Rais Samia anatumia mbinu zilizomuangusha Joyce Banda Malawi, na yeye anaweza kuanguka 2025

Rais Samia anatumia mbinu zilizomuangusha Joyce Banda Malawi, na yeye anaweza kuanguka 2025

Akifanikiwa kuuza bandari, wananchi wakakichagua CDM 2025, we itakusaidia nn?

Nchi itapata faida Gani ikiwa itakosa power ya idhibiti na mapato ya bandari?

Si sawa kuingiza itikadi za vyama kwenye Issue ya KITAIFA kama bandari.
 
Kamwe tusije kubali tawaliwa na mwanamke



Kwanini ?

Jadilini hoja kama kiongozi wa kawaida bila kujali jinsia yake,

Mkileta Habari ya uanawake zidi ya uanaume tutawashinda kwa hoja mapema sana,

Matharani:

Tangu tupate Uhuru na Kuungana kuliwahi kuongozwa na mwanamke?

Mbona mambo hayajaimarika?

Mbona shida ziko palepale?

Kila Mwaka shida hizi,
Maji shida
Umeme shida,
Barabara shida,
Vifaa tiba shida,
Madawa shida, hospitali kufikika shida,
Elimu kufikika shida,
Vituo vya polisi kufikika shida,

Huduma ya uzazi kwa mama na Mtoto Na wajawazito shida,

N.k.

Viongozi wanaume Ndiyo walotufikisha hapa ambapo adui bado ni umaskini, ujinga, magonjwa, uongozi bora n.k.

Acheni kabisa kujaribu kuleta hoja ya eti sababu ni mwanamke.

Wanawake wanaweza.

Na Samia anaweza [emoji123]

Sema tu Kuna mambo anatakiwa kuyarekebisha yakae sawa.

Anatakiwa awe anashiriki moja Kwa moja kwenye mambo nyeti,

Asitegemee delegation tu,

Asiwaamini sana wasaidizi wake,

Ajue ku-apply Proffesional Sceptism .

Na kuhusu huo mkataba ni kweli hauko vizuri, tulitegemea bunge liisadie Serikali Kwa kuukataa kisha kutoa mapendekezo ya namna uwekwe lakini kwa akili zao wakaupitisha vile.

Walipaswa hata kuunda Kamati ya mapitio (Review Committee) kisha watoe mapendekezo mfano;

1. Mkataba lazima useme ukomo wa muda waziwazi bila kumumunya maneno.

2. Muda wa mkataba usizidi miaka 20 kama ilivyokuwa ule wa Ticts

3. Sheria za kumpa mkataba mwekezaji Zizingatiwe / Zifuatwe kwa uwazi.

4. Ni lini Tanzania utaanza kupokea faida ya huo uwekezaji? Iwekwe wazi tupime kama tunakubali au tukatae.

5. Uwepo mchanganuo wa gharama na faida na jinsi ya kugawana ili tuone tunakubali au kukataa .

6. Watanzania tunaweza wenyewe kuendeleza bandari yetu kwa faida.

N.k.

Washiriki wawe wawe wenye uadilifu mkubwa wasijewakakubali kupewa chochote.

Taarifa ije kusomwa bungeni kwa uwazi ,

Wabunge ni wawakilishi wa wananchi wa Tanzania.

Wasiwasaliti walowatuma kuisimamia serikali.

Wabunge wajisikie kuwiwa kuamua kwa niaba ya watanzania walowatuma kuwa hapo.
 
Pia Joyce Banda hawafanani na sa100!!

Banda alikuwa Binti wa mstaafu wakati sa100 huku hakuwa.
 
Kumbe badari ipo kwenye muungano mbona wazanzibar hatujui ilo
 
Mwaka 2009 Joyce Hilda Banda alijikuta kwenye mshangao wa bahati baada ya kupendekezwa na Rais Bingu wa Mutharika kuwa makamu wa Rais nchini Malawi. Surprise ya namna hii pia ilimkuta Bi. Samia Suluhu Hassan baada ya kupendekezwa na chama chake CCM kuwa mgombea mwenza wa John Pombe Magufuli katika uchaguzi mkuu 2015.

Wote Joyce Hilda Banda na Samia Suluhu Hassan hawajawahi kuwa na ndoto za kuwa makamu wa uRais achilia mbali kuota Urais ambao ulikuja kuwaangukia baadaye kwa nyakati tofauti. Kwa hiyo nafasi hizi za umakamu wa Urais na Urais zimekuja kuwaangukia by surprise bila wao wenyewe kuwa na matarajio hayo.

Tukianza Joyce Hilda Banda mwaka 2012 alijikuta akishika madaraka makubwa ya kuwa Rais wa Malawi baada ya kifo cha ghafla cha Rais Bingu wa Mutharika. Hii tukio halina utofauti na tukio lililomfanya Bi. Samia Suluhu kushika madaraka 2021 baada ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli. Joyce Banda alishika madaraka hayo ikiwa imebakia miaka miwili Malawi kuingia katika uchaguzi mkuu huku Bi. Samia akishika madaraka hayo ikibakia miaka minne nchi iingie katika uchaguzi mkuu.

Hivyo basi Joyce Banda alikuwa na nafasi kubwa ya kujijenga zaidi kisiasa na kijamii kwa kuwa mstari wa mbele kutatua shida na kero za wananchi. Kwa bahati mbaya Joyce alishindwa kutumia nafasi hiyo. Kashfa nzito zikaanza kumwandama mwanamama huyo, kashfa nyingi zikihusisha ufisadi wa mali na pesa za umma pamoja na kuiingiza Malawi katika mikataba mibovu. Wapinzani waliposimama na hoja za ufisadi, silaha pekee ambayo Bi. Joyce Banda aliona inafaa ni jinsia yake. Yeye na wafuasi wake wakasimama na kuwajibu wapinzani kwamba wanamshambulia Joyce na hoja za ufisadi kwa sababu yeye ni mwanamke.

Rais Joyce Banda aligeuza jinsia yake kama ngao na kinga yake dhidi ya tuhuma za ufisadi zilizokuwa zimemwandama. Aliwalipa viongozi wa dini na kimila wamtetee na hoja hiyo ya jinsia. Aliwalipia press conference wafuasi wake watetee jinsia yake badala ya kashfa za ufisadi zilizokuwa zinamwandama, akiamini zitamsaidia uchaguzi mkuu uliokuwa unafuata 2014. Wamalawi hawakuwa wajinga uchaguzi mkuu ulipofika waliamua kumpiga chini na kuchagua upinzani.

Joyce akatumia mamlaka yake ya Urais kufuta matokeo ya uchaguzi kwa sababu hakushinda. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alikataa na kumtangaza aliyeshinda kutoka chama cha upinzani. Waziri wa Joyce ambaye alikuwa kiherehere na tabia mbovu kama alivyo Nape alijiuwa kwa kujinyonga akihofia maisha yake baada Joyce Banda kuanguka.

Miaka 10 baada ya anguko la Joyce Banda anatokea Samia Suluhu Hassan ambaye anatumia njia zilezile zilizomwangusha Rais Joyce Banda za kujibu kashfa zake za uuzaji wa bandari kwa DP World kwa mkataba wa milele. Tangu sakata la kuuza/kukodisha bandari lianze kupamba moto kwa wiki mbili sasa, Rais Samia ameshindwa kujibu hoja za wanaopinga mkataba huo na badala yake anatumia silaha ya Bi. Joyce Banda, ijapo yeye kaiboresha kwa kuongeza udini na Uzanzibari.

Watu mbalimbali wanasiasa na wasiokuwa wanasiasa wanahoji maswali haya matatu kwamba:

1- Kwanini mkataba huo wa kukodisha bandari hauna kikomo cha muda yani ni wa milele?

2- Kwanini mkataba huo hauwezi kuvunjika hata kama wawekezaji hao wana performance ndogo?

3- Kwanini bandari za Zanzibar hazijajumuishwa kwenye mkataba huo na badala yake ni bandari za Tanzania Bara pekee pamoja na kwamba bandari ni sehemu ya mambo yaliyopo kwenye muungano kwa katiba na sheria za nchi?

Huwezi kuamini kwamba pamoja na washauri wa kisiasa alionao Samia, wataalamu na watu wengine wote waliomzunguka, wameshindwa kujibu hoja hizi. Njia pekee aliyoona inafaa ni kujificha kwenye kichaka jinsia, udini na Uzanzibari ili kutafuta uhalali wa kuuza ama kukodisha bandari zetu kwa mikataba mibovu.

Yani unakodisha/kuuza bandari kwa mkataba wa hovyo , watu wanahoji unajibu kwa sababu mimi ni mwanamke ama muislamu au kwa sababu mimi ni Mzanzibar? Kwani ukiwa mwanamke ama Mzanzibar au mwislamu ndio una uhalali wa kuuza nchi kwa kusaini mikataba mibovu? Aliyekuambia dini au jinsia ni kichaka cha kuficha maovu ni nani?

Ukweli ni kwamba njia hii haitamsaidia Samia na badala yake anaenda kuanguka. Miezi 10 sasa Samia anapoteza ushawishi. Mfumuko wa bei, tozo pamoja na kashfa za ufisadi katika serikali yake ni moja ya vitu vinavyompunguzia mvuto kwa wananchi.

Suala la kuuza bandari kwa mkataba wa milele na milele ndio limemchinja mazima Samia. Mkutano alioufanya Mwanza majuzi ulikuwa na watu wachache licha ya kusomba watu kwa malori lakini ni kama alikuwa anahutubia viongozi wa ccm na watumishi wa umma aliotoka nao Dodoma, halmashauri na jiji. Ile ilikuwa ni message kwamba kwa sasa Samia hatakiwi tena. Njia pekee ambayo itamnyanyua Samia kutoka matopeni alikokwama ni kutupilia mbali mkataba huo wa kuuza bandari pamoja na kuwachukulia hatua mafisadi wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG. Tofauti na hapo hawezi kupata kibali tena 2025 hata angetumia majeshi. Ushauri huu ni chungu kama sumu ya nyigu lakini ukifuatwa ni mtamu kama asali.

Mdude Nyagali 7 x 70.View attachment 2661162
Ipo tofauti kubwa kati ya Malawi na Tanzania, Malawi rais huchaguliwa kwa wingi wa kura halali wakati Tanzania aliyeko madarakani anajimegea bonge la kura na ikiwezekana zote, balozi Karume alijisemea wazi kuwa CCM haijawahi kushinda uchaguzi.
 
Ipo tofauti kubwa kati ya Malawi na Tanzania, Malawi rais huchaguliwa kwa wingi wa kura halali wakati Tanzania aliyeko madarakani anajimegea bonge la kura na ikiwezekana zote, balozi Karume alijisemea wazi kuwa CCM haijawahi kushinda uchaguzi.
Ni Kweli, lakini pia Si Kweli ktk angle ingine.

Ingekuwa Watawala wanategemea wizi wa kura pekee, wasingekuwa wanaoenda kukopa billions of money kuhonga wapigajura na kufanikisha logistics za compain Nchi nzima.

Sifa , Image ya mgombea Urais wa CCCM Huwa ni mtaji mkubwa, mengine hufuata,

Ndomana waliachana na Lowwarsa baada ya kumchafua sana Ili kumfichia Aibu mkubwa.

Kuna Kila dalili aliyepo HATOGOMBEA Kwa scandal kubwa zinazomwandana.

Tusubiri.
 
Ni Kweli, lakini pia Si Kweli ktk angle ingine.

Ingekuwa Watawala wanategemea wizi wa kura pekee, wasingekuwa wanaoenda kukopa billions of money kuhonga wapigajura na kufanikisha logistics za compain Nchi nzima.

Sifa , Image ya mgombea Urais wa CCCM Huwa ni mtaji mkubwa, mengine hufuata,

Ndomana waliachana na Lowwarsa baada ya kumchafua sana Ili kumfichia Aibu mkubwa.

Kuna Kila dalili aliyepo HATOGOMBEA Kwa scandal kubwa zinazomwandana.

Tusubiri.
Mgombea wa CCM hutumia pesa za serikali na hakuna wa kumhoji kama kanuni inavyotaka.
 
Mgombea wa CCM hutumia pesa za serikali na hakuna wa kumhoji kama kanuni inavyotaka.
Ndo nasema, hata kama wanaiba kura kamwe usitegemee vilaza kama Mwigu, kipara na pena kutoboa na kupewa tiketi kugombea.

Huwa wako makini sana na mgombea Urais wao!!
 
Ndo nasema, hata kama wanaiba kura kamwe usitegemee vilaza kama Mwigu, kipara na pena kutoboa na kupewa tiketi kugombea.

Huwa wako makini sana na mgombea Urais wao!!
Wangekuwa makini sana kwenye kimchagua mgombea urais kisingetokea mgongano uliotokea kati Lowassa na Magufuli, walipoingia ukumbini huko Dodoma JK alijua Lowassa huku wengine wakijua ni Magufuli! Huyo Magufuli naye bado taarifa zake binafsi hazikuwa sahihi sana.
 
Yaliyotokea Malawi Nigeria na zambia ndio yanaenda tokea 2025.
Rais kufia madarakani makamu anashika hadi uchaguzi mkuu then makamu anapigwa chini upinzani wanachukua kisha chama cha ukombozi kinafikia mwisho.
 
Banda kaangushwa kwa ishu ya kupromote ushoga na kutaka kuingiza Malawi kwenye vita ya kugombea ziwa nyasa na Tanzania.
Wamalawi wakasema watz ni ndugu zetu wa damu hatupo tayari kuingizwa kwenye vita na ndugu zetu.
Hivyo wakaadhimia kumponda nyoka kichwa na ajenda ya ushoga ikafa plus chokochoko ya kugombea ziwa ikafa
 
Back
Top Bottom