Rais Samia anatarajiwa kuzindua daraja la Magufuli, Kigongo - Busisi Juni 19 2025

Rais Samia anatarajiwa kuzindua daraja la Magufuli, Kigongo - Busisi Juni 19 2025

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema jina rasmi la daraja la Kigongo - Busisi atalitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atakapokwenda kwenye uzinduzi rasmi wa daraja hilo.
wACHA WAITE MAJINA HATA YA WATOTO WAO, KUNA SIKU UPUUZI WOTE HUO UTAFUTWA KATIKA USO WA DUNIA
 
Daima litajulikana na kuitwa kingongo busisi hata kama wakilipa jina jina la mtu. Kuna daraja la kigamboni linaitwa nyerere ila linaendelea kuitwa la kigamboni.
 
Watakuwa wametukosea adabu wasukuma kwa kiwango Cha Rami, Bora kama wakikosa Jina waliite Ng'wanamalundi Bridge 🌉
Kwani likiitwa Magufuli bridge kuna tatizo gani? Sio ndio muanzilishi wake au ?
 
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema jina rasmi la daraja la Kigongo - Busisi atalitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atakapokwenda kwenye uzinduzi rasmi wa daraja hilo.
Napendekeza lipewe jina la Daraja la HECHE. kwakuwa mama yetu ni msikivu naimani atalifanyia kazi..
 
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema jina rasmi la daraja la Kigongo - Busisi atalitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atakapokwenda kwenye uzinduzi rasmi wa daraja hilo.
Huyu bibi miradi waanzishe wenzake yeye aite majina
 
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema jina rasmi la daraja la Kigongo - Busisi atalitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atakapokwenda kwenye uzinduzi rasmi wa daraja hilo.
Utadhani alitoa fedha zake mfukoni
 
Watu mnasoma bila kuelewa,heading inasema vingine na ujumbe ni mwingine

Wengi mmekurupuka na kichwa cha habari
 
Athubutu aone nguvu ya sisi watu wa kanda ya ziwa ipoje. Naona sasa wanataka kutuzoea
 
aliite anavyotaka lkn tutakuja kubadilisha kila kitu, hawezi kukalia hapo forever …
 
Daima litajulikana na kuitwa kingongo busisi hata kama wakilipa jina jina la mtu. Kuna daraja la kigamboni linaitwa nyerere ila linaendelea kuitwa la kigamboni.
ujinga wote huu utafutwa wakifa ua kuondka madarakani
 
Tatizo hamfikiri vizuri,maza angeitelekeza ingekamilika?..hiyo sgr huyo Mungu wenu aliiacha 30%,hilo daraja liliachwa %ngapi?
Samia na Serikali yake abuni yake, mbona hatujasikia kuanzishwa kwa miradi mipya ya kimkakati, kila siku tunasikia 'umaliziaji' miradi ya Magufuli?

Serikali ya awamu ijayo itamalizia miradi gani iwapo yeye hajabuni na kuasisi miradi mipya kama aliyoianzisha mwenzaje?

Kusema 'je kama angeitekekeza':
kwa sababu imeanzishwa na Serikali kisha yeye akaitelekeza, ingelikuja kukamilishwa na awamu zinazofuata.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua daraja la Kigongo- Busisi (KM 3) juu ya Maji linalounganisha wilaya za Misungwi na Sengerema ifikapo tarehe 19 Juni, 2025.

Taarifa hiyo imetolewa na Abdallah Ulega (MB) Waziri wa Ujenzi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katikati ya daraja hilo alipokua akielezea kazi zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi imefanikiwa sana kwenye ujenzi wa madaraja, barabara, vivuko na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.

Ulega amesema pamoja na kukamilika kwa daraja hilo lililogharimu Bilioni 716, serikali ya awamu ya sita imejenga madaraja mengine mengi kama Tanzanite (KM 1) juu ya bahari, Wami (Mita 510), Kitengule (140 Mita), Msingi- Singida (Mita 100).

Amesema, daraja la Kigongo Busisi limejengwa na kampuni ya CCECC kwa kushirikiana na wataalamu wazawa ambao ni wabobevu kwenye kazi hizo na kwamba nchi za jirani wajiandae kwa neema ya barabara hiyo.

Aidha, amebainisha kuwa daraja hilo lina uwezo wa kupitisha magari zaidi ya elfu 20 kwa siku na kwa dakika 3 hadi 5 tu gari itakua imeshavuka kutoka upande mmoja na mwingine.

Vilevile, amefafanua kuwa kwa umahiri wa Rais Samia amefanisha kukamilisha daraja hilo ambalo wakati anaingia madarakani lilikua limejengwa kwa asilimia 25 tu lakini serikali yake imekamilisha asilimia 75 zilizobaki kwa kulipa zaidi ya Bilioni 500.

Vilevile Waziri Ulega amebainisha uwezo wa daraja hilo kuwa lina uwezo wa kubeba gari zenye uzito usiozidi tani 160 kwa wakati mmoja sawa na magari manne yenye tani zaidi ya 45 na amewataka wananchi kulinda rasilimali za daraja hilo na miundombinu mingine kwa manufaa ya watanzania wote.

Sambamba na madaraja amefafanua kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka Kilomita elfu 36 hadi 37. 4 kutokana na kupandishwa kwa hadhi ya barabara kutoka wilaya kwenda kuwa za mikoa huku akizitaja barabara za Mbambabay (KM 66), Kigoma-Kasulu (KM) 100
View attachment 3360818
Kimoyomoyo hiyu mama na chawa wake wanatamani kubdili jina liitwe Daraja la Mh. Dr. Mama Samia Sululu Hasan
 
Liitwe Wanu-Mchengelwa Bridge maana nchi hii ni mali yao na sisis ni watwana wao
 
Binafsi ni mmoja wa watu waliokuwa pro-Magufuli kindakindaki na wasiwasi wangu namba moja baada ya mama kumrithi Magufuli ilikuwa je mama ataweza kuendeleza miradi ya Magufuli?

So far naweza kusema maza na Magufuli wanatofautiana parefu sana staili zao kiuongozi lakini kuna kitu kimoja maza hajaniangusha. Miradi ya kimkakati aliyoianzisha Maguguli maza anatembea nayo vizuri sana.

Ni kwa muktadha huo nafikiri anaweza kusimama na kuwa Rais miaka mitano ijayo. Nitampigia kura.

Yes, kuna majambazi yanautamani sana urais na kuna figisu nyingi sana dhidi yake, but kwa wastani na kwa sasa maza anavumilika.
Hiyo miradi ya magu kama ingekuwa haijaanza kutekelezwa wanaipiga stop Walishindwa tu ila hawakupenda hilo daraja lijengwe.
 
Back
Top Bottom