Rais Samia anataka nani watolewe rumande?

Rais Samia anataka nani watolewe rumande?

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Mi naona huu msemo wa 'kesi za kubambikizwa' kama mama samia kauchukulia sawa na lugha za vijiweni.

Ni kweli kuna kesi za kubambikiwa ila naamini polisi wenye kubambika wana uwezo wa kupika ushahidi tena kwa kushirikiana na mahakimu na kupiga hela au kuwafunga wahasimu wao. Kwa kesi za kubambikiwa wengi wako gerezani. Ndio wale magufuli aliwakuta wamefungwa kule butimba Mwanza.

Lakini hao wanaomshinikiza Mama wenye kesi za kubambikiwa watolewe binafsi naona wanataka wahalifu wa ufisadi waliyoko rumande ndio waachiliwe.

Wenye shutuma kubwa za ufisadi uchunguzi wa kesi zao wengi kutokana na uwezo kifedha unakua mgumu kwani hata wakiwa lockup mitandao yao inauwezo wa kufanya kazi ya uchunguzi kua ngumu. Badala ya kushinikiza jeshi la polisi kuwaachia watu eti kwa kukosa ushahidi angewahimiza polisi kuongeza maarifa ili kuweza kukamilisha uchunguzi na asitumie lugha kama vile anaingilia kazi ya polisi.

Kama polisi wanasababu ya kumshikilia mtuhumiwa kwa upelelezi wasifanyiwe shinikizo bila sababu ya msingi na wanasiasa Vinginevyo tutakuja juta kwa kuwaachia watu ambao kutokana na wao kua na kesi kumekuepo nidhamu na upungufu mkubwa wa vitendo vya ufisadi nchini.
 
Kwanza inaweza ikasababisha rushwa ndio ikazidi.

Maana unahknga tu ili polisi waseme hawana ushahidi wa kutosha
 
Back
Top Bottom