Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Mwaka wa ALAT Machi 11, 2025

Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Mwaka wa ALAT Machi 11, 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa 39 wa Mwaka wa Mamlaka ya Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) utakaofanyika Machi 11-12, 2025 jijini Dodoma katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Murshid Ngeze amesema mkutano huo ni wa kawaida ambao hufanyika kila mwaka, ambapo pamoja na mambo mengine, utajadili masuala mbalimbali yanayoendelea katika serikali za mitaa na utafanya tathmini ya mipango na mikakati ya ALAT

Ngeze amesema mkutano huo utahudhuriwa pia na wageni kutoka ndani na nje ya nchi ambapo Rais wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa pamoja na wajumbe wenzake watano watakuwepo katika mkutano huo.

Amesema Katibu wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Afrika Mashariki na mabalozi kutoka mataifa ya nje nao wanatarajiwa kuhudhuria katika mkutano huo.

Ngeze ametumia nafasi hiyo pia kuwakaribisha kuhudhuria mkutano huo wajumbe wa mkutano huo akiwataja wajumbe hao kuwa ni wakurugenzi wa halmashauri zote nchini, mameya wa halmashauri zote nchini, wenyeviti wa halmashauri zote nchini na wabunge (katika kila mkoa mbunge mmoja) pia amewaalika pia wananchi kufuatilia matangazo ya mkutano huo kupitia vyombo vya habari mbalimbali vitakavyorusha matangazo hayo moja kwa moja kutoka jiji Dodoma.
1741433366456.png
 
Back
Top Bottom