Rais Samia anatarajiwa kuzindua daraja la Magufuli, Kigongo - Busisi Juni 19 2025

Tatizo hamfikiri vizuri,maza angeitelekeza ingekamilika?..hiyo sgr huyo Mungu wenu aliiacha 30%,hilo daraja liliachwa %ngapi?
Aitelekeze afanye miradi ipi sasa?

Ripot ya CAG, imekuwa na upotevu wa mabilioni ya shilingi kupotelea kwenye shughuri zisizo rasimi

Hii ni sawa na kusema, umejiwekea mpango na bajeti ya kujenga, baada ya kupata fedha, unampa mkeo akasuke nywele saloon

Hiyo ni akilii au???

No reforms no election
 
Upotevu wa pesa kwenye ripoti ya cag ipo kitambo tangu mkapa,tena ilikua 30%
 
Kibinafsi, mama kaferi pakubwa saaana na hajawahi na wala hatoweza kuvaa gwanda za Magufuli

Mikopo ni mingi na ilihali wamekuwa wakituaminisha makusanyo ni mara mbili ya JPM

Unajiuliza, kama ndivyo, pesa za mikopo zote hizo, ukijumlisha na mapato ya ndani, yoote kweli iishie kwenye miradi hiyo tu na bado haijakamilika?

Mikopo ya mama ni zaidi ya mikopo iliyowahi kukopwa na maraisi wote watano, maana yake, tumgeona ujenzi wa miradi mara mbili zaidi ya miradi iliyowahi kuwepo tangu uhuru

Inakuweje mikopo yote hiyo isitoshee hata kwenye miradi iliyopo?

Utanishawishi kwa lipi kumpigia kura Mama?

No reforms no election
 
Asante kwa taarifa, tunasubiri hotuba yenye vichambo na taarab mpaka tukome
 
Hii ya kupigwa ndege zetu zisitue katika nchi za umoja wa ulaya jamani limekaeje? Mwenye nyuzi kamili, huko mwanza waendelee tu
Mambo ya anga ni ya kitaalamu zaidi na usomi usiotiliwa shaka ndio kigezo muhimu. Sasa ajira za sehemu nyeti kama hizo zinaposhikwa na darasa la saba wenye kadi hai ya CCM, unategemea nini kutoka jumuia za kimataifa? ๐Ÿ˜ฒ
 
Matumizi ni makubwa,
Goli la mama,
Michango makanisani na misikitini,
Ukubwa wa misafara ya viongozi,
Mkuu wa Mkoa tu ziarani gari 60, as if magari yanatumia maji
 
Magugu maji yameondolewa? Kufungua daraja jipya lililozungukwa na uchafu wa mazingira ni kuliaibisha taifa wakati huu ambapo nchi imechafuka.
 
Mpitisheni Saa100 barabara ya Babati kwenda Singida ,kuelekea mwanza ili ajionee ,ubovu wa Barabara nchini.
 
Hizo kazi zote ambazo mhe waziri kazitaja, zote ni matokeo ya JPM, daraja hili, lile la Wami, bwawa la umeme, daraja la Tanzanite zote ni kazi za jembe kutoka Chato. Bado tunasubiri ubunifu wa mama na team yake; kwa haya yaliotajwa hapa tumpatie heshima mwendazake; tuweni wakweli.
 
Sarakasi za hovyo kabisa, daraja linatumika yeye anaenda kuzindua!? ๐Ÿšฎ
Nasikia mnavukaga kwa kuhonga, mama anakwenda kuondoa HONGO ili lianze kutumika officially. But as you said, daraja limeisha siku nyingi sana, hadi Msukuma ali record clip na akatutukana wananchi ๐Ÿ˜ƒ ๐Ÿ˜€ ๐Ÿ˜„ ๐Ÿ˜ ๐Ÿคฃ ๐Ÿ˜‚ alituita "shenzi/washenzi"
 
Angeitelekeza vipi wakati iko kwenye mipango na bajeti ya Serikali? Ule ni wajibu wala sio hisani ya mtu aliyeshika nafasi ya urais. ๐Ÿ˜ณ
Chawa wapumbavu wanafikiri taifa linaongozwa kama unavyoongoza familia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ