Rais Samia anawaapisha viongozi wateule Ikulu ndogo ya Tunguu-Zanzibar leo Desemba 10, 2024

Rais Samia anawaapisha viongozi wateule Ikulu ndogo ya Tunguu-Zanzibar leo Desemba 10, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

Rais Samia anawaapisha Viongozi Wateule Ikulu Ndogo ya Tunguu Zanzibar, leo tarehe 10 Disemba, 2024.

  • Akiwa anazungumza katika uapisho wa mawaziri, Rais Samia amedokeza kuwa ni viongozi tu ndo wamebadilishiwa majukumu lakini serikali ni ile ile.

  • Pia Rais Samia alitumia hotuba yake kutoa sababu za kwanini aliamua kuifumua Wizara ya Habari na kuirudisha kuifanya kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kusema kuwa, kwa sasa Serikali imejipanga kuboresha sekta ya mawasiliano nchini na ndio maana jukumu la mawasiliano na ndio maana amefumua Wizara hiyo.

  • Aidha Rais Samia alimpongeza Hamad Masauni kwa kazi nzuri aliyoifanya katika Wizara ya Mambo ya Ndani na kudokeza kuwa amemuweka kwenye nafasi yake mpya mahususi kwa ajili ya kusaidia sekta ya mazingira nchini na kudumisha masuala ya Kimuungano

  • Rais Samia pia alitumia hotuba yake, kutangaza kuwa amemteua Profesa Janabi kuwa mgombea anayeiwakilisha Tanzania kwenye kinyang'anyiro cha Ukurugenzi wa Shirika la WHO


 
Janabi atashindwa kura.Eti wanamuandaa akagombee WHO Africa.Hana ile attirance ya watu wampigie kura Ninamuona hayupo Humble.Ila bora wapeleke jina wajue feeling ya kushindwa pia.
Halafu hii imekaaje kumpendekeza mgombea kabla hata uchaguzi haujatangazwa? Je, WHO wakighaili kufanya uchaguzi?

Yani huyu mama anachowaza ni uchaguzi tu. Ndio maana anagawa pikipiki za kampeni SSH 2025; ilihali hata mimi nina mpango wa kuchukua fomu ndani ya chama
 
Wakuu,

Rais Samia anawaapisha Viongozi Wateule Ikulu Ndogo ya Tunguu Zanzibar, leo tarehe 10 Disemba, 2024.



Yaani untumia gharama kujaza viongozi wote wakuu kwa ajili ya hafla fupi tu ya uapisho. Hawa ni watu waliojiweka madarakani na wana uhakika wananchi hawawezi kuwawajibisha. Hawana uchungu hata kidogo na kodi zetu. Wakitoka hapo wanaenda kusaidiwa kujenga matundu ya vyoo na wahisani wakati matundu kibao ya vyoo mashuleni yangepatikana kwenye hafla kama hizi zisizo na tija yeyote
 
Back
Top Bottom