Rais Samia anavyokimbiza mradi wa mwendokasi ili kuondoa foleni Dar es Salaam

Rais Samia anavyokimbiza mradi wa mwendokasi ili kuondoa foleni Dar es Salaam

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Na Bwanku M Bwanku.

Kwenye Gazeti la Tanzania Leo nimefanya uchambuzi wangu kuhusu mradi mkubwa wa magari yaendayo haraka (DART) unavyokimbia kwenye awamu zingine Jijini Dar es Salaam. Wote tunajua namna Dar ilivyo na foleni kubwa, Sasa Serikali ya Rais Samia inaendelea kukimbiza mradi huu wa magari ya mwendokasi ili kuondoa foleni Dar na watu waharakishe shughuli zao.

Hakuna kilichosimama, chini ya Serikali ya Rais Samia inaendelea na awamu ya pili, ya tatu mpaka ya 6 kuelekea Mbagala, Gongolamboto na kuendelea ili kuondoa foleni Dar na kurahisisha kwa haraka shughuli za kila siku za wananchi. Soma Makala yangu hii uone chini ya Rais Samia mradi huu wa magari ya mwendokasi unavyokimbia na unavyoenda kulifungua zaidi Jiji la Dar kibiashara na kiuchumi. Nani kama Mama?
Screenshot_20230403-142854.png
 
Route ya gongo la mboto hauna utakuwa na.maana mpaka utakapofika chanika maana nako kushatapika
 
Kukimbiza maana yake ni nini?

kama kuna mkataba na mkandarasi may be kujenga kwa miaka 2 yeye anakimbia kwa kupunguza iwe mwaka mmoaja ?

au na yeye anabeba beleshi kusukuma kifusi
 
Wanafiki wakubwa, mmetia bichwa Mama wa watuz alafu huku mnaliibia Taifa.

Sasa mmeanzan tena sifa zenu nyambafu
 
Ukiona mtu anakupamba na kukusifia pasi na sababu stuka huyo atakupiga na kitu kizito kichwaani Soon alisema mh. Magu alipokua anakabidhiwa udaktari wa heshima pale UDOM
 
Back
Top Bottom