no shi ngapi vile?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…