Rais Samia anatakiwa kuwa makini afanyapo teuzi

Inatakiwa akifa raisi nchi irudi kwenye uchaguzi Ili kupata watu sahihi.Mama atoshi.
Yes na hapo ndio umuhimu wa katiba mpya unapokuja
Makamu wa raisi wengi hawanaga uwezo kabisa
 
Kuna Mmoja namjua Kahonga sana na Karoga mno ila Uteuzi bado umempitia tu Kando ( Kaukosa ) je, huyu Mtu tumsaidiaje Mkuu? Na je, huku Kukosa kote kote kwa Kuhonga na Kuroga 'Kitaalamu' kunaitwaje?
Genta hawa wapuuzi hawawezi kukuelewa my my man
 
Dollar Rajab Kusenge Ameteuliwa Mara Mbili Kuwa Mkurugenzi Kwenye Miji Tofauti

Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotoka Ameteuliwa Kuwa Mkurugenzi wa Mji wa Njombe na Pia Ameteuliwa Kuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Kasulu
 
And pigeni makelele yenu, mama hawezi kujibizana na vilaza
 
Bado nashindwa kuelewa ni either hajauzoea urais au ni kwamba hayupo tu makini.

Moja ya vitu ambavyo ni maajabu sani ni pale unapoona taarifa ya uteuzi kutoka Ikulu ikiwa na makosa kila Mara
Hiyo kutokuwa makini na katabia ka kukosa uadilifu kwa maafisa wetu serikalini ni chanzo kikubwa cha yote haya. Kuna kujuana sana na kubebana. Sisi bado hatujafikia kiwango cha kutazama matokeo ya jambo lilipo mezani, sisi tunajali mahusiano zaidi. Yani hatupo result-oriented. So, hao wanaohusika na vetting ndiyo wana shida, wapigiana pasi tu. Ilipaswa mama awakamue pale wanapomlisha shudu.

Utamaduni pia unatukaba. Tabia yetu hii ya mkubwa hakosei inaturudisha nyuma sana. Kwa staili hii hata ushauri kupokea ni shida. Tazama utamaduni huu wa mkubwa hakosei ukifanya kazi kwa kubofya kiunganishi hiki hapa chini. Cheki kuanzia dakika ya 8:25.

 
Tuwe watulivu jamani, tumpe mama nafasi ya kuweka mambo vzr jamani! mbona viherehere hivyo?
 
Bado nashindwa kuelewa ni either hajauzoea urais au ni kwamba hayupo tu makini.

Moja ya vitu ambavyo ni maajabu sani ni pale unapoona taarifa ya uteuzi kutoka Ikulu ikiwa na makosa kila Mara...
Nina mashaka ata na ujuzi na uzoefu wa kazi kwa wateuliwa, inawezekana watu wengi wenye sifa wanaachwa,nimeona watoto wa vigogo kibao ambao sidhani kama wanafahamu changamoto za wakulima vijijini.
 
Watakuambia yeye analetewa majina

Katiba letu bovu bovu ndio linaendelea kuwabeba.
Unateua kitoto kilichotoka juzi shule hata maziwa hayajauka mdomoni kuwa mkurugenzi wa wilaya nafasi ya utendaji serikalini aisee this is too much

Nafasi kama hizo zinahitaji watu wenye uzoefu wa shughuli za kiserikali kwa miaka 15 consecutively.

Huyo mama yenu hayuko makini

Aliwahi pia mteua yule mpuuzi aliemtishia zitto kumuua eti awe mkurugenzi wa wa tpdc.

Hivi anapitia hayo majini kwa msingi ga Sheria au kwakua yeye ni rais anateua tu anavyojisikia .

Watu wakianza kumzingua na kumdharau asilalame kwamba kuna chokochoko wakati yeye mwenyewe mambo yake yanaendaenda tu .

Nimesikitika Sana
 
HUYU MAMA, YEYE AKISHALETEWA MAJINA

HAANGAIKI WALA HAJISHUGULISHI KUPITIA.

ALISHASEMA, YEYE SIO KAMA MAGUFULI


NDIO MAANA UNAONA ANAFANYA VITU VYA AJABU AJABU KABISA

AIBUUUUU AIBUUUU.
 
tulieni tuliii!!mama anaucheza mwingi.[emoji23][emoji23]
Hahaaaa!!sasa mbona mashambulizi anayaleta langoni kwake!!ana pewa mapande safi badala ya kufunga anaanza kurudisha tena nyuma!!anatupa tabu mabeki
 
Hapo tumepigwa hakuna kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…