Njemba Soro.
JF-Expert Member
- Oct 5, 2013
- 4,280
- 7,485
Acha kuandika ushubwada....Ukweli haujifichi!
Mama apewe tu Maua yake!
Kazi kubwa imefanyika!
Kubwa sanaaaa!
Acha kuandika ushubwada....Ukweli haujifichi!
Mama apewe tu Maua yake!
Kazi kubwa imefanyika!
Kubwa sanaaaa!
1. Mtue Ndoo Mama ( miradi ya Maji Safi nchi nzima)....ajenge ya kwake nayeye
Huu ujinga wote uliouandika hapo unazidiwa na mladi mmoja tu wa Magufuri1. Mtue Ndoo Mama ( miradi ya Maji Safi nchi nzima)
2. Alama za mitaa nchi nzima
3.Mradi wa kuchora upya mipaka ya nchi
4. Mradi wa kununua Umeme kwa bei nafuu kutoka Nje
5. Upanuzi wa mtandao wa njia za Mwendokasi jijini Dar es Salaam
6. Kuwezesha Makampuni binafsi kuuza korosho kwenye SGR (PPP)
7. Mradi wa kuzalisha na kuuza mbegu za avocado kwa ruzuku (PPP)
8. Mradi wa kukusanya mapato ya kusaidia nchi bila shuruti kupitia miamala!
9. Kuaminika kukopesheka kama nchi kiasi cha kuweka utaratibu wa zabuni kwa wanaojisikia wanaweza kutukopesha.
10. 4R za Mama.
11. Mradi wa tiba za kibingwa kutoka Havana -Cuba kwa uratibu wa Wizara ya Nje na balozi wa huko
12....
13....
....
..https://panganidc.go.tz/storage/app/uploads/public/67a/6f3/4c8/67a6f34c8f628188899539.pdf
Objective politicsHuu ujinga wote uliouandika hapo unazidiwa na mladi mmoja tu wa Magufuri
Nimegundua huna unacho kijua kuhusu historia ya hilo daraja.Porojo porojo tu,yaani mkandarasi umounguzie muda kwa miezi 12(mwaka),kwani muda wa mwanzo mlikubaliana vipi?!
Kabla ya ujenzi panakua na uchambuzi yakinifu na kujua lini mradi utaanza na kuisha, huwezi kubaliana nae mradi ukamilike kwa miezi 48,halafu katikati ya kazi umwambie amalize ndani ya miezi 32Nimegundua huna unacho kijua kuhusu historia ya hilo daraja.
Sa kwani si na kwa Magufuli mlisema kakopa kuliko awamu zote au?Hahaaa!
Mkuu, kwani na wewe unabisha kwamba mama kakopa mkopo mkubwa kushinda awamu zote tano zilizomtangulia na kazi aliyo fanya ni ndogo saaana ukilinganisha na waliokopa theruthi ya mkppo wote aliokopa?
Imebidi nikuheshimu kwa sababu ya upande mmoja kuwa mkweliSa kwani si na kwa Magufuli mlisema kakopa kuliko awamu zote au?
Inshu ni kwamba hii nchi alivokufa Magufuli tuliingia cha kike. Sioni mtu pale wa kuvivaa viatu vya Magufuli zile suluari pale zote ni mijambazi tupu. Maza by chance aliukwaa urais na as long as hakuna uharibifu wa kunistua ngoja amalize awamu zake ajisepe ali mradi miradi ya Magufuli inatembea.
By the time anamaliza awamu zake labda mwenye nafuu atakuwa ashajitokeza.
Binafsi ni mmoja wa watu waliokuwa pro-Magufuli kindakindaki na wasiwasi wangu namba moja baada ya mama kumrithi Magufuli ilikuwa je mama ataweza kuendeleza miradi ya Magufuli?
So far naweza kusema maza na Magufuli wanatofautiana parefu sana staili zao kiuongozi lakini kuna kitu kimoja maza hajaniangusha. Miradi ya kimkakati aliyoianzisha Maguguli maza anatembea nayo vizuri sana.
Ni kwa muktadha huo nafikiri anaweza kusimama na kuwa Rais miaka mitano ijayo. Nitampigia kura.
Yes, kuna majambazi yanautamani sana urais na kuna figisu nyingi sana dhidi yake, but kwa wastani na kwa sasa maza anavumilika.
Uchambuzi yakinifu ndio Upembuzi yakinifu au vitu viwili tofauti?.... 😳 🤔Kabla ya ujenzi panakua na uchambuzi yakinifu na kujua lini mradi utaanza na kuisha, huwezi kubaliana nae mradi ukamilike kwa miezi 48,halafu katikati ya kazi umwambie amalize ndani ya miezi 32
Akitoka huko apitilize Saudi Arabia kwenda kuhiji kwenye kaburi la role model wake Iddi Amini Dada.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua daraja la Kigongo- Busisi (KM 3) juu ya Maji linalounganisha wilaya za Misungwi na Sengerema ifikapo tarehe 19 Juni, 2025.
Taarifa hiyo imetolewa na Abdallah Ulega (MB) Waziri wa Ujenzi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katikati ya daraja hilo alipokua akielezea kazi zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi imefanikiwa sana kwenye ujenzi wa madaraja, barabara, vivuko na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.
Ulega amesema pamoja na kukamilika kwa daraja hilo lililogharimu Bilioni 716, serikali ya awamu ya sita imejenga madaraja mengine mengi kama Tanzanite (KM 1) juu ya bahari, Wami (Mita 510), Kitengule (140 Mita), Msingi- Singida (Mita 100).
Amesema, daraja la Kigongo Busisi limejengwa na kampuni ya CCECC kwa kushirikiana na wataalamu wazawa ambao ni wabobevu kwenye kazi hizo na kwamba nchi za jirani wajiandae kwa neema ya barabara hiyo.
Aidha, amebainisha kuwa daraja hilo lina uwezo wa kupitisha magari zaidi ya elfu 20 kwa siku na kwa dakika 3 hadi 5 tu gari itakua imeshavuka kutoka upande mmoja na mwingine.
Vilevile, amefafanua kuwa kwa umahiri wa Rais Samia amefanisha kukamilisha daraja hilo ambalo wakati anaingia madarakani lilikua limejengwa kwa asilimia 25 tu lakini serikali yake imekamilisha asilimia 75 zilizobaki kwa kulipa zaidi ya Bilioni 500.
Vilevile Waziri Ulega amebainisha uwezo wa daraja hilo kuwa lina uwezo wa kubeba gari zenye uzito usiozidi tani 160 kwa wakati mmoja sawa na magari manne yenye tani zaidi ya 45 na amewataka wananchi kulinda rasilimali za daraja hilo na miundombinu mingine kwa manufaa ya watanzania wote.
Sambamba na madaraja amefafanua kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka Kilomita elfu 36 hadi 37. 4 kutokana na kupandishwa kwa hadhi ya barabara kutoka wilaya kwenda kuwa za mikoa huku akizitaja barabara za Mbambabay (KM 66), Kigoma-Kasulu (KM) 100
View attachment 3360818
View attachment 3360820
Kwa maoni yangu... Umezungumza vema sanaBinafsi ni mmoja wa watu waliokuwa pro-Magufuli kindakindaki na wasiwasi wangu namba moja baada ya mama kumrithi Magufuli ilikuwa je mama ataweza kuendeleza miradi ya Magufuli?
So far naweza kusema maza na Magufuli wanatofautiana parefu sana staili zao kiuongozi lakini kuna kitu kimoja maza hajaniangusha. Miradi ya kimkakati aliyoianzisha Maguguli maza anatembea nayo vizuri sana.
Ni kwa muktadha huo nafikiri anaweza kusimama na kuwa Rais miaka mitano ijayo. Nitampigia kura.
Yes, kuna majambazi yanautamani sana urais na kuna figisu nyingi sana dhidi yake, but kwa wastani na kwa sasa maza anavumilika.