Rais Samia anatoa wapi takwimu za walipakodi?


Kwa Indirect taxation system ilishafutwa TZ
 
Unafikiri kuna anaeweza kujibu haya?...si umeona hata humu watu wamekaa mbali....
Nikuambie ukweli mchungu kwamba bongo ukipatwa na tatizo ni lako binafsi hakuna msaada...futa kabisa
 
Sidhani, labda ungesema tu Mama Samia anaongelea Direct Tax basi ila kuanza kusema mteja akilipa VAT anakua hajalipa kodi huku ukijua kabisa VAT ni shiftable tax kuanzia kiwandani mpaka mteja wa mwisho ile bei anayouziwa inakua VAT inclusive sasa kivipi mteja huyo umwambie hajalipa kodi?

Mfano mwingine ni kodi ya majengo tunalipa kwa luku nako hatulipi kodi? kisa tu mtu hana TIN number au sio muuzaji?
 
Baada kuiuliza ChatGPT kuwa "Je mnunuzi ni mlipa kodi?". Haya ndiyo majibu yake:-
Ndio, mnunuzi anaweza kuwa mlipa kodi kulingana na aina ya biashara na mazingira ya kifedha. Hasa, katika muktadha wa biashara za bidhaa na huduma, kuna aina mbili kuu za kodi zinazoweza kuhusika:

1. Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT): Katika nchi nyingi, mnunuzi hulipa kodi hii wakati wa kununua bidhaa au huduma. Mfano ni katika nchi za EU, ambapo VAT inalipwa na mnunuzi, lakini biashara inayouza bidhaa inakusanya na kulipa kodi hii kwa serikali. Hii inamaanisha kuwa mnunuzi anaiona kama sehemu ya bei ya bidhaa au huduma anayonunua.

2. Kodi ya Mapato: Hii ni kodi inayohusiana na faida inayopatikana na mjasiriamali au biashara. Hata hivyo, mnunuzi mwenyewe haulipi kodi hii moja kwa moja, lakini ikiwa biashara itafanya vizuri, inaweza kuwa na athari kwenye bei za bidhaa na huduma, kwani biashara inaweza kupandisha bei ili kujilipa kwa kodi.

Katika baadhi ya nchi, kama vile Marekani, kuna pia sales tax (kodi ya mauzo), ambayo mnunuzi hulipa moja kwa moja kwa serikali wakati anaponunua bidhaa au huduma.

Kwa hivyo, ingawa mnunuzi ni mlipa kodi kwa upande wa VAT au sales tax, si kila aina ya kodi inahusisha mnunuzi moja kwa moja.
 
Nenda TRA wana definition iliyo clear zaidi.

Consumer sio mlipa kodi.

Mfanyabiashara anaetoza kodi ya VAT kwa niaba yao ndio wanamtambua rasmi.

Wana definition yao ‘taxable person’ ni nani na hii ndio takwimu serikali inayotambua.
 
Walipa kodi ni wengi ila waliosajiliwa kulipa kodi ndio wachache, labda tuseme hivyo
 
"Namuagiza waziri mkuu hili nalo mkaliangalie"
 
Nenda TRA wana definition iliyo clear zaidi.

Consumer sio mlipa kodi.

Mfanyabiashara anaetoza kodi ya VAT kwa niaba yao ndio wanamtambua rasmi.

Wana definition yao ‘taxable person’ ni nani na hii ndio takwimu serikali inayotambua.
Kodi inalipwa na kila mwenye kufanya manunuzi na kupewa stakabadhi, nayo inaitwa VAT, kuna kodi inalipwa na wajasiriamali na wafanya biashara nayo ni kodi ya mauzo, huenda hiyo ndiyo anayozungumzia mheshimiwa raisi.
 
Najua ni ngumu kuelewa.
Hapana, ni rahisi tu kuelewa. Ni wewe unayetaka ku - complicate uelewa wa wengine sahihi walio nao..
Ukinunua kitu muuzaji ndio mlipa kodi sio mnunuzi, yeye ndio mwenye jukumu la KUKATA hiyo pesa uliompa na KUILIPA kwenda TRA. Yeye ndio MLIPA kodi “TAX PAYER.”
Na shida inaanzia hapa..

Si mwisho wa siku, hiyo kodi inajumuishwa kwenye gharama ya bidhaa hiyo na mnunuzi kubeba gharama hiyo..?

Ungesema kuwa mnunuzi analipa "indirect tax" ungeeleweka kirahisi...
Kwenye income kama mshahara wewe ndio mlipa kodi kwa sababu Pesa ZAKO ndio zinakatwa kwenye Stahiki zako au faida kwenye biashara yako. Ukishanunua bidhaa ile pesa si yako ni ya mwenye duka.
You are repeating the same mistake...

Ungesema mwenye duka ni wakala (agent) wa TRA kukusanya kodi toka kwa final consumers ambao ni wateja wa kununua kiberiti, soda, pipi nk ungeeleweka...
Risiti ipo kuhakikisha TRA wanapata rekodi sahihi ya mauzo ya mwenye duka ili yeye alipe kodi.
Na pesa anayolipa kodi huyu mwenye duka naye huwatwisha mzigo huo wanunuzi, final consumers..
Mwenye duka asipopeleka VAT hiyo mwisho wa mwezi ataulizwa yeye kwa nini hajalipa kodi iliopaswa ikatwe kwenye mauzo YAKE.
Atakuwa mwizi kwa sababu atakuwa amekusanya kodi toka kwa wanunuzi (final consumers) halafu yeye akakaa na pesa isiyo yake...!

NOTE: Kwa mifumo ya kodi duniani kote, watu wote wanalipa kodi ikiwemo mimba au mtoto wa mwaka mmoja so long as anatumia bidhaa zozote kv nguo, sabuni..

Kuna direct and indirect taxes. Zote hizi ni kodi na zinakwenda kwenye mfuko wa hazina ya taifa...

Hawa 2,000,000 wanaosemwa kama ndio walipa kodi wanaojulikana ni wale walio kwenye kundi la "direct tax". Wengine wote wako kwenye kundi la "indirect taxe"...

Lakini ni bahati mbaya tu kuwa wengi hata hawajui kuwa nao ni walipa kodi wazuri tena waaminifu kabisa kwa kuwa "indirect tax" haina longolongo, haikwepeki kwa kuwa imo kwenye mahitaji yetu ya kila siku tunayotumia....

Hivyo usitupotoshe brother. Tunaelewa vizuri sana...
 
Najua ni ngumu kuelewa. Ukinunua kitu muuzaji ndio mlipa kodi sio mnunuzi, yeye ndio mwenye jukumu la KUKATA hiyo pesa uliompa na KUILIPA kwenda TRA. Yeye ndio MLIPA kodi “TAX PAYER.”
Ukinunua kitu mnunuzi ndiye mlipa kodi wa VAT na unaikabidhi hiyo kodi kwa muuzaji. Muuzaji ni Tax agent/muwasilisha hiyo kodi.
Muuzaji anakuwa Tax payer pale anapolipa kodi yake ya mapato, sio anapokabidhiwa VAT.
 
Kodi inalipwa na kila mwenye kufanya manunuzi na kupewa stakabadhi, nayo inaitwa VAT, kuna kodi inalipwa na wajasiriamali na wafanya biashara nayo ni kodi ya mauzo, huenda hiyo ndiyo anayozungumzia mheshimiwa raisi.
Mleta mada ametaka kujua raisi Samia anatoa wapi takwimu za walipa kodi. Kwa mtazamo wake yeye kila mwananchi analipia kodi ya VAT halafu serikali ina kuja na idadi ya watu kidogo.

Ndio watu wanamueleza takwimu za serikali za walipa kodi ni biashara na wafanyakazi. Ata kama wewe unanunua bidhaa na kulipa VAT serikali aikuweki kwenye takwimu zao, wao wana hesabu mfanyabiashara aliesajiliwa kulipa VAT ndio mlipa kodi sio wateja wake.
 
Na ukweli ndio huo mnunuzi wa mwisho ndiye anayebeba kodi yote ya ongezeko la thamani na mfanyabiashara ni wakala tu wa kukusanya hiyo kodi na kuipeleka tra
Lakini anayetambulika kama mlipa kodi ni mfanyabiashara
 
Ahsante sana kwa elimu sahihi kwa walipakodi
 
We hulipi kodi una survive tu walipa kodi wapo ndo hao hawazili million 2
 
Na ukweli ndio huo mnunuzi wa mwisho ndiye anayebeba kodi yote ya ongezeko la thamani na mfanyabiashara ni wakala tu wa kukusanya hiyo kodi na kuipeleka tra
Lakini anayetambulika kama mlipa kodi ni mfanyabiashara
Ndiyo maana kukawa na makundi mawili ya walipa kodi;

1. Direct Tax payers

➡Ndani ya kundi hili la kodi, zipo kodi lukuki zinazolipwa moja kwa moja na huyo mlipa kodi.

➡Hili kundi ndilo la hawa wanaotajwa kuwa hawazidi 2,000,000 nchi nzima

2. Indirect Tax payers

➡Hili ni kundi la walipa kodi wengine wote waliobaki kati ya Watanganyika zaidi ya 64,000,000

➡Hawa hulipa kodi zao kupitia bidhaa na huduma wanazonunua na kutumia na ndiyo maana ikaitwa "indirect tax" kwa sababu mnunuzi hailipi yeye moja kwa moja bali inakusanywa na wakala (agent) muuza bidhaa au mtoa huduma fulani...

➡Inapotokea malalamiko kuwa maisha magumu, bidhaa zimepanda bei nk, tusiwalaumu wauzaji na watoa huduma. Wa kulaumiwa ni serikali maana inakuwa imeshawaambia muuza bidhaa na watoa huduma husika kuongeza bei ya bidhaa na huduma zao ili amtwishe mzigo huo mlaji wa mwisho na kisha pesa ya ziada aipeleke serikalini na hivyo kuitwa "kodi"

➡Na serikali nyingi za nchi za dunia ya 3 kama Tanzania macho na akili za kukusanya kodi huzielekeza kwenye category ya walipa kodi hawa kwa sababu ni rahisi na hawawezi kukwepa...

➡Nchi makini duniani zinaboresha na kuinua viwango vya maisha ya watu wao kwa kuhakikisha kuwa nchi inapata mapato yake kupitia rasrimali asili, manufacturing industries, international trade nk na sio kwa kutegemea kodi kupitia bidhaa na huduma muhimu za kila siku kama soda, sabuni, simenti, mabati, petrol, pombe, usafirishaji, maji, umeme nk....

➡Ni ngumu sana kuwatoa watu kwenye umasikini na uduni wa maisha kama nchi itategemea kodi kutoka kwa wananchi wasiozalisha kwa ku - inflate bei ya bidhaa na huduma hizo☝🏻☝🏻muhimu za kila siku eti ili tu serikali ipate kodi...

➡Angalia kwa mfano bei ya bidhaa ya mafuta ya petrol ni kubwa na hupanda mara kwa mara na kuna kodi lukuki ndani yake na zote analipa yule final consumer...

Kwa hiyo kila mtu analipa kodi, asikudanye mtu
 
Direct tax na indirect tax havipo sawa?
 
Mnaweweseka tu km majuha..wewe muulizaji na wajinga wenzio..ni kweli hamuelewi TIN ndio jibu la unachouliza?? utalipa VAT,Income tax na kodi nyingine bila kuwa na TIN?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…