Rais Samia anatumia mbinu zilizomuangusha Joyce Banda Malawi, na yeye anaweza kuanguka 2025

Akifanikiwa kuuza bandari, wananchi wakakichagua CDM 2025, we itakusaidia nn?

Nchi itapata faida Gani ikiwa itakosa power ya idhibiti na mapato ya bandari?

Si sawa kuingiza itikadi za vyama kwenye Issue ya KITAIFA kama bandari.
 
Kamwe tusije kubali tawaliwa na mwanamke



Kwanini ?

Jadilini hoja kama kiongozi wa kawaida bila kujali jinsia yake,

Mkileta Habari ya uanawake zidi ya uanaume tutawashinda kwa hoja mapema sana,

Matharani:

Tangu tupate Uhuru na Kuungana kuliwahi kuongozwa na mwanamke?

Mbona mambo hayajaimarika?

Mbona shida ziko palepale?

Kila Mwaka shida hizi,
Maji shida
Umeme shida,
Barabara shida,
Vifaa tiba shida,
Madawa shida, hospitali kufikika shida,
Elimu kufikika shida,
Vituo vya polisi kufikika shida,

Huduma ya uzazi kwa mama na Mtoto Na wajawazito shida,

N.k.

Viongozi wanaume Ndiyo walotufikisha hapa ambapo adui bado ni umaskini, ujinga, magonjwa, uongozi bora n.k.

Acheni kabisa kujaribu kuleta hoja ya eti sababu ni mwanamke.

Wanawake wanaweza.

Na Samia anaweza [emoji123]

Sema tu Kuna mambo anatakiwa kuyarekebisha yakae sawa.

Anatakiwa awe anashiriki moja Kwa moja kwenye mambo nyeti,

Asitegemee delegation tu,

Asiwaamini sana wasaidizi wake,

Ajue ku-apply Proffesional Sceptism .

Na kuhusu huo mkataba ni kweli hauko vizuri, tulitegemea bunge liisadie Serikali Kwa kuukataa kisha kutoa mapendekezo ya namna uwekwe lakini kwa akili zao wakaupitisha vile.

Walipaswa hata kuunda Kamati ya mapitio (Review Committee) kisha watoe mapendekezo mfano;

1. Mkataba lazima useme ukomo wa muda waziwazi bila kumumunya maneno.

2. Muda wa mkataba usizidi miaka 20 kama ilivyokuwa ule wa Ticts

3. Sheria za kumpa mkataba mwekezaji Zizingatiwe / Zifuatwe kwa uwazi.

4. Ni lini Tanzania utaanza kupokea faida ya huo uwekezaji? Iwekwe wazi tupime kama tunakubali au tukatae.

5. Uwepo mchanganuo wa gharama na faida na jinsi ya kugawana ili tuone tunakubali au kukataa .

6. Watanzania tunaweza wenyewe kuendeleza bandari yetu kwa faida.

N.k.

Washiriki wawe wawe wenye uadilifu mkubwa wasijewakakubali kupewa chochote.

Taarifa ije kusomwa bungeni kwa uwazi ,

Wabunge ni wawakilishi wa wananchi wa Tanzania.

Wasiwasaliti walowatuma kuisimamia serikali.

Wabunge wajisikie kuwiwa kuamua kwa niaba ya watanzania walowatuma kuwa hapo.
 
Pia Joyce Banda hawafanani na sa100!!

Banda alikuwa Binti wa mstaafu wakati sa100 huku hakuwa.
 
Kumbe badari ipo kwenye muungano mbona wazanzibar hatujui ilo
 
Ipo tofauti kubwa kati ya Malawi na Tanzania, Malawi rais huchaguliwa kwa wingi wa kura halali wakati Tanzania aliyeko madarakani anajimegea bonge la kura na ikiwezekana zote, balozi Karume alijisemea wazi kuwa CCM haijawahi kushinda uchaguzi.
 
Ipo tofauti kubwa kati ya Malawi na Tanzania, Malawi rais huchaguliwa kwa wingi wa kura halali wakati Tanzania aliyeko madarakani anajimegea bonge la kura na ikiwezekana zote, balozi Karume alijisemea wazi kuwa CCM haijawahi kushinda uchaguzi.
Ni Kweli, lakini pia Si Kweli ktk angle ingine.

Ingekuwa Watawala wanategemea wizi wa kura pekee, wasingekuwa wanaoenda kukopa billions of money kuhonga wapigajura na kufanikisha logistics za compain Nchi nzima.

Sifa , Image ya mgombea Urais wa CCCM Huwa ni mtaji mkubwa, mengine hufuata,

Ndomana waliachana na Lowwarsa baada ya kumchafua sana Ili kumfichia Aibu mkubwa.

Kuna Kila dalili aliyepo HATOGOMBEA Kwa scandal kubwa zinazomwandana.

Tusubiri.
 
Mgombea wa CCM hutumia pesa za serikali na hakuna wa kumhoji kama kanuni inavyotaka.
 
Mgombea wa CCM hutumia pesa za serikali na hakuna wa kumhoji kama kanuni inavyotaka.
Ndo nasema, hata kama wanaiba kura kamwe usitegemee vilaza kama Mwigu, kipara na pena kutoboa na kupewa tiketi kugombea.

Huwa wako makini sana na mgombea Urais wao!!
 
Ndo nasema, hata kama wanaiba kura kamwe usitegemee vilaza kama Mwigu, kipara na pena kutoboa na kupewa tiketi kugombea.

Huwa wako makini sana na mgombea Urais wao!!
Wangekuwa makini sana kwenye kimchagua mgombea urais kisingetokea mgongano uliotokea kati Lowassa na Magufuli, walipoingia ukumbini huko Dodoma JK alijua Lowassa huku wengine wakijua ni Magufuli! Huyo Magufuli naye bado taarifa zake binafsi hazikuwa sahihi sana.
 
Yaliyotokea Malawi Nigeria na zambia ndio yanaenda tokea 2025.
Rais kufia madarakani makamu anashika hadi uchaguzi mkuu then makamu anapigwa chini upinzani wanachukua kisha chama cha ukombozi kinafikia mwisho.
 
Banda kaangushwa kwa ishu ya kupromote ushoga na kutaka kuingiza Malawi kwenye vita ya kugombea ziwa nyasa na Tanzania.
Wamalawi wakasema watz ni ndugu zetu wa damu hatupo tayari kuingizwa kwenye vita na ndugu zetu.
Hivyo wakaadhimia kumponda nyoka kichwa na ajenda ya ushoga ikafa plus chokochoko ya kugombea ziwa ikafa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…