benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi karibuni lilipitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23. Sote tunafahamu hii ndio bajeti ya kwanza ambayo maandalizi yake yote yamefanyika chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu tofauti na bajeti ya 2021/22 ambayo Rais aliingia madarakani kwenye robo ya mwisho ya mwaka wa fedha 2020/21.
Katika bajeti ya 2022/23 tumeshuhudia ongezeko kubwa la bajeti ambayo imefikia Trilioni 41.48. Hili ni ongezeko kubwa sana ukilinganisha na bajeti ya mwaka uliopita wa fedha 2021/22 ambayo ilikuwa ni Trilioni 36.3 huku mwaka 2020/21 ikiwa ni Trilioni 34.88. Katika bajeti hiyo mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Shilingi Trilioni 28.02 sawa na 67.5% ya bajeti yote.
Wizara ya Kilimo ni moja ya sekta zilizotajwa kuwa za kipaumbele kuchochea ukuaji wa uchumi, Ajira na Kipato na zimetengewa fedha nyingi kwenye bajeti.
Bajeti ya kilimo kwa mwaka huu wa fedha imeongezeka kwa takribani asilimia 371 hadi kufikia Sh. Bilioni 954 kutoka shilingi Bilioni 229 Bajeti ya Mwaka 2020/21 hili ni jambo la kupongezwa sana.
Rais Samia kipekee kupitia ongezeko la bajeti hii ameonesha dhamira ya kufikia ukuaji wa zaidi ya 10% katika sekta ya kilimo ifikapo 2030 ikizingatiwa sekta ya kilimo ni mwajiri mkuu wa nguvukazi ya Taifa na mchangiaji mkuu katika pato la Taifa.
Serikali pia ipo katika mpango wa ujenzi wa kiwanda kikubwa zaidi Afrika Mashariki cha usindikaji wa mafuta ya kula ambacho kitahakikisha upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya kuongeza thamani kwenye bidhaa za kilimo hadi 100% ifikapo 2030 na kuongezeka uzalishaji kwenye kilimo cha umwagiliaji kutoka 10% hadi 50%.
Bajeti ya Kilimo imeonesha dhamira ya Kuongeza idadi ya mashamba makubwa (Block Farms/Commercial Farms) kutoka 110 kwa mwaka 2020 hadi 10,000 mnamo mwaka 2030 kwa kuzingatia michikichi na kilimo cha alizeti
Kubwa zaidi lililonivutia katika bajeti hii ni kuja na mkakati utakaowasaidia wakulima katika kipindi hiki ambacho kuna mfumuko mkubwa wa bei duniani kote kutokana na sababu mbalimbali.
Bajeti ya kilimo imeanisha kwamba:
“Katika kukabiliana na athari za kupanda kwa bei ya mbolea duniani, Wizara itaimarisha mfumo wa utoaji ruzuku ambapo inatarajia kutumia SHILINGI BILIONI 150KUTOA RUZUKU YA MBOLEA KWA MAZAO YOT”, Kwa kipekee mfumo wa utoaji wa ruzuku utawalenga wazalishaji wa ndani"
KAMA UTEKELEZAJI WA BAJETI HUU UTAFANIKIWA JAPO KWA ASILIMIA 80, BASI HAKIKA NCHI YETU ITAPIGA HATUA KUBWA SANA